Je, shetani/ibilisi anatoka koo zipi miongoni mwa koo za majini? Wazazi waliomzaa ni akina nani?

Mkuu acha kupotosha watu, ni sawa binadamu wa leo akaye na malaika au jini halafu binadamu aseme kwamba kaumbwa kwa udongo na jini kaumbwa kwa moto kwa hiyo haimaanishi kwa kusema hivyo imfanye huyo binadamu awe ndiye binadamu wa kwanza kuumbwa.

Na si kweli kwamba malaika walisaidiwa na majini ili kupambana na majini wengine , kaa ukijua malaika wawili tu wanaweza wakasambaratisha majini yote yaliyopo duniani sasa unaposema malaika walisaidiwa na majini inamaanisha kwamba malaika walikuwa wamezidiwa nguvu na majini kitu ambacho ni kufuru kubwa sana.
 
Inavyoonekana umekariri vibaya mkuu tena vibaya mno!
 
Sitaki kuji envolve na mada kama hizi ila subiri watakuja masheikh kuthibitisha hili ila jua tu kuwa si malaika waliomuomba mungu wamlee ibilisi karudie kusoma upya
kama sio malaika waliomuomba waishi naye Ibilisi ,je ni nani aliyemuombea Ibilisi aishi na malaika?
 
IBILISI/SHETANI NDIO KIZAZI KILICHO KATIKA MAFICHO YA UPEO WA MACHO NAE IBILISI NA MAJINI WALIUMBWA KABLA YA ADAM NA ALITOKANA NA KUUMBWA KWA NDIMI ZA MOTO "Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto."(QURAN 15:27).....KIHISTORIA IBILISI ALIKUWA MCHAMUNGU KIASI CHA KUITWA BABA WA SIJDA KUTOKANA NA KULE KUMSUJUDIA MWENYEZI MUNGU KIASI CHA KILA SEHEMU YA ARDHI ILIENEA SIJDA ZAKE....ALIASI KWA KULE KUTAKABALI KWAKE NAKUJIONA BORA ZAIDI YA ADAMU NA KUKATAA KUMPA SIJDA YA HESHIMA ADAM PINDI ALIPOUMBWA ``11. Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.12. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.13. Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe u miongoni mwa walio duni.14. Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa.15. Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula.16. Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.17. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.18. Akasema:Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote."(QURAN 7:11-18)
.....IBILISI ALIKUWA KTK KIZAZI CHA MAJINI "Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu."(QURAN 18:50) ILA BAADA YA KUASI KWAKE ALITEREMSHWA DUNIANI...IBILISI ANA KABILA ZAKE IKIWA NI PAMOJA NA MAJINI/PEPO/ NA MASHETANI(KUNA NA MASHETANI WATU) NALO NDILO LINAUNDA JESHI LAKE ``Na majeshi ya Ibilisi yote.``(QURAN 26:95)
HAKUNA MAFUNGAMANO/USHIRIKA BAINA YA MAJINI NA BINADAMU HATA KAMA UNA KUNUFAISHANA"Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua."(QURAN 6:128)..ILA MWENYEZI MUNGU AKITAKA YEYE KWA IDHINI YAKE ANAWAAMRISHA MAJINI YAMTUMIKIE MJA WAKE APENDAVYO KAMA ALIVYOYAAMRISHA MAJINI YAMTUMIKIE MFALME NABII SULEIMAN "Na Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyayushia chemchem ya shaba. Na katika majini walikuwako walio kuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anaye jitenga na amri yetu katika wao, tunamwonjesha adhabu ya Moto unao waka."(QURAN 34:12)
SOMA ZAIDI KWENYE POST HII
JINI,SHAYTWAAN NA UCHAWI
 
Mkuu sababu kubwa sichangii humu huwa sipendi hoja za kijinga, kama mimi naleta ushahidi wa aya na wewe unajibu maneno makavu kwa heri, wengine wataendelea kuchangia.
 
Mkuu, umezunguka sana lakini hujajibu maswali yangu haya.

1)Wazazi wa ibilisi ni akina nani?

2)Anatokea ukoo upi au aina ipi ya majini?

3)Historia yake ya kuzaliwa kwake ilikuwa kuwaje ,kulikuwa kuna ishara yoyote ile isiyo ya kawaida?

4)Je majini na wao waliwahi kuishi peponi kabla ya kushushwa duniani?

5)Historia yake mara baada ya kulaaniwa ikoje? Uzao wake ulikuwaje? Nani alikuwa mtoto wake wa kwanza?
 
Maswali ya ziada

6)Kama ikiwa Ibilisi alipewa ruhusa ya kuishi mpaka mwisho wa dunia ,je hiyo ruhusa ilikuwa inawahusu mpaka vizazi vyake vilivyotokana na yeye??

