Je, Serikali ya Kenya ilifadhili baadhi ya machafuko katika maandamano ya leo?

Je, Serikali ya Kenya ilifadhili baadhi ya machafuko katika maandamano ya leo?

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Jumatatu tarehe 27 Machi 2023 imekuwa ni siku ya taharuki katika maeneo mengi nchini Kenya huku vuguvugu la maandamano linaloongozwa na Raila Odinga likizidi kurindima.

Leo imekuwa ni siku ya pili ya maandamano hayo ya Jumatatu huku mengine yakitarajiwa siku ya Alhamis.

Hatahivyo maandamano ya leo wameibua maswali mengi miongoni mwa Kenya ikilinganishwa na yale ya wiki Jana. Haya ni baadhi ya maswali yaliyomo kwenye fikra za watu wengi:

(a) Imekuwaje leo shamba la Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kushambuliwa na mamia ya watu wasiojulikana, wakakata miti na kuondoka na mamia ya mbuzi?

(b) Imekuwaje leo kampuni ya gesi ya Spectre Limited inayomilikiwa na Raila Odinga kuvamiwa na watu wasiojulikana?

(c) Ni kwa nini maafisa wa polisi wamechelewa kufika eneo la Kibra ambapo makundi mawili yamezozana usiku wa Jumatatu; ikizingatiwa kuwa maafisa hao hao walikuwepo mchana kutwa kudhibiti waandamanaji katika eneo hilo la Kibra?

Baada ya kuuliza maswali hayo, itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 19 Machi 2023, Kiongozi wa wengi Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa eneo-bunge la Kikuyu Mheshimiwa Kimani Ichung'wa alimuonya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwamba huenda pia mali yake ikavamiwa, akidai kuwa Kenyatta ndiye mfadhili mkubwa wa maandamano ya Odinga kwa kusudi kuinyima Serikali ya William Ruto utulivu [Msikilize Kimani Ichung'wa hapo chini].

Jambo lililowashangaza Wakenya wengi Leo ni uvamizi wa shamba Hilo la Uhuru Kenyatta ambalo pia ni makao makuu ya kampuni yake ya Maziwa iitwayo Brookside. JE, NI KWELI KUWA BWANA KIMANI UCHUNGUZI ALIMAANISHA MANENO YAKE? Ikumbukwe Ichung'wa ni mwandani wa karibu mno wa Rais William Ruto.

Jambo la pili, kwa mara ya kwanza Leo kampuni ya Raila Odinga Spectre Limited iliyoko eneo la Industrial area vilevile ilivamiwa asubuhi ya Jumatatu japokuwa hakuna chochote kilichoibwa ila tu uharibifu mkubwa wa vioo na kamera za CCTV. Yawezekana wafuasi wa Odinga walikwenda kuharibu mali ya Kiongozi wao? Hilo pia ni swali la msingi. Ikumbukwe Jumapili tarehe 26 Machi 2023, Mhe' Raila Odinga alidai kuwa palikuwepo na njama ya kuvuruga maandamano, ambapo alimshtumu Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kuwa aliwalipa vijana kutekeleza agizo la kuharibu mali na kuvuruga maandamano kwa lengo la kumchafua Odinga kama mtu wa purukushani.

Mwisho kabisa, mzozo wa makundi mawili yaishio eneo la Kibra umeibua maswali si haba. Duru za kuaminika zinasema kuwa kikundi kimoja kiligoma kushiriki maandamano yaliyoshuhudiwa mchana kutwa kikidai hayana manufaa jambo lililopelekea mzozo baina yao na waliokuwa wakiandamana. Mzozo huo ulipelekea vita vikubwa Kibra huku msikiti mmoja ukiteketezwa moto(japokuwa moto ulidhibitiwa) na baada ya hapo kanisa moja nalo likachomwa moto.

Kinachoshangaza ni kuwa maafisa wa polisi walisita kwenda kutuliza Hali hio licha ya kuwa walikuwa wakipiga doria mchana kutwa. Ni kwa nini maafisa wa polisi walidinda kwenda kutuliza hali kwa haraka? Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja mwenyewe katika ukurasa wake wa twitter alikiri kuwa Jeshi lake la Zimamoto liliogopa kwenda kuzima moto likiomba kusindikizwa na Polisi.

Matukio haya matatu yamewaacha wengi na SWALI Moja la Msingi....JE, INAWEZEKANA KUWA SERIKALI ILIFADHILI BAADHI YA WATU KUFANYA FUJO KWA LENGO LA KUCHAFUA UPINZANI ZAIDI????
 
Back
Top Bottom