Je, shida yetu na JK sio ‘mental health issue’ kweli

Mbowe alikua anatumikia maslahi yake hakua mpinzani ndo maana Magu alivyogundua kwamba mambo ambayo walikua wanalilia wapinzani ndo nafanya mbona wananigeuka mwanzoni mwa urais Magu aliwapenda wapinzani aliwahi kwenda kwenye msiba wa Dada ake Lissu akaja kustuka upinzani wa mchongo Ndo JK aliweza kurelax Jk na mbowe wanafahamina vizuri mno Mbowe alikua na Club kubwa bongo Bilcanasi ageshidwa vipi kufahamina na Mbowe ambae alifanya BOT watu wa madeal sasa hawa Walugaluga kutoka vijijini ndo wameleta shida huyu Mkemia na huyu Kutoka Singinda watu kutoka mikoani ndo wamembadilisha Jk
 
Hebu nami nitie neno kidogo kwa mtazamo wangu,, huyu mkwere huyu tokea huko 1995-2015 kwenye harakati zake za kisiasa alionekana mtu poa baada ya hapo mnaona kama kabadilika lakini hajabadilila ni yule yule wa siku zote,, kipindi chake rushwa na ufisadi ulimea mizizi na kuota mapembe, akajikusanyia alivyoweza,, akaachia wapinzani waseme chochote wawezavyo alifanya makusudi sababu alijua hakuna wa kumgusa wala kumchezea sharubu,, sakata la RICHMOND akamtoa sadaka rafiki yake kwa siku nyingi Lowasa kama mbinu ya kummpunguza nguvu kisiasa, sababu alikuwa anakubalika kumzidi, 2015 mnakumbuka kilichotokea alitaka kuweka mtu ambae atamuongoza yeye kwa kufanya kila alichotaka ili kile alichochota kwenye awamu yake kizalishe maradufu,,, mpango ukabuma maana JPM hakumpa hiyo nafasi happ ndipo sasa akaanza kupambana kuhakikisha anamtoa Jpm maana alimimnywa sawasawa kiasi kwamba kile alichochota miaka yake 10 hakikuwa na maana kilipukutika chote,

Kafanikiwa kumtoa JPM,, kaingia huyo mzanzibari anamcontrol anavyotaka kufidia kile alichoiba na kukizalisha kile alichopoteza kwa miaka 5 ya hayati JPM,

Anachofanya saiv ana hofu hataki huyu hawara yake atoke kwenye hicho kiti kwa kuogopa atakaekuja huenda akawa aggressive zaidi ya JPM ataumbuka na hana muda mrefu tena huko mbele kwa umri wake kuendelea kujipanga nk, ndo maana yupo tayari kumwaga damu ili tu lake liende,, kwahiyo hana mental problem yoyote, hivyo ndivyo alivyo hiyo ndio asili yake,, mlafi, mbinafsi na mwenye roho mbaya ni hasara kwa taifa hili.
 
JPM alimbadilisha JK kwa namna hii(kwa njema wa mbaya),
Kwanza JPM aliachana na utamaduni wa marais wa CCM kutilia maanani au kuheshimu viongozi wazee vigogo wa CCM waliopita akiwemo JK labda wengi hawakuwa upande wake au na msaada wowote wa yeye kuupata urais kwa hiyo alifikiri hakuwa na deni kwao, hakuwahi kuwa kiongozi wa chama kwa hiyo hakuwa ni mtu anayefahamu na kujali sana tamaduni za chama na pia kwa sababu mtindo wao wa uongozi ulikuwa tofauti kabisa Kikwete akiwa muumini wa mijadala na kufikia miafaka na JPM akiwa muumini wa kutawala kwa amri za kiongozi.

JPM kutokuwa na sikio kwa JK ina maana ilibidi JK aufyate aendane na mdundo wa chuma alinde maslahi yake na ya familia yake(kumbuka jiwe alikuwa haogopi au hana aibu kumshughulikia yoyote), hakuweza kuwasaidia watu wake wa karibu kama Manji na wengine waliokuwa wakimlilia awasaidie, alipojaribu kuzungumzia demokrasia mara moja tulisikia upande mwingine ukijibu wastaafu waache kuwashwashwa na vijana wa jiwe wakamfyatua hasa, kwa mtu aliyekikalia hicho kitu akipewa heshima zote hilo haliwezi kuacha kuuma kama shubiri na kujichunga akiwa anajua vizuri nguvu ya hicho kiti kwa hiyo lilibidi atulie zaidi sana aendane na muziki.

Jiwe ameondoka kitini akiwa ameibadili kabisa CCM kama chama kisichojali tena demokrasia bali kushika dola tu kwa namna yoyote huku kikiwa na hardliners wa kutosha lakini kwa bahati nzuri kwake JK aliyebaki kitini kama mrithi ni mtu wake kabisa anayemmudu na anayemsikiliza.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Mpaka Mnyika alimbatiza jina la dhaifu asiweza fanya maamuzi.

