Je, Simba kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu 22-2023?

Je, Simba kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu 22-2023?

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
8,542
Reaction score
18,340
Sare anazopata Simba zinamuweka katika hali ngumu ya kurejesha ubingwa pale Msimbazi. Mpaka sasa inabidi Yanga ipoteze angalau michezo miwili ndipo Simba ipate ahueni.

Lakini pamoja na yote, swali la Msingi ni kwamba Simba imefikaje katika hali hii? Hapa ndipo kwenye tatizo la msingi. Simba kuna mahali walikwama ndio sababu leo wako hapa.

Kwanza walifeli katika usajili. Kati ya wachezaji saba waliosajiliwa Simba ni Augustine Okrah na Moses Phiri tu wameweza kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza.

Bahati mbaya zaidi ni kwamba hao wengine licha ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza hawana hata msaada wakitokea benchi. Inashangaza sana.

Simba Walifeli mno Hasa eneo la kati kati ya uwanja 6,8 na pia eneo la ushambuliaji. Matokeo yake akitoka John Bocco ataingia Kibu Denis. Mchezaji fulani wa mchongo.

Mshambuliaji ambaye anasifika zaidi katika kukaba. Wakati kina Ayoub Lyanga, Sixtus Sabilo wakisifika kufunga na kutoa pasi za mwisho, Kibu anasifika kukaba. Inachekesha sana.

Vipi asipokuwepo Sadio Kanoute. Anayesua sua. Nafasi yake atacheza Jonas Mkude ama Victor Akpan. Huyu Akpan ni mchezaji mzuri wa kawaida. Simba walihadaika na zile pasi zake pale Coastal Union, lakini ukweli mchungu ni kuwa siyo mchezaji wa daraja lao.

Mkude amechoka. Nadhani pengine sababu ya kucheza mfululizo kwa miaka mingi ama umri umeanza kumtupa mkono. Yupo unga kwelikweli. Anajitengea kieneo chake na kucheza anavyojisikia yeye.

Hayupo fiti tena kucheza kwa dakika 90. Lakini sasa kama Kanoute hayupo ungetaka acheze nani mwingine. Yupo Mkude na ndiye chaguo lililobaki kwa Mgunda.

Kwa upande wa mastraika Simba ndio imefeli zaidi. John Bocco siyo mchezaji wa kumtegemea sana. Naye amecheza muda mrefu. Pia ana majeraha ya mara kwa mara.

Tangu msimu uliopita Bocco amefunga mabao sita tu. Ni pungufu ya mabao aliyofunga Mayele msimu huu peke yake. Sasa utawezaje kushindana na Yanga.

Mchezaji pekee hatari pale mbele ni Moses Phiri. Bahati mbaya naye amepoteza fomu yake hapa karibuni. Ukame wa mabao unamwandama kama mgawo wa umeme unavyoiandama nchi.

Matokeo yake Simba sasa inahangaika kufunga. Nje yupo nani? Habibu Kyombo. Ni mchezaji mzuri, lakini bado hapaswi kuwa tegemeo.

Wachezaji aina ya Kyombo pale Yanga wapo wengi na hawapati hata nafasi. Kina Yusuph Athuman, Crispin Ngushi na wengineo. Lakini pale Simba watu wanataka Kyombo acheze na afunge. Ni ajabu sana.

Hivyo lazima Simba ikubali kuwa ilifeli sokoni. Imeshindwa kupata wachezaji mahiri wa kuifanya timu kuwa hatari zaidi.

Tumeona hili zaidi alipokosekana Clatous Chama. Timu ilikosa ubunifu kabisa. Hakuna mchezaji wa angalau kufanania kile anachofanya Chama. Timu ikawa katika hali mbaya.

Tutamlaumu sana Mgunda lakini kwa kikosi kile hata akaroge Kwamsisi hakuna maajabu makubwa yatapatikana. Simba ikikutana na mechi ngumu itadondosha tu alama. Hasa hizi mechi za mikoani.

Simba pia ilifeli katika benchi la ufundi. Haikuwa bahati mbaya wakaangukia kwa Juma Mgunda. Walikwama na hawakuwa na chaguo zaidi.

Mapema hapa walimleta Zoran Maki. Ni kocha mzuri, lakini hakuwa anaendana na falsafa ya Simba. Uamuzi wake ulikuwa mgumu mno. Unawezaje kukaa na kocha ambaye ana wasiwasi hadi na kiwango cha Chama.

Bahati mbaya huyu ndiye alishiriki kuandaa timu mwanzo wa msimu. Akaondoka wakati mashindano ndiyo yameanza tu. Iliwavuruga Simba hapa. Wangefanya nini?

Kimbilio la haraka likawa Juma Mgunda. Walimchukua kwa ajili ya mashindano ya CAF. Akafanya vizuri wakamwachia na ligi. Sasa unajiuliza Mgunda amewahi kushinda nini hadi utegemee kuwa ataipa Simba ubingwa.
 
