Je, striker mpya wa Yanga Fiston Abdul Razaq ni bora kuliko Mo Salah?

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
1.kikosi bora Cha Afcon 2019 alikuwepo

2.Abdul Razaq alimpita magoli Salah kwenye mechi za kuqualify AFCON

 
Tunamtakia kila la heri kwenye timu yake mpya ya Wananchi. Tumeanza na Mapinduzi! Tutachukua VPL na pia ASFC!!

Huu ni mwaka wa Yanga. Wale wanao abudu MAPAKA,watuvumilie tu safari hii. Jambo letu hili ni lazima litimie.
 
hahahaha yaani magoli ya mechi za kufuzu ndiyo unasema kikosi bora cha afcon?jamani hii propaganda kiboko aisee
 
katika magoli 6 aliyofunga matano ni dhidi ya south sudan embu punguzeni munkari utopolo hivi mmesahau kuna kipindi mrisho ngasa alikuwa top joint score wa champions league akiwa na magoal 6 yanga walitolewa round ya kwanza lakini katika round ya awali yanga peke yake aliwapiga wa commoro goals 6 ina maana ngassa alikuwa hatari sana au?
 
Tunamtakia kila la heri kwenye timu yake mpya ya Wananchi. Tumeanza na Mapinduzi! Tutachukua VPL na pia ASFC!!

Huu ni mwaka wa Yanga. Wale wanao abudu MAPAKA,watuvumilie tu safari hii. Jambo letu hili ni lazima litimie.
Mgeni akiambiwa Young Africans sports club anaona bonge la timu, akijiunga nayo sasa na kupelekwa magomeni primary school kufanya mazoezi duh anashangaa mbona hamna tofauti na Lipuli fc.
 
watu wameona picha za top scorers wa kufuzu afcon wanadhani ndicho kikosi bora ch a afcon jamani hahahahahahahaha,pich aimejaa washambuliaji na viungo
Duh watu wanalazimisha furaha kwa kila namna mkileta uongo sisi tunawapa fact check tu...katika hizo 6 zake ,tano kawaotea vibonde wa south sudan.
 
Nyani ni kuwaacha kama walivyo
 
Naona bado unaweweseka na matokeo ya Zanzibar, umebaki kudharau kombe. Mbumbumbu ni mbumbumbu tu.
Nyani ni nyani, ishu ni hadhi ya hilo kombe wewe kima, mumelichua sawa then what next? Kombe la VPL mshindi anashiriki Champions League, Kombe la Shirikisho vile vile mshindi anaiwakilisha nchi ,jee hilo birika lenu umesikia kuna mashindano ya kimataifa ya kuvuta shisha?
 
Kama ulikuwa unayajua hayo ulifuata nn Zanzibar? Msimu huu mjiandae kisaikolojia Ni tofauti na mlivyozoea huwa mna kelele na kejeri nyingi mwisho wa siku mnagwaya gwaya ,Sasa endeleeni kutamba kuhusu kwenye makundi kitakachowakuta huko mtaleta maneno mengine Mara hivi Mara vile kwa maneno haya mnayoongea baada ya kupigwa na kukosoa kombe la Mapinduzi bilashaka mkipigwa kipigo Cha Mbwa koko na kutolewa kwenye makundi mtakuja hapa na vimaneno maneno vya kujifariji badala ya kukiri umeshindwa wapi na kutafakari nn Cha kufanya ili usifungwe tena kwa wakati mwingine ujao.Yani mashabiki wa Simba vigeu hey hatari leo mnaongea hivi kesho mnakataa mlichoongea leo.Mkishindwa muwe mnakiri mmeshindwa msilete sababu za hovyo hovyo mnajidharaulisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…