Jamaa alikuwa anakosolewa kila kona wazi wazi ndio msingi wa interview ya mtoto.

I wish ningeipata ile (najua nitaipata baadae) kama kiambatanisho usikie mwenyewe from the horse’s mouth. Ridhiwani akilalama ata yeye kwa baba yake matusi yamezidi na majibu aliyopewa hujui nguvu zangu kikatiba nikitaka kuzuia.

Sasa hivi tuna kichaa kapewa rungu, ajabu JK ndio msindikizaji.

Kaazi kweli kweli
 
Sijasema bora demokrasia na ufisadi, mimi naamini inawezekana kuwa na demokrasia ukipambana na ufisadi.
Hata hivyo upinzani ambayo jiwe alikuwa anapambana nao kuumaliza haukuwa umehusika na ufisadi uliokuwa unafanya na CCM wala haukuwa unamzuia kwa namna yoyote kufanya miradi yake aliyokuwa anaona ni ya muhumu zaidi kuliko katiba mpya na demokrasia.

Jambo lingine ambalo limejadiliwa sana ni kwamba ni vigumu kufanya tathmini ya ufisadi wa wakati wa jiwe kwa sababu aliondoa kabisa uhuru wa media, ofisi ya CAG na bunge.
 
Sababu kubwa iliyowafanya watu wakaandamana na wakapigwa risasi kwa maelfu sasa hivi ni kwa sababu ya demokrasia(kukosekana kwa dalili zozote za uchaguzi wa maana mtindo ulionza na JPM 2019), ingekuwa watu wanaandamana kupinga ufisadi wangeandamana tarehe nyingine tofauti na October 29.
 
Kama inakuja hivi hii kuhusu Mzee wetu Jk
 
Mawazo Yako, haki Yako kuongea.
 
Lissu aliyepigwa risasi 16 alifaidika vipi na utawala wa JK?
Kwa nini Jiwe hakumkamata Mbowe kwa kesi yoyote ya upigaji deal enzi za JK? Kuna tatizo gani Mbowe kufahamiana na JK wakati huo??
 
Malalamiko ya Ridhiwani kuhusu baba yake kutukanwa ni exaggerations kama sio uongo mtupu. Kiongozi katika nchi iliyo Jamuhuri inayojinasibu kuwa ni ya kidemokrasia kuitwa dhaifu, Vasco dagama au fisadi wala sio matusi.
Hata hivyo Waswahili Kuna lugha za kuremba wamezizoea kwa hiyo labda wakati zinapotumika lugha kali kidogo zisizo za kuremba ndio wanaita matusi.
 
moja ya mambo yanayo sumbua ni upweke alio nao ktk nafasi yake.
 
SimzungumziimJakaya wa 2015 na kwenda mbele.

Namzungumzia yule aliekuwa raisi 2005 mpaka 2015, mwenye hekima, uvumilivu na maslahi mapana ya CCM.

Yule sio huyu Waleo kabisa mwenye tamaa, nini kimempata.
Swali sahihi, ni nini kimewapata mnao uliza swali.
 

lkn hayo ulioyaorodhesha yanafiti kwenye mental illness, kichaa siyo yule anayeokota makopo tu barabarani, psycopathy ni ukichaa, kwa maana binadamu wa kawaida hayuko hivyo, ndiyo maana unaona kuna maraisi wengi duniani kote wanakuja wanamaliza muda wao wanapita wanatulia na kuwapisha wengine, lkn kwa nini wengine wanaharibu hiyo trend na kufikiri kwamba wao ndiyo wana haki ya uraisi klk wengine waliopita? huo ni ugonjwa wa akili.

ubinafsi na hiyo mnayoiita roho mbaya ni ugonjwa wa kili kwa maana binadamu wa kawaida hayuko hivyo, hawa watu siyo wa kawaida angalia kwa mfano sadamu huseni au hata gadafi walikuwa na uwezo wa kuondoka libya na irak na walipewa huo muda na hata walipangiwa exit, Afrika Kusini ilimpa hifadhi gadafi mpaka hata ilituma airforce kwenda kumchukua libya lkn aligoma na bado walibisha hata pale ambapo kila mtu dunia nzima alijua hawatoboi matokeo yake wamekufa kifo cha mateso sana, kama gadafi mpka nasikia waarabu walimbaka na kumlawiti kabla ya kumuua ushenzi wa warabu, sadamu alinyongwa tena kwa kamba live on tv lkn kuna njia nyingine mfano assad wa siria alipoona kwamba hawezi toboa alikubali akapanda ndege akaondoka na familia yake, leo hii anaishi urusi.

hivyo kipi kinachowatofautisha sadamu, gadafi vs assad ? ni ukichaa, gadafi na sadamu walikuwa ni psychos, wana different reality tofauti na binadamu wengine ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…