Je Tanzania ni nchi moja?

Nonda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
13,358
Reaction score
4,307
Nimesoma habari hii

https://www.jamiiforums.com/habari-...amba-ya-zanzibar-naweza-kuitumia-tz-bara.html

Na nimeona michango hii ambayo inanifanya nijiulize je ni kweli kuwa Tanzania ni nchi moja?
Naelewa kuwa wengi tunaamini Tanzania ni nchi moja, mimi si mmoja kati ya hao.
Mimi naelewa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili.

Michango ya wanaJF hawa imenifanya nianzishe mjadala huu.

Itabidi usajili TRA upate namba mpya, vinginevyo usumbufu utakaokuwa ukipata utakukera na kukugharimu sana...hawaelewi somo,na ndo utajua bara na zbr ni nchi moja au 2 tofauti


Je wewe msomaji una mawazo au mtazamo upi?
Tanzania ni nchi moja au Tanzania ni nchi mbili?

Eleza sababu zako.

Kama Tanzania ni nchi mbili, unaweza kuzitaja kwa majina?
 
Wakuu.
Tanzania ni jina la nchi au jina la Muungano?

Je Muungano uliunda nchi moja?

Je Tanganyika na Zanzibar waliunganisha mambo mengapi?

Mambo gani yalibakia katika mamlaka ya Tanganyika na mambo gani yalibakia katika mamlaka ya Zanzibar?

Mambo yepi yaliitwa mambo ya Muungano?

Na Muungano iliitwa kwa jina lipi?

Jina Tanzania liliundwa lini? Kwa sababu gani?

Kabla ya Mwalimu kubadilisha jina la Muungano...je kulikuwa na nchi ngapi?
 
Mimi ninavyojua majina na vitendo ni vitu tofauti. Tanzania ni nchi moja yenye kisiwa cha Zanzibar ambacho kina uhuru wake na namna fulani.
 
Leo 2011....Je kuna mambo ambayo bado yapo chini ya Mamlaka ya Tanganyika (Tanzania bara)?

Je kuna mambo ambayo bado yapo chini ya Mamlaka ya Zanzibar?

Kwa sababu gani mambo ya Muungano yamekuwa yakiongezeka?
 
Mimi ninavyojua majina na vitendo ni vitu tofauti. Tanzania ni nchi moja yenye kisiwa cha Zanzibar ambacho kina uhuru wake na namna fulani.
Mkuu.
Tanzania ina visiwa vingapi?
Kwa nini Kisiwa cha Zanzibar tu ndio chenye uhuru wake na namna fulani?
 
Tanzania ni nchi moja iliyotokana na muungano wa nchi mbili. Lakini hali ya sasa inaonesha ni nchi mbili zilizo lazimishwa kuwa moja
 
Tanzania ni nchi moja iliyotokana na muungano wa nchi mbili. Lakini hali ya sasa inaonesha ni nchi mbili zilizo lazimishwa kuwa moja
Mkuu.
Nchi mbili ziliungana kuwa nchi moja au ziliunganisha mambo kumi na moja tu na kubaki na yenyewe mengine yaliyobaki?
Kama zililazimishwa, nani alilazimisha?
 

Kwanza kabisa mkuu, hii kitu ni contradiction kwenda mbele, kabla sijaendelea sana, naomba nikudokeze vitu vichache- Zbr ni nchi ambayo pamoja na vitambulisho vingi vya nchi vilivyopo, ni hivi majuzi tu wamezindua mamlaka ya mapato ya kwao binafsi ZRA, mbali na TRA, pili, wapo katika mipango ya kuanzisha Central bank yao, na michakato ikienda vizuri, majeshi ya ulinzi na usalama kure-place TPF na TPDF, then kwenye swali; Authorities zote zinazojiita za JMT zilipaswa ku-affect Zbr kama ilivyo kwenye huu upande usio na jina (maanake ukisema bara sharti uwe na nchi inaitwa visiwani, sasa hivi haipo, Zbr ndiyo nchi)- ukisema nchi ni mbili, basi moja ni Zbr,na ingine haina jina, na rais wake ata-hang somewhere like you said. Kwa kweli swali lako linarudisha contraverse kubwa sana ambayo wengi hawaijui, au wameipuuzia pale wanapofikiria kudumisha fikra (sahihi-my leg) za ....
My fella, people just stop thinking ikija kwenye kujadili mada ngumu! Well, this is a mythical union, kama wako tayari, na wanpenda muungano, well lets define this thing!
 
Tanzania ni nchi moja iliyotokana na muungano wa nchi mbili. Lakini hali ya sasa inaonesha ni nchi mbili zilizo lazimishwa kuwa moja
Mkulu wetu anatoa kauli tofauti tofauti.

Kuna ile: Zanzibar ni nchi ndani lakini nje si nchi.

Leo amekuja na hizi, Kauli hizi ziko katika hotuba yake kutoka link hii. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ri;-asema-madai-ya-walimu-hayatekelezeki.html

