Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
AfCTA ni wazo ambalo lilizaliwa mwaka 2018 na umoja wa Afrika, na limeanza kufanya kazi kuanzia tarehe 1 januari mwaka 2021. Huu ni mpango ambao ulianzishwa na umoja wa Afrika huku dhamira kuu ikiwa kuelekea agenda ya 2063 ya kurahisisha biashara ndani ya bara la Afrika na kupanua uwanda wa kibiashara wa nchi za Afrika katika soko la kimataifa.
Huu ni mpango ambao unazitaka nchi wanachama wa umoja wa Afrika kuondoa ushuru mpaka kufikia 90% ya bidhaa zake huku wakiruhusu urahisi na upatikanaji wa bure wa bidhaa pamoja na huduma katika bara zima.
Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa, unadai kuwa AfCTA utakuwa ni eneo kubwa zaidi la kibiashara ambayo ni biashara huria duniani kwa kuangalia kigezo cha nchi washiriki.
Mpaka kufikia mwezi Januari mwaka 2022 nchi wanachama zipatazo 41 kati 55 zimeshaidhinisha mkataba wa AfCTA. Mpango huu utakwenda kufungua soko kwa watu zaidi ya bilioni 1.2 huku pato la taifa likitegemewa kufikia mpaka dola trilioni 2.5 katika nchi zote za Afrika.
Tume ya Uchumi ya umoja wa mataifa kwa upande wa Afrika UNECA, imekadiria kuwa AfCTA itakuwa na uwezo wa kukuza biashara ya ndani ya bara la Afrika kwa 52%, hii ni kutokana na kuondolewa kwa ushuru wa bidhaa kutoka nje ya nchi wanachama. Mbali na hivyo, pia mpango huu utakwenda kuongeza wingi wa bidhaa na huduma katika biashara bara bara hii ni baada ya vikwazo visivyo vya kiushuru vitaondolewa, na mwisho kupitia AfCTA tutapata Afrika yenye soko pana la bidhaa zake mwenyewe.

Malengo mapana ya AfCTA ni kutengeneza soko moja la bidhaa, pamoja na huduma, huku pia wakirahisisha harakati za watu ambapo hii itapelekea kuimarika kwa ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi wanachama. AfCTA ina lengo jingine kubwa la kuweka misingi wa kuanzishwa kwa umoja wa forodha wa bara la Afrika hapo mbeleni, ambapo nchi zitatumia mfumo mmoja wa forodha ambao utasaidia sana katika biashara.

Siku ya alhamis katika jiji la Dodoma, katika ukumbi wa bunge tukufu la Jamhuri ya muuungano wa Tanzania kwa umoja wake, liliridhia mkataba wa kuanzisha eneo huru la biashara la bara la Afrika, na kujiunga kikamilifu na AfCTA. Maana yake ni kwamba, Tanzania imeridhia bila kusita kupunguza na baadaye kuondoa kabsa ushuru wa 90% wa bidhaa zinazouzwa chini ya mpango wa AfCTA, na hii ikafungua uwanja kwa Tanzania kuanza mazungumzo na nchi washiriki wa mpango huu, kutazama namna ambavyo AfCTA inateleta baraka ndani ya bara la Afrika.

Tanzania imefanya jambo zuri la hekima sana kuridhika mkataba huu kwa sababu hizi;
1. Tanzania itapata masoko mapya ya bidhaa zake;
Sio suala la kificho kuwa nchi washiriki ikiwemo Tanzania itapata fursa mpya za kupata masoko mapya ya bidhaa pamoja na huduma zake, hivyo Tanzania itaweza kupata wateja wapya katika nchi zingine za Afrika, hivyo kufanya uwezekaji kuwa na ubunifu mkubwa zaidi.
2. Uchumi wa Tanzania utakuwa zaidi.
Sekta ya viwanda ndani ya Afrika huchangia 10% tu ya pato la Afrika kwa wastani wake, kiwango hiki ni kidogo sana ukilinganisha na nchi zingine zinaoendelea. Na endapo mpango wa AfCTA ukifanikiwa basi itapunguza pengo hili, na kadri sekta ya viwanda inavyotanuka basi ndipo viwanda vidogo vidogo vitapata nafasi ya kutengeneza ajira zenye masilahi zaidi haswa kwa vijana na wanawake, hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira na umasikini.
3. Kupungua kwa gharama za uendeshaji
Mpango wa AfCTA utakwenda kuweka ahuweni kwenye mchakato wa kuingiza malighafi kutoka nchi moja kwenda nyingine, hivyo kurahisha uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali. Pia utasaidia viwanda vidogo na vya kati kuanzia viwanda vingine kwenye nchi washiriki, ili waweze kupata nafasi ya uzalishaji mwepesi wa bidhaa kwa ajili ya soko ndani ya nchi husika.

