Je, sheria hapa inasemaje?

Je, sheria hapa inasemaje?

GIPAMA

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2016
Posts
1,103
Reaction score
541
WanaJF na mawakili wasomi wote mlioko humu, amani na iwe kwenu....

Naomba kufahamishwa na kufafanuliwa sheria inasemaje juu ya hili?

Mfano, mtu aliyeathirika na anajijua kuwa ni muathirika na anatumia ujanja janja wake na ushawishi wa kila namna hata wa hali na mali na kumshawiahi mtu ambae uelewa wake uko chini na kumuambukiza ugonjwa UKIMWI...

Iko hivi, mimi nina kakaangu, ni mlemavu wa kusikia na kuongea (Bubu) anamiaka 46, kashawishiwa na limama fulani ambalo ni liathirika likiwa na uwezo wa kuongea, yaan lina akili timamu na halina ulemavu wowote, likamshawishi huyu kaka angu na kufanya nae ngono.

Baadae watu wakaribu na hilo jimama wakamwambia kaka kuwa hilo limama ni liathirika, mahusiano ya kingono yalianza 18.04.2017 alipockia hizo tetesi kaka akaenda kupima 19.06.2017 akakutwa ni mzima, ila leo karudia tena kupima akakutwa ni H.I.V postive.
Sasa mimi nikiwa mtegemewa wa huyu ndugu yangu, naweza kuchukua hatua gani za kisheria, je sheria inasemaje juu ya hilo?

Je nikichukua hatua hzo nitapata msaada upi ama nitakuwa nimemsaidiaje huyu ndugu yangu ambaye ni tegemezi na kashaambukizwa!?

USHAURI TAFADHALI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni Kosa kisheria, kifungu cha 179 , cha sura ya 16 ya sheria za jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, inasema(S.179 of the Penal Code, cap 16. R.E. 2002, Provides, Any person who unlawfully or negligently does any act which is, and which he knows or has reason to believe to be likely to spread the infection of any disease dangerous to life, is guilty of a misdemeanour) ila ukisoma kipengele cha 6.6 cha sera ya ukimwi mwaka 2001, serikali iilikua na mkakati wa kurekebisha sheria ya kanuni za adhabu, http://www.tanzania.go.tz/pdf/serayaukimwi.pdf ) ( ili kutia watu hatiani kwa kuambukiza ukimwi, makusudi, sina taarifa sahihi kama hili limeshafanyika kama limeshafanyika..... Nimeicaught humu jukwaani

The general principle of interpreting a penal status is by LITERAL approach. Ukisoma kwa tafsiri ya kisheria (sio ya lugha/semantics) hicho kifungu cha 179 hakitumiki hapa/katika kesi hii.

Swali la msingi zaidi ni kwmb.....Je kufanya mapenzi (watu wa jinsia tofauti/ME/KE) ni kitendo cha kosa?? "Is copulation unlawful act??" Kwa mjibu wa kifungu hiki kitendo hicho kiwe kosa kisheria "unlawful abi initio" mfano;

1. Kukohoa mbele ya uso wa mtu ukijua kuwa una TB ili nae apate TB
2. Dr. Kukuongezea damu isiyo salama, huku akijua damu hyo sio salama na ukapata ugonjwa.

NB; ili kuwa na hatia chini ya s. 179 ni lazma kitendo kilichofanyika/kilichofanywa kiwe ni UNLAWFUL act. (Kiwe kinyume cha sheria).
 
Back
Top Bottom