Je, serikali ni matapeli?

Je, serikali ni matapeli?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wanahabari wamelalama kuwa wanadai serikali jumla ya bilioni 18 za kitanzania. Haya malimbikizo ya madeni kwa miaka kadhaa ambayo yametajwa kuathiri uchumi wa vyombo vya habari.

Suala la madeni sio tu kwa sekta ya habari, nimesikia wadau kadhaa wakilalamika kutolipwa na serikali kiasi cha madeni hayo kukua au wakati mwingine kuathiri uchumi wa waliotoa huduma husika kwa serikali.

Kama serikali iko serious kwenye kukuza uchumi wa watu na haitaki kulipa madeni yake, je inakuwa serikali ya kitapeli kama wahuni wanaokopa benki na baadae hawalipi? Je, kuwe na utaratibu wa kuishtaki serikali na kuvishikilia baadhi ya vitu vya serikali ikiwa imeleta shida ya kutolipa kwa wakati?
 
kwani ulikua hujui ...? afu serikali ni kwani ...? eeenh serikali si ni mimi na wewe yaani huyu na yule ...? wewe sio tapeli...? mimi sio tapeli...? kwa upande wangu mm ni tapeli hata na wengine nao ni matapeli
 
Back
Top Bottom