Je sisi Tanzania tuna Jeshi la Polisi au na sisi tuna GESTAPO kama ile ya Hitler wa Ujerumani?

Je sisi Tanzania tuna Jeshi la Polisi au na sisi tuna GESTAPO kama ile ya Hitler wa Ujerumani?

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
861
Reaction score
2,515
Yanayoendelea sasa hivi hapa nchini yamenifikirisha sana na kunikumbusha wakati wa ZCO ACP ya Abdallah Zombe.

Baada ya uchunguzi wa Tume ya Jaji ikagundulika kuwa wale waliouwawa na polisi eti ni majambazi walikuwa wafanya biashara na walichukuliwa na Polisi, kufungwa vitambaa machoni kisha kupelekwa msituni kupangwa foleni na kumiminiwa risasi kama walivyokuwa wanafanyiwa Wayahudi na polisi wa Hitler wajulikanao kama GESTAPO kabla ya vita kuu ya pili ya dunia.

Sasa tujiulize, jee serikali hii ya CCM imeunda jeshi la Polisi (Tanpol) au imenda kikundi chake cha kuendesha mauaji kama kile cha Hitler GESTAPO?
 
Mkongwe taratibu mpaka nimestuka hiyo GEstaPo ilikua kisanga kuliko Ss battalion wale jamaa walikua wanakuja kukuchomoa mbele ya mkeo alafu unakula za kichwa hapo hapo kafie mbele
 
Umesoma ka History 2 kako twisheni ukafanye ka mtihani ka private candidate
 
Back
Top Bottom