Je Serukamba ni Mkweli kuhusu Dowans?

Je Serukamba ni Mkweli kuhusu Dowans?

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Posts
4,635
Reaction score
2,271
Mh.Serukamba katika gazeti la Mtanzania la 07/03/2009 anasema Sitta na mwakyembe wanaihujumu CCM.Haya maneno ni ya kweli kwa mwakilishi wa wananchi na anayewatakia maendeleo wananchi wake.

Je Serukamba anapata wapi jeuri ya kumshutumu Spika kwenye vyombo vya habari.Si bure kuna kitu kinaendelea katika nchi hii ambayo imefichwa.

Wana JF mtupe data kuhusu suala hili.

Mimi ninafikiri Sitta na Mwakyembe wanaihujumu ufisadi na mtandao wa wahujumu uchumi wa TZ.
 
Gazeti la Mtanzania wana kitu na Dowans, kwa nini wasimhoji na Mwakyembe pia kama alivyonaya ITV walipomhoji Zitto na wakamhoji na Mwakyembe?

Suluhisho ni kundi mojawapo la Serukamba au la Mwakyembe kuwaachia wenzao chama na wao waanzishe cha kwao.
 
Huyu Serukamba ni mropokaji tu,ni mtu ambaye anajua kujipendekeza sana,na anapenda watu wenye uwezo,ndio maana ana babaikia mafisadi....,lakina hana point katika hili,wa kupuunzwa tu....
 
Gazeti la Mtanzania wana kitu na Dowans, kwa nini wasimhoji na Mwakyembe pia kama alivyonaya ITV walipomhoji Zitto na wakamhoji na Mwakyembe?

Suluhisho ni kundi mojawapo la Serukamba au la Mwakyembe kuwaachia wenzao chama na wao waanzishe cha kwao.

Tatizo ni kwamba hakuna kundi linalokubali kuachia chama kutokana na gharama ya kujijenga upya,labda viongozi wa juu wa CCM wamue kuwa wazi ili wanaojiita wanaCCM mtandao,mpasuko na maslahi watengwe na kubakiza CCM ya 1977.
 
Tatizo ni kwamba hakuna kundi linalokubali kuachia chama kutokana na gharama ya kujijenga upya,labda viongozi wa juu wa CCM wamue kuwa wazi ili wanaojiita wanaCCM mtandao,mpasuko na maslahi watengwe na
 
huyu jamaa ni part ya mafisadi thus why he is defending the group. Kwa mtanzania wa sasa mwenye akili timamu huwezi kusauport ujinga wa namna hii. Serikali na tanesco walitakiwa kuwa na long plan kuhusu tatizo la umeme ukizingatia kuwa hali ya maendeleo ya nchi. Hivi tuseme kama downs ingekuwa imeshaondolewa hapa Tanzania baada ya malipo yao kuzuiwa wangeshauri nini kwa Serikali/Jamii ya watanzania?
 
Mheshimwa huyu hana hoja, kinacotakiwa kufanya ni kuwa 2010 asiingie bungeni. Uwezo wake kiakili umeonesha kuwa hana uwezo wa kuwawakilisha wananchi, bali lengo lake kubwa ni kuwalinda wezi. Yeye nchi yake, chama chake, wapiga kura wake na jimbo lake havina maana kwake kuliko kuwalinda mafisadi. Yeye mafisadi ndio miungu yake.
 
Huyu serukamba ni mtu hovyo kabisa,anajikomba sana kwa wenye uwezo wakati yeye katoka familia masikini.Ukiona anasifu kitu ujue anatafuta sifa hapo.Anadhani kuomba uongozi akiwa IFM ndo uwezo wa kutafakari hata mawazo ya zaidi ya watu 20,000 wa jimbo lake.Anachojua yeye ni ngono tu.Mkifuatilia historia yake kabla ya Kuwa mbunge alikuwa anajigonga sana kwa wakubwa hasa watoto wao,fisadi lowasa kupitia kwa mtoto wake ndo kulikompa ubunge.Mwaka 2010 hana lwake huyooooooooooooooo!!!!!
 
Wana JF tufahamu kuwa uchaguzi mkuu unakaribia. Kama kawaida ya wagombea wetu, rushwa mbele ili wapate ubunge then maslahi ya wapiga kura wao nyuma. Serukamba, ninavyomfahamu, aliupata ubunge katika jimbo la kigoma mjini baada ya wananchi kumchoka aliyekuwa Mhe. Kaburu, wakaona bora wampe yeyote yule hata kama ni ganda la nazi. Sasa ganda la nazi ndio hilo tunaliona, badala ya kuupiga vita ufisadi na mafisadi, Serukamba, anauunga mkono, kuunga kwake mkono sio bure, ni maandalizi ya kutafuta fedha za kampeni. Kwani hapa TZ fedha hizo atazipata wapi kama si kwa hao mafisadi? Naona ndio sababu ya huyo jamaa kuwapiga vita akina Sitta na Dr. Mwakyembe. Niungane na Sevrine hapo juu, ni kwamba, Serukamba kamwe hatauona ubunge wa kuchaguliwa katika jimbo analilishikilia kwa sasa.
 
mheshimwa huyu hana hoja, kinacotakiwa kufanya ni kuwa 2010 asiingie bungeni. Uwezo wake kiakili umeonesha kuwa hana uwezo wa kuwawakilisha wananchi, bali lengo lake kubwa ni kuwalinda wezi. Yeye nchi yake, chama chake, wapiga kura wake na jimbo lake havina maana kwake kuliko kuwalinda mafisadi. Yeye mafisadi ndio miungu yake.

na zitto je?
 
na zitto je?

Mh.Zitto Kabwe kama hataseme ni mdudu gani alimwingi hadi kushabikia Dowans na yeye ni bora awe kwenye orodha ya kutemwa 2010.Huyu bwana anaidhalilisha CHADEMA kwa sasa ni bora wamshauri ajiunge na mtandao wa ufisadi.Tangu aingizwe na Rais kwenye Kamati ya madini amebadilika na Chadema wasipoangalia ni ukoma utakaowatafuna muda mfupi ujao.
 
huyu Serukamba anatabia ya kujipendekeza kwa akina Rostam na washirika wake.Hii tabia alianza mapema toka alipokuwa Makao makuu Benki ya Posta, mpaka akaamua kugombea ubunge kule Kighoma.hivyo anajaribu kulipa fadhila za hao wafisadi waliomsadia kupata ubunge.
 
Back
Top Bottom