Je, Taifa la Tanzania limeanguka kutoka mila za mababu na ndiyo maana maandamano yamefeli?

Je, Taifa la Tanzania limeanguka kutoka mila za mababu na ndiyo maana maandamano yamefeli?

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Kukosekana historia ya kupigania taifa leo, imeiacha nchi katika mgawanyiko mkubwa.

Hakuna kitu cha kutuunganisha watanzania kihistoria. Pengine vita ya Kagera ingeweza kutumika kujenga uzalendo wa kuipenda, kuilinda na kutetea uwepo wa haki ili kila mtu afanyapo jambo anakuwa anarejea lengo letu moja nalo ni kulinda maslahi ya nchi na raia waliopo ndani ya mipaka.

Tanzania hilo jambo halipo mfano vuguvugu la uhuru wa Tanganyika wengine wanasema TANU ya wakuja wasomi ndiyo ilitukomboa. Huku kuna upande mwingine unasema la hasha siyo kweli, waliotukomboa wa wazee walioanzisha TAA katika miji ya Tanganyika walipoishi waswahili wengi Tabora, Dar es Salaam, Lindi, Tanga n.k

Likija suala la kushawishiwa kupita imani kuna wanaoamini miongozo ya kiomani kutoka Madina, Mecca, Jerusalem na Rome ndiyo inayowaongoza sawa sawa na siyo miongozo ya wanasiasa wa ndani ya nchi kupitia vyama vya siasa.

Kukosekana huko kwa kitu kinacho
tuunganisha, raia hawaaminiani, makundi ya kijamii hayaaminiani kila mmoja ana mshuku mwenziwe kuwa na ajenda siri. Nchi imekosa mwolekeo wa wapi tuna kutana na kukubaliana kama taifa bila kuingiza masuala ya migawanyiko.

Taifa la Tanzania inabidi liunde historia yake kwa kuanzia inaweza kuwa Vita ya Kagera ikawa ndiyo msingi wetu. Kutuelekeza hatukubali kuvamiwa, hatukubali pande la nchi kunyakuliwa, hatukubali raia wetu wauawe, hatukubali kunyanyasika kwa hali yoyote iwayo.

Huku tukirejea vita vya Kagera itukumbushe hayo, ambayo ndiyo itakuwa dira yetu ya kukataa kuvamiva, kuuza maeneo ya nchi, raia kupotezwa, kutekwa nyara na kuuawa.

Soma Pia: LIVE Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024

TOKA MAKTABA:

UMUHIMU WA KUWA NA KITU CHA KUTUUANGANISHA .

Mojawapo ya programu kuu za Kanuni ya Augustan ilikuwa ule wa upya wa kitamaduni. Kufikia karne ya 1 KK, Warumi wengi waliamini kwamba watu wa Kirumi walikuwa wameanguka kutoka kwa "mores mairoum" au "mila ya mababu" ambayo jiji hilo, na kupitia hilo, ufalme ulianzishwa.

Kwa karne nyingi Roma ilikumbwa na uchoyo, ukosefu wa utulivu wa kisiasa na vita vya mara kwa mara. Baada ya kupata amri ya umoja na "imperium" mwaka wa 27 KK, Augustus alishughulika sana na kuanzisha enzi ya amani huko Roma kwa kutumia wazo hili la upyaji wa kitamaduni.

Sanaa ya Augustan na usanifu kwa kawaida ulionyesha asili ya Kirumi ya mythological sanjari na ukoo wake wa kifalme; kwa ushawishi dhahiri wa Kikale na Kihelenisti, Augustus alianzisha aina ya "lugha ya picha ambayo iliwawezesha wakazi wote wa Imperium Romanum kushiriki katika ufufuaji wa utamaduni wa Kikale na maadili yake huku bado wakihifadhi utambulisho wao wa kitaifa." (Zanker) Vivyo hivyo, Augustus alitumia sanaa na usanifu kama njia ya kueneza propaganda za pro-Principate na kupata upendeleo wa umma kwa makaburi yake ya kifahari ya marumaru.

Suetonius anamshukuru Augustus kama akisema, "'Niliipata Roma iliyojengwa kwa matofali; naiacha ikiwa imevikwa marumaru.'" (Suetonius) Matumizi yake ya Luna Marble pia ni mwelekeo kuelekea ushawishi wa Kikawaida katika programu yake ya uhuishaji wa kitamaduni. Augustus pia alitumia kazi za umma za sanaa na usanifu kama njia ya kukuza familia ya kifalme - katika Res Gestae yake, Augustus anaelezea jinsi anavyoweka wakfu mahekalu na sinema sio kwa jina lake mwenyewe, lakini kwa jina la jamaa zake.
 
WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA HAKI NA KUTUNZA AMANI



Na Mwandishi Wetu, MWANZA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa amewataka viongozi wa dini nchini kuhakikisha wasimamia haki na kuienzi na kusimamia amani kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

"Niwasihi sana ninyi viongozi wetu wa dini kutukumbusha mara kwa mara sisi, waumini na watu wote kuhusu umuhimu wa kusimamia haki na kudumisha amani na kuiombea nchi yetu na viongozi wake" alisema Majaliwa.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa alisema hayo leo tarehe 16 April 2023
 
Back
Top Bottom