Endapo Simba atafanikiwa kushika nafasi ya pili msimu huu, watakua wamepambana Kwa namna ya kipekee sana.Naiona Simba nafasi ya Tatu Kwa taaabu sana.
 
Ikiwa Yanga itachukua ubingwa mwaka huu basi kwa kuponea kwenye tundu dooogoooo maana Simba imewazidi kila kitu...idadi ya magoli..clean sheets etc... yani inawezekana mshindi wa kipindi hiki akapenya kwa point 3 au 2..
Kuna watu hapa watanishukukia kama mvua ya mawe
 
Yani mnavyoandika hizi nyuzi utadhani Simba ni mbovu kuliko..bahati mbaya takwimu zinakuabisha Kwa baadhi ya maeneo,pamoja na Simba kutokuwa na mshambuliajia wanaomtaka wengi lakini ndio timu iliyofunga magoli mengi,ndio timu iliyofungwa magoli machache,kinachowasumbua wavivu kama wewe ni kutamani Simba icheze kama misimu iliyopita kitu ambacho sio kweli,hata wakati inaonekana Simba ina kila nafasi mashabiki uchwara wakiamini imekamilika bado ushindi wake hakikuwa mkubwa kama mnavyotaka kuaminisha watu,Simba iko vizuri ni sehemu chache za kupata watu wa kuongezea. Ni kushinda mechi Tu.
 
Ikiwa Yanga itachukua ubingwa mwaka huu basi kwa kuponea kwenye tundu dooogoooo maana Simba imewazidi kila kitu...idadi ya magoli..clean sheets etc... yani inawezekana mshindi wa kipindi hiki akapenya kwa point 3 au 2..
Kuna watu hapa watanishukukia kama mvua ya mawe
Imewazidi kila kitu na ipo nafasi ya tatu? be serious please
 
Kiufundi kufungwa na sare anazopata simba zina maana kuliko huo ushindi wa bahasha wanaopata yanga Caf champions league na Caf confederation cup ina majibu ya team gani bora kati ya simba na yanga hakuna team inayokuwa bora kwenye league tu halafu kimataifa wanabondwa bahasha hazifanyi kazi.
 
Nyie wenyewe mnachukua bahasha wengine hatawastahili kuchukua? Msimu huu mmechukua bahasha kwa Azam FC na Yanga punguzeni wivu
 
Nyie wenyewe mnachukua bahasha wengine hatawastahili kuchukua? Msimu huu mmechukua bahasha kwa Azam FC na Yanga punguzeni wivu
Mechi ya simba na yanga inavyocheza ni sawa na mechi nyingine?
Jibu swali tuendelee na mada
 
Wakati Yanga wanakwenda kuchukua ubingwa wa 29, Simba wakiwa nafasi ya tatu wanashangilia kombelao la takwimu.
 
Mechi ya simba na yanga inavyocheza ni sawa na mechi nyingine?
Jibu swali tuendelee na mada
Kama Yanga wana mbinu ya kuifunga Simba kwanini wasi itumie kwa timu zingine mpka wagawe bahasha? Pili mlipokea sh ngapi kutoka kwa Azam FC?
 
Mnaongoza point 4 hivyo msijione ni zile 10
 
Barbara kaondoka, lazima tuchukue ndoo
 
Kama Yanga wana mbinu ya kuifunga Simba kwanini wasi itumie kwa timu zingine mpka wagawe bahasha? Pili mlipokea sh ngapi kutoka kwa Azam FC?
Hujajibu swali bado team zikicheza na yanga inampa mpira feisal na mayele wafunge kama vp tuweke dau yanga akishinda hata mechi moja Caf confederation cup tuweke dau
 
Hujajibu swali bado team zikicheza na yanga inampa mpira feisal na mayele wafunge kama vp tuweke dau yanga akishinda hata mechi moja Caf confederation cup tuweke dau
nyinyi hua mnampa awafunge? kwa hizi akili mtasota miaka 10 mfurulizo bila kombe! Kimataifa Yanga kasha mfunga Al Ahly, Club African unataka tu bet nini tena?
 
Hujajibu swali bado team zikicheza na yanga inampa mpira feisal na mayele wafunge kama vp tuweke dau yanga akishinda hata mechi moja Caf confederation cup tuweke dau
Hakika kweli wewe ni mbumbumbu uliye tukuka, Sasa kama Yanga hajawahi kushinda mechi yoyote ya confederation angefika vip hatua ya Makundi!! Ama hakika Ngada haijawahi kumwacha mtu salama.
 
Endapo Simba atafanikiwa kushika nafasi ya pili msimu huu, watakua wamepambana Kwa namna ya kipekee sana.Naiona Simba nafasi ya Tatu Kwa taaabu sana.
Nakazia
 
Hakika kweli wewe ni mbumbumbu uliye tukuka, Sasa kama Yanga hajawahi kushinda mechi yoyote ya confederation angefika vip hatua ya Makundi!! Ama hakika Ngada haijawahi kumwacha mtu salama.
Soma uelewe usikurupuke hivi shule mnasomea ujinga
 
Back
Top Bottom