Je simba walinunua mechi jana dhidi ya alliance?

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Ushindi wa jana wa simba wa magoli 5 dhidi ya Alliance umegubikwa na utata..Alliance waliingia uwanjani bila ya kocha wao mbwana makata ambaye alijiondoa kwenye benchi la ufundi mara baada ya viongozi wa Alliance kumuingilia katika masuala ya ufundi

Makata anadai alikuwa ameshaandaa game plan na line up ila dakika za mwisho viongozi wa alliance waliingia chumba cha kubadilishia nguo na kupanga kikosi chao na kumlazimisha kocha atumie kikosi hicho jambo lililomuudhi mwalimu huyo na kusepa zake hivyo mkurugenzi wa alliance alisimamia mechi hio akiwa kwenye bench la ufundi kama kocha

Mwisho wa siku simba iliibuka ushindi mnono wa magoli 5



 
Sasa hapo simba ananunuaje mechi,wakati sababu ya wao kufungwa goli zote hizo ushaisema
 
Kujiondoa kwa kocha hakuna uhusiano wowote na kununua mechi. Kwasababu

1) kwa maelezo ya kocha ni kwamba viongozi wa Alliance walikuwa wanamuingilia upangaji wa timu kabla hata ya mchezo dhidi ya Simba hivyo hata Alliance alipocheza na timu zinginezo pia ilikuwa ni tatizo hilo hilo.

2) matokeo mabovu ilikuwa ni muendelezo tu wa timu ya Alliance. Hakuanza kupata matokeo mabovu dhidi ya Simba bali hata Yanga na timu zingine zimejipigia.

Kama sababu ndio hizo basi itakuwa timu zote zilizomfunga Allince zimenunua mechi na wala sio Simba pekee.
 
huyo kocha alishaona dalili za timu yao kupigwa nyingi kwa kujitunzia heshima akazusha sababu asiaibike, kama timu ilikuwa inaingiliwa muda mrefu mbona mechi nyingine hakujiweka pembeni
 
Hako katimu ni ka bovu sana, siafiki hoja ya simba kununua mechi! Hata Yanga wangekuwa makini wangekapiga goli nyingi tu
 

Kwa Simba SC hata kama hiyo Alliance ingekuwa na huyo Kocha pamoja na akina Mourinho na Guardiola bado ' Kipigo ' cha ' Shalubela ' kingekuwepo pale pale. Wewe kama Timu ina ' Fundi ' na mwenye Mpira wake na ' Injini ' yenye ' udambwidambwi ' mwingi Clatous Chota Chama kwanini usifungwe idadi kubwa ya Magoli?
 
Inaonekana hio alliance imefika ligi kuu kwa kuhonga sasa anakipata cha moto.
 
Akili ya kuvuka barabara inatosha kujua kwamba Simba haina haja ya kununua mechi. Mnavyoiua Singida hatuoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…