PostGE2025 Je, Serikali inayaendea maridhiano kwa maslahi ya Taifa? Kauli za viongozi kuhusu maridhiano zinabeba dhamira ipi?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

JF Analyst

Member
Joined
Jan 30, 2025
Posts
11
Reaction score
14
Wimbo wa maridhiano umekuwa ukisikika masikioni mwa Watanzania kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025. Hata hivyo, hadi sasa umebaki kuwa kitendawili kinachohitaji kuteguliwa.

Wapo walioimba wimbo huu kabla ya uchaguzi. Wanaharakati, baadhi ya viongozi wa dini na wanasiasa walitoa wito wa kuwepo kwa maridhiano, lakini wito huo ulibaki kuwa sauti isiyotekelezwa kwa vitendo.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lilishauri kuwepo kwa maridhiano kabla ya uchaguzi. Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nao ulipendekeza kufanyika kwa muafaka wa kitaifa kabla ya uchaguzi. Humphrey Polepole naye alishauri muafaka ufanyike kabla ya kwenda kwenye uchaguzi.

Wengi walitoa maoni yao, akiwemo mwanasiasa mkongwe Joseph Warioba. Hata hivyo, Oktoba 29 uchaguzi ulifanyika bila kitendawili hicho kuteguliwa. Katika kampeni za mgombea wa CCM wa nafasi ya urais, Samia Suluhu, ambaye baadaye alitangazwa mshindi, aliahidi kuwa baada ya uchaguzi kungefanyika maridhiano kwa lengo la kuimarisha umoja wa kitaifa.

Baadhi ya wadau waliona maridhiano yalikuwa muhimu katika kipindi hicho ili kuepusha athari kwa mwelekeo wa demokrasia. Wapo waliodai kuwa maridhiano ya mapema hupunguza uwezekano wa migogoro na kuongeza ustawi wa demokrasia. Wengine walieleza kuwa maridhiano kabla ya uchaguzi yangeweza kupelekea uchaguzi unaozingatia misingi ya kweli ya demokrasia ya vyama vingi.

Chadema, chama kikuu cha upinzani, kilieleza utayari wake kabla ya uchaguzi kukaa na kujadiliana muafaka wa kubadili baadhi ya mambo, hususan sheria za uchaguzi.

Nini kinaendelea?

Hadi leo, ni takriban siku 100 tangu Rais Samia alipoapishwa kwa muhula wake wa pili, lakini kitendawili hiki kinaendelea kulikuna Taifa kila kona.

Serikali imeeleza msimamo wake kuwa ipo tayari kufanya maridhiano. Wadau wengine, kama Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Mzee Joseph Butiku, walijitokeza kutaka kupalilia njia ya kuelekea maridhiano, lakini bado kumekuwepo na ukimya.

Chama kikuu cha upinzani CHADEMA hadi sasa hakijaonesha dalili ya kuingia katika maridhiano hayo, huku kikiendelea kusimamia msimamo wake wa kutoutambua uchaguzi uliofanyika.

Soma Kesi ya Lissu na hatima ya maridhiano

Serikali, kupitia msemaji wake Gerson Msigwa, imeeleza wazi kuwa suala la maridhiano ni la hiari, na hakuna mtu au kundi linaloweza kulazimishwa kushiriki katika mchakato huo.

Kauli ya Msigwa, soma Msigwa: Maridhiano ni jambo la hiari sio kulazimishwa

Wakati Msigwa akisema hivyo, baadhi ya jumuiya za kimataifa zimekuwa zikitoa wito kwa Serikali ya Tanzania kutumia njia ya maridhiano kukabili changamoto mbalimbali, ikiwemo za kidemokrasia, zilizojitokeza katika kipindi cha hivi karibuni.

Pia soma Baada ya mauaji ya Oktoba 29, CCM inahitaji maridhiano kuliko CHADEMA

Mlolongo wa kitendawili hiki kinacholikuna Taifa unaibua tafakari juu ya tafsiri halisi ya maridhiano. Baadhi ya wananchi wamekuwa wakiona mchakato huo kama mtego wa kisiasa ambao kila upande anahofia kuingia kwa haraka.

Hali hiyo inaonekana katika kushindwa kufanyika kwa uamuzi wa maridhiano kabla ya uchaguzi, kama walivyoshauri baadhi ya wadau wa siasa za Tanzania. Aidha, taswira hiyo inaendelea kujitokeza hata baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, wapo wanaoamini kuwa maridhiano yanapaswa kufanyika kwa namna yoyote ile kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa. Kundi hilo linataka kuona dhamira ya dhati katika mchakato huo.
 
gentleman,
maridhiano chini ya serikali sikivu ya CCM, yana dhamira njema ndio maana yapo kwenye ratiba za serikali.
Maridhiano kama hayo yalishawahi kufanyika Zanzibara na Bara pia, yakileta matokeo chanya kwa pande zote zinazohusika.
Hata hivyo,
ni vizuri kufahamu kwamba maridhiano ni suala la hiyari, na sio lazima kwa sote kushiriki jambo hili la kitaifa.
 
Kwanini walikataa maridhiano kabla ya uchuguzi?
Wameua raia wengi wasio na hatia 29oct leo mkae meza moja na wauaji mridhiane nini?
Mazafanta!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…