Je, serikali inashindwa kutoa mikopo ya trekta kwa wakulima wajasiriamali?

Emmanuel Mkwama

Senior Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
166
Reaction score
124
Wanajukwaa heri nyingi ziwafikie. Dhumuni la kuja kwenu leo, ni kujaribu kushare nanyi kuhusu inshu ya serikali yetu kushindwa kutoa mikopo ya tractor kwa wajasilia mali wakulima wenye kumiliki mashamba kwanzia heka 10 na kuendelea.

Natumai hili swala ni zuri sana kama wenye kulifanya hili kutolifanya kibinafsi zaidi. Nikiwa na maana kuacha siasa kutumika ili malengo na nia ya dhati katika kufanikisha suala hili.
 
Kama wameshindwa maji safi, umeme wa uhakika, madarasa ya watoto, wataweza kununua matrekta mkuu, labda ungesema viongozi wopewe v8 hilo linawezekana
 
Wanajukwaa heri nyingi ziwafikie. Dhumuni la kuja kwenu leo,ni kujaribu kushare nanyi kuhusu inshu ya serikali yetu kushindwa kutoa mikopo ya tractor kwa wajasilia mali wakulima wenye kumiliki mashamba kwanzia heka 10 na kuendelea.

Natumai ili swala ni zuri sana kama wenye kulifanya hili kutolifanya kibinafsi zaidi. Nikiwa na maana kuacha siasa kutumika ili malengo na nia ya dhati katika kufanikisha swala hili.
Wajasilia mali = wajasiriamali, kwanzia = kuanzia. Achana na kuwaza mikopo ambayo itakufanya ulipe bei hata mara tatu ya bei ya kawaida sokoni. Jipinde ujiagizie trekta lako mwenyewe.
 
Shukrani kwa kunirekebisha mkuu,kikubwa dhumuni langu lifike na ninashukuru kwa kunihamasisha katika kujipanga ili ninunue la kwangu.

Mkuu changamoto inakuja uwezo tunatofautiana na vyanzo vya mapato pia tunatofautiana. Kuna wengine wanapata fursa nyingi kwasababu baba,mama ama mjomba wapo na nafasi nzuri serikalini. Tofauti na mimi nitoke niende shambani nikatafute chochote kile ili familia ipate chochote kitu. Tena shambani kwenyewe itanibidi iwe msimu hadi msimu.

Tractor zinaanzia kwanzia million 35 na kuendelea,je unahisi kwa mtu wa hali yangu ya chini naweza kumudu hizi gharama mkuu? Lakini ukihitaji tractor nzuri Zaid zipo bei imechangamka kidogo 46....50 na kuendelea.

Ila kama kunakuwa na uwezekano wa kutoa mikopo kama ile ya mikopo ya boda boda na bajaji zinavyotolewa inaweza kuwa msaada kwa watu wengi sana.
 
Shukrani kwa kunirekebisha mkuu,kikubwa dhumuni langu lifike na ninashukuru kwa kuniamasisha katika kujipanga ili ninunue la kwangu.

Mkuu changamoto inakuja uwezo tunatofautiana na vyanzo vya mapato pia tunatofautiana. Kuna wengine wanapata fursa nyingi kwasababu baba,mama ama mjomba wapo na nafasi nzuri serikalini. Tofauti na mimi nitoke niende shambani nikatafute chochote kile ili familia ipate chochote kitu. Tena shambani kwenyewe itanibidi iwe msimu hadi msimu.

Tractor zinaanzia kwanzia million 35 na kuendelea,je unahisi kwa mtu wa hali yangu ya chini naweza kumudu hizi gharama mkuu? Lakini ukihitaji tractor nzuri Zaid zipo bei imechangamka kidogo 46....50 na kuendelea.