Lakini katika ukurasa mwingine Tanzania ni kama tumeingia mkenge kwa sababu hizi;
1. Mpango huu unaweza kupelekea uchafuzi wa mazingira
AfCTA inahubiri kwa kina sana biashara huria ila haizungumzii balaa la uwepo wa ushindani mkubwa wa makampuni ambayo yatakuwa hayana mipaka, yaani kampuni ya utengenezaji wa samani za ndani kutoka Tanzania likipata wateja Kenya basi inaweza kupelekea ukataji wa miti kwa kiasi kikubwa ili kupeleka bidhaa Kenya kwa wateja wake, AfCTA inaweza kupelekea nchi nyingi kuharibu mazingira ili tu bidhaa zipate kuwafikia wateja. Hili nalo ni kipengele cha muhimu ambacho kama nchi tunapaswa kukiangalia kwa makini.
2. Mazingira duni ya ufanyaji wa kazi na kupotea kwa ajira.
Lazma tujiandae kisaikolojia kwa kuwa ni uhalisi usiopingika kuwa Tanzania hatuna Uchumi imara kama nchi zingine ambazo nazo zimeungana nasi kwenye mpango huu wa AfCTA, nchi kama Afrika kusini ambao wao walikuwa na pato la dola bilioni 361.2 yaani ni sawa na shilingi 852,682,000,000,000/= huku sisi Tanzania tukiwa na pato la dola bilioni 56.6, sawa na shilingi 132,272,000,000,000.
Kitaalamu ni kwamba pato la Afrika kusini ni mara 6.4 ya pato letu, hapo kuna nchi tunaungana na Somalia, Mali, Lesotho, Zimbabwe, Uganda pamoja na Msumbiji kupoteza ajira, endapo tu mataifa makubwa kama Afrika kusini, Misri, Aljeria, Sudani na angola yakiamua kutumia pato lake kwenye uzalishaji mkubwa bidhaa na huduma pamoja na nguvu kazi.
3. Nguvu kubwa ya ushindani kutoka mataifa makubwa.
Ndani ya AfCTA tutegemee kukutana na ushindani mkubwa sana wa masoko, tena kipindi ambacho nch nyingi za Afrika zina Uchumi ambao unategemea kilimo kwa ajili ya kuwapatia ajira watu wake. Hivyo kilimo cha mashamba madogo madogo ambacho kinafanyika Tanzania, Uganda, Lesotho, na Zimbabwe hakiwezi kushindana na kilimo cha ushindani Kinachofanyika kwenye mataifa kama Kenya, Misri, Afrika kusini na Nijeria pamoja na Ethiopia.
Hivyo hapo tujiandae kupoteza mashamba yetu tu, huku tukisubiria kiwango kikubwa zaidi ya ukosefu wa ajira na umasikini.

Bado tuna muda wa kuangalia mpango huu na kujadiliana kwa kina kuhusu mpango huu ili mwishoni tusije kuingia kwenye shimo la nyoka tukiwa tumetanguliza kichwa. Ninafurahi sana kuona mashirikia mbalimbali na asasi za kiraia zikiwa zinazungumza suala la AfCTA katika mijadala yao huku wengine wakisema kuwa AfCTA ni sawa na mipango iliyopo kwenye kasi ya ASEAN pamoja na CARICOM. Yote kati ya yote umakini unahitajika kwa kiwango kikubwa tusije kupigwa kitu kizito.
Nakupenda sana Afrika, Nakupenda sana Tanzania mpenzi wangu.

Attachments
Upvote
2