7)Nani alikuwa mke wake waliyeanzisha naye familia?
 
Mkuu sababu kubwa sichangii humu huwa sipendi hoja za kijinga, kama mimi naleta ushahidi wa aya na wewe unajibu maneno makavu kwa heri, wengine wataendelea kuchangia.
Kwani nani aliye kutag humu?

Si umejileta mwenyewe ?

Kila nikikuuliza swali unajiuma uma tu .
 
1)Wazazi wa ibilisi ni akina nani?
MUNGU ALIMUUMBA KUTOKANA NA NDIMI ZA MOTO NA UPEPO(ALITOKA KATIKA MAJINI)
2)Anatokea ukoo upi au aina ipi ya majini?
NI KATIKA MAJINI WALIOASI?WABAYAI (KUNA NAJINI WEMA/WACHAMUNGU NA WABAYA) YEYE NDIO MKUBWA WAO KATIKA HAO WAOVU
3)Historia yake ya kuzaliwa kwake ilikuwa kuwaje ,kulikuwa kuna ishara yoyote ile isiyo ya kawaida?
KAMA VILE ADAM ALIVYOUMBWA KWA UDONGO YEYE/MAJINI WALIUMBWA KWA NDIMI ZA MOTO NA UPEPO..YEYE KUJA KUWA SHETANI(KULAANIWA) NI BAADA YA KUMUASI ALLAH KWA KUKATAA KUMPA SIJDA YA HESHIMA ADAM
4)Je majini na wao waliwahi kuishi peponi kabla ya kushushwa duniani?
PEPONI KAMA PEPONI BADO KUINGIA MPAKA IPITE SIKU YA HESABU ILI KUCHAMBUA WEMA WA PEPONI NA WABAYA WA MOTONI (KUNA WALIOKWISHA KUINGIZWA AMBAO NI WATOTO WALIOKUFA WANGALI WACHANGA)...KAMA PEPONI UMEMAANISHA BUSTANI YA EDENI BASI IBILISHI ALIKUWEPO NA NDIO ALIMSHAWISHI HAWA KULA TUNDA.......KUNA MAANDIKO KATIKA UISLAMU YANASEMA ATAKAYE INGIA PEPENI ATADUMU HUMO MILELE SO NIWAZI KWAMBA SHETANI/IBILISI HAJAWAI KUINGIA PEPONI...
NA ALLAH ANAJUA ZAIDI
 
Kwa mujibu wa jibu lako la kwanza unamaanisha kwamba Ibilisi hakuzaliwa bali aliumbwa kama Adamu , kwa hiyo bila shaka Ibilisi ndiye Jini wa kwanza kabisa kuumbwa siyo?

Je kama ikiwa yeye ndiye jini wa kwanza kuumbwa historia ya hao wengine waliofuatia ilikuwaje?

Swali la pili umedai Ibilisi ametokea ukoo wa majini wabaya na yeye ndiye mkubwa wao ,sasa inawezekana vipi yeye ndiye awe mkubwa wa majini wote wabaya halafu malaika walipoenda kuwasambaratisha majini wabaya wawasambaratishe wote halafu yeye mlengwa aachwe?
 
Maswali ya ziada

6)Kama ikiwa Ibilisi alipewa ruhusa ya kuishi mpaka mwisho wa dunia ,je hiyo ruhusa ilikuwa inawahusu mpaka vizazi vyake vilivyotokana na yeye??

7)Nani alikuwa mke wake waliyeanzisha naye familia?
6)Kama ikiwa Ibilisi alipewa ruhusa ya kuishi mpaka mwisho wa dunia ,je hiyo ruhusa ilikuwa inawahusu mpaka vizazi vyake vilivyotokana na yeye??
NI YEYE NDIO ALIYEPEWA MUHULA WA KUISHI HADI MWISHO WA DUNIA NA KUISHILIA MOTONI YEYE NA JESHI LAKE(WAASI WENZAKE)
7)Nani alikuwa mke wake waliyeanzisha naye familia?
HANA MKE HANA FAMILIA ILA JAMII YAKE NI KTK MAJINI NAO MAJINI YANAZALIANA NA KUFA..MAJINI AKIWEMO YEYE IBILISI WALIUMBWA NA MUNGU KUTOKANA NA NDIMI ZA MOTO NA UPEPO
 
Swali la tatu nimekuuliza kuhusu kuzaliwa/kuumbwa kwake kulikuwa kuwaje , kulikiwa na ishara yoyote lakini cha ajabu unakuja kutoa sababu ya kulaniwa? Embu yasome maswali yangu kwa umakini kisha toa jibu kulingana na swali nililouliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…