Ila kama kunakuwa na uwezekano wa kutoa mikopo kama ile ya mikopo ya boda boda na bajaji zinavyotolewa inaweza kuwa msaada kwa watu wengi sana.
Mkuu kaa chini piga hesabu zako vizuri. Kama mkopo ndo rahisi kwako chukua. Ila kwa uzoefu wangu ni kwamba kama unaanza usichukue kabisa mkopo. Anza na kilicho ndani ya uwezo. Bora hata baadae ukaja kukopa hela ukaongezea na ulicho nacho kisha ukanunua trekta kuliko kuchukua trekta la mkopo kwa bei mara 2 zaidi.
 
Nenda bank ,Mimi nikupe? Ujamaa umewaharibi sana nyie Kila kitu mnataka mtafuniwe
Mbona kama umepaniki mkuu,tupo hapa ili kuelimishana. Ndiyo maana nikakuomba kama unauelewa kuhusiana na mikopo ya kilimo,ni heri ungetupa elimu kwanza hapa ili kupa elimu kwanza kabla ya kusogelea taasisi yenyewe kwanza. Kwani si unakumbuka ule usemi ukitaka kuruka agana na nyonga kwanza.
 
Usumbufu usio na Tija Huwa sitaki
 
Wajasilia mali = wajasiriamali, kwanzia = kuanzia. Achana na kuwaza mikopo ambayo itakufanya ulipe bei hata mara tatu ya bei ya kawaida sokoni. Jipinde ujiagizie trekta lako mwenyewe.
Itachukua miaka mingi sana.
Tungekuwa na akili tungeanzisha mfuko wa kata ili kujichanga na kupata trekta la kata ambalo litalima kwa bei nafuu au kwa mkopo nsimu wa mavuno mkulima analipa gharama ambapo hio hela inaendeleza kununua matrekta mengine.
Baada ya muda wakulima wanaweza kuja kuwa na uwezo wa kununua matrekta yao binafsi .
Kipindi cha kikwete zilitolewa kubota siijui mradi uliishia wapi!
Vile vile tusisahau kuwa kipindi cha nyuma zilikuwepo trekta za kijiji ila wajanja walifilisi.
 
Sio kwa Tanzania hii ndugu. Hela za huo mfuko zitaliwa tu na wachache. Yaani hakuna namna yoyote itakayofanya zisiliwe.
 
Itachukua miaka mingi sana.
Tungekuwa na akili tungeanzisha mfuko wa kata ili kujichanga na kupata trekta la kata ambalo litalima kwa bei nafuu au kwa mkopo nsimu wa mavuno mkulima analipa gharama ambapo hio hela inaendeleza kununua matrekta mengine.
Baada ya muda wakulima wanaweza kuja kuwa na uwezo wa kununua matrekta yao binafsi .
Kipindi cha kikwete zilitolewa kubota siijui mradi uliishia wapi!
Vile vile tusisahau kuwa kipindi cha nyuma zilikuwepo trekta za kijiji ila wajanja walifilisi.
Zile tractor nazi kumbuka mkuu. Kiukweli sela ya nchi na chama ni kilimo lakini vitendo na maneno ni tofauti,ama laa njia moja wapo ya wauni wachache kupiga deal.
 
Tena ni njia yao nyepesi zaidi maana karibia asilimia tisini ya vijana nchi nzima wenye nguvu na wasaa wa kuhangaika na kilimo, wako barabarani wanaendesha bodaboda na bajaj huku wakijiaminisha kwamba kazi ya kilimo ni ya mtanzania maskini kabisa wa kijijini ndani ndani huko!

Na kwa vile hao wahuni ndio viongozi wa hizo departments za kuhusika na kilimo na elimu kuhusu faida za kilimo na kukumbushia sera na mipango ya serikali kuhusu kilimo, basi ndio tupo hapa tulipo.

Laiti kama program ya Kilimo Kwanza ingesimamiwa kama ambavyo ilihubiriwa tofauti na makusudio ya unyonyaji, tungekua ndio wasambazaji wakuu wa chakula Africa nzima.

Hatujachelewa lakini, japo huu mpango wa sasa ndio wamepuyanga haswaa!
 
Back
Top Bottom