Je, Singida kuna mbuga ya maajabu?!!

Guus

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
1,139
Reaction score
842
Habari wana forum?

Juzi nilikuwa nasafiri kutoka Dodoma kuelekea Singida wakati wa usiku. Nikiwa eneo la Sukamahela, kwa mbali upande wa kushoto nilikuwa naona mwanga mkubwa sana. Mwanzoni nilihisi kuna moto mkubwa, lakini kadri nilivyojitahidi kutazama sikuona "ukimove" kwa staili yeyote kuashiria ni moto. Kwa kweli nilikosa jibu, nikamuuliza mmoja wa "team members" niliyekuwa naye safarini ambaye ni mwenyeji wa mkoa huo, akaniambia kuwa hiyo ni mbuga ya maajabu. Usiku huwa inaonekana kama moto, na inatoa mwanga vivyo hivyo uonavyo.

Siku iliyofuata tulikuwa tukirudi Dodoma (bahati nzuri safari hii ilikuwa mchana). Nilijitahidi nisikopeze hata kope nikiwa maeneo yale ya inayosemwa ni mbuga. Safari hii ikiwa ni upande wa kulia, nilijitahidi sana kulitazama lile eneo. Kwa umbali uliopo toka barabarani, ilikuwa vigumu kutambua kama niliyoona ni nyasi ndefu au miti (lakini hakukuwa na majengo eneo lile).

Hapa nilipo najiuliza, hivi hii inayoitwa mbuga ya maajabu ipo, au ni macho yangu hayakufanikiwa kung'amua vizuri kitu kilichopo umbali ule??? (Msaada mwenye kulijua hili)
 
SINA JIBU LA SWALI LAKO.ILA NAOMBA NIONGEZEE HAYA..
Sukamahela ndio kijiji kilichokuwa katikati ya tanzania.. "yani pale ndio kati ya tanzania".. pale ndipo makazi ya ombaomba waliokusanywa maeneo tofauti walipojengewa makazi
pale bado ni dodoma maana singida inaanzia manyoni..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…