Je tanzania ilishaenda nchi gani kuwekeza kama wafanyavyo mataifa ya nje hapa kwetu?

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229
Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la viongozi mbali mbali wa matifa duniani kuja Tz kusaini mikataba ya uwekezajia katika rasilimali zetu, na Katika kufatilia kwangu mambo ya kiuchumi hasa uwekezaji nimekuja kubaini kuwa sijawahi kuona hata siku moja Tz inasema kuwa imeenda nchi yoyote hasa zile kubwa na zilizoendelea na kwenda kusaini mikataba mikubwa na minono ya kiuchumi na uwekezaji kama wafanyavyo wageni wanokuja hapa kwetu, je kuna mwenye kunisaidia uwekezaji na mikataba ambayo Tz imeenda huko nje na kusaini, kwa mfano:Mkulu wa kaya kwenda USA au china , Thailand, au Ujerumani na kusaini kuwa tz itaanza kuchimba dhahabu yao kwa mkataba fulani, au itaanza kuwinda wanyama wao au kujenga vitega uchumi vya maana (tofauti na balozi uchwara zetu) , naomba kuwasilisha nafasi ya tz katika kuwekeza nje ya nchi kwani yasije kuwa yale yale ya kina chief mangungo wa msovel.
 
Tanzania imewekeza kwenye biashara ya dawa za kulevya,kuna watanzania wana pesa nyingi sana wamewekeza huko,mfano wapo maeneo ya SOUTH AFRIKA,UCHINA,HK,NA ULAYA,,,,
 
Tanzania imewekeza kwenye biashara ya dawa za kulevya,kuna watanzania wana pesa nyingi sana wamewekeza huko,mfano wapo maeneo ya SOUTH AFRIKA,UCHINA,HK,NA ULAYA,,,,
Hilo nalo neno mkuu, kwani yaonekana kuwa tz ni wawekezaji wazuri kwenye hii kitu ya kutumia punda watu.
 
mkuu tanzania ina hela kweli ya kuwekeza wakati kila kukicha bakuli linasuuzwa ready for another round of begging in the world. Leo China, UK, kesho Uswisi, keshokutwa Marekani then Ujerumani mpaka kieleweke.
Utapata wapi hiyo hela ya kuwekeza mkuu? Just do simple mathematics.
 
"Katiba ijayo lazima sasa iondoe kinga kwa marais ili mtu yeyote aweze kumshtaki Rais na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa," Mateo Qaresi (2013).
 
Kuna nchi ya Afrika kwenye ni hivyo visiwa vidogo vya bahari ya Hindi karibu na Madagascar na wao wanaongea Kiswahili(sikumbuki jina lake), Kikwete alisaini huko mikataba. Wafanyabiashara wakitanzania wamewekeza huko.
Na tunaona na CRDB wamefungua tawi Burundi.
Huu uwekezaji unaendana sana na hali ya kipato cha nchi husika.
 
Kwani bado kakibaba hakajaa kutokana na tule tubiashara twetu yuwili tukuu twa gvt trophies (wanyama kama twiga , tembo na wengineo) , pamoja na kale ka zungu la unga , coz naona ni kabishara ambako tunazid kupata soko la uhakika na kuleta ushindani wa kweli hata kwa mataifa yaliyokuwa juu yetu, au waonaje mkuu?
 
"Katiba ijayo lazima sasa iondoe kinga kwa marais ili mtu yeyote aweze kumshtaki Rais na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa," Mateo Qaresi (2013).

Hilo litawezekana tu endapo magmba watang'olewa madarakani coz wakiendelea kuwapo madarakani itakuwa ngumu kwa wao kujihukumu kwa makosa yao wao wenyewe.
 
Hilo litawezekana tu endapo magmba watang'olewa madarakani coz wakiendelea kuwapo madarakani itakuwa ngumu kwa wao kujihukumu kwa makosa yao wao wenyewe.

magamba ni wafanyabiashara ndani ya nchi. Sifa moja ya mfanyabiashara yeyote ni kuangalia opportunities na kukwepa risk. baaaaaasssiiiiiiii
 
Nini kwenda nch nyngne hata manzese kumewashnda.

Sasa sisi ndo tumegeuka na kuwa soko la kimataifa au mnada wa kimataifa wa kuja kuchukua na kuondoka . Hakika TZ itaendelea kuwa shamba la bibi au kichwa cha mwenda wazimu ambacho kila mtu anjifunzia kunyoa.
 
waende wapi mkuuu wa tanzania wamebaki kuuza rasilimali zetu tuangalie watakuja kutuwekeze hata sisi wananchi maana kila kitu kimewekezwa
 
waende wapi mkuuu wa tanzania wamebaki kuuza rasilimali zetu tuangalie watakuja kutuwekeze hata sisi wananchi maana kila kitu kimewekezwa

ok,sasa tufanye hivi, tuwaumbue tu mpaka watakosa pa kujificha coz kila angle itakuwa ishajulikana, ila pia naamini kuwa kiama chao chaja muda si mrefu.
 
Tumeshindwa hata kuwa na maji ya kunywa na ya kuoga, nyumba za kulala, panadol za kututibu maumivu tupatayo kwa maisha mabovu na ya kusukuma siku! Kweli tutaweza kwenda kuwekeza nje ya home!
 
Tumeshindwa hata kuwa na maji ya kunywa na ya kuoga, nyumba za kulala, panadol za kututibu maumivu tupatayo kwa maisha mabovu na ya kusukuma siku! Kweli tutaweza kwenda kuwekeza nje ya home!

Ila hilo nalo neno coz hakuna kimoja tulichojaribu kukifanya , mfano:TATA walianza kiutani utani ila leo ni kampuni kubwa xana duniani. ila bongo bao twaenda mwendo wa kobe katika karne hii ya 21 kwa kujifanya wema sana na kuwakarimu wageni plenty of our endowed resouces , hakika zimwi likujualo halikuli ukakwisha.
 
Azam wamewekeza katika nchi zote jirani na Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…