Najaribu kufuatilia hizi teuzi za viongozi naona watu wanatolewa na kurudishwa hadi najiuliza kwani nchi yetu haina kabisa sura mpya?
Yani inteligensia ya taifa imezunguka nchi nzima kutafuta vijana hata wasiokuwa serikalini ikakosa kabisa watu wa kuongoza hizo NHC au TTCL? Namaanisha vijana wazalendo ambao wanaongoza kampuni zinazofanya kazi kama hizo waje kuleta kitu kipya.
Hata hao Diaspora nao hawapo? Yani hakuna Mtanzania hata mmoja anayefanya kazi katika kampuni kubwa labda ya mawasiliano anayeweza kuleta kitu kipya.
Watu walewale kila siku na hakuna jipya wanalofanya. Wanasema Rais anajua taarifa nyingi za taifa ila hapa mbona panakuwa pagumu?
Au lazima tuweke watu tutakaoongea lugha moja?