Kwanini kesi ya Deus Soka inatumiwa na dola isisikilizwe mapema
Ni kwamba inatumika na dola kutishia raia kuwa usishiriki siasa. Kwa Deus Soka na wenzie kutokuwa mikononi mwa polisi serikali inasema haihusiki na inajiburuza kufanya uchunguzi.
REJEA MWAKA 2023
MAHAKAMA YAIBANA POLISI KWA KUKAA NA MTUHUMIWA SIKU 18
Mahakama Kuu, Masjala ya Dar es Salaam imeliamuru Jeshi la Polisi nchini kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Nezak Investment Limited, Zakaria Kapama ambaye yuko mahabusu kwa siku 18 bila kufikishwa kortini.
Kifungu cha 32 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya mwaka 1985 na marekebisho yake, kinataka mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24, isipokuwa kwa makosa yale ambayo adhabu yake inakuwa ni kunyongwa hadi kufa.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, ikiwa haiwezekani, basi mtuhumiwa aachiwe kwa dhamana, lakini kumekuwa na kilio katika vituo mbalimbali vya polisi kuwa, baadhi ya watuhumiwa husota muda mrefu mahabusu za polisi bila kufikishwa kortini kwa wakati.
Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Wilfred Dyansobera, baada ya maombi ya jinai yaliyowasilishwa mahakamani na Kapama dhidi Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Oysterbay, Kamanda wa Polisi Kinondoni na Inspekta Jenerali wa Polisi.
Katika maombi hayo namba 132 ya 2023, Kapama alimuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kama mjibu maombi wa nne na aliiomba Mahakama kuwaagiza wajibu maombi hao kumwachia wanavyomshikilia au kumweka kizuizini isivyo halali.
Pia, aliomba kama hawatamwachia, basi Mahakama iwaamuru wajibu maombi kufika mahakamani kueleza sababu za kumnyima uhuru wake, kumzuia, kumuweka kizuizini nje ya muda wa kisheria na kuwataka kutimiza majukumu kwa mujibu wa sheria.
Kupitia kwa wakili wake, Deogratias Butawantemi, Kapama ambaye pia kampuni yake inamiliki KP Motors inayohusika na uagizaji wa magari, anaeleza Septemba 29 mwaka huu 2023 alikamatwa na polisi na kuwekwa mahabusi Kituo cha Oysterbay.
Kwa mujibu wa hati ya kiapo chake, hadi anawasilisha maombi hayo juzi alikuwa bado anashikiliwa kituoni hapo bila kupewa dhamana wala kufikishwa mahakamani, kama sheria za nchi zinavyoelekeza.
Akitoa uamuzi wa maombi hayo jana, Jaji Dyansobera aliwaagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Oysterbay na wajibu maombi wenzake, kuhakikisha mleta maombi huyo anafikishwa mbele ya Mahakama na amri hiyo itekelezwe sio zaidi ya siku ya leo (Jumatano).
(Imeandikwa na Daniel Mjema)
Soma Hukumu : Ya Jaji Wilfred Dyansobera, wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Source :
Zakaria Anthony Kapama vs. Officer Commanding Station Oyterbay (OCS) & 3Others) (Misc. Criminal Application No. 132 of 2023) [2023] TZHC 21830 (17 October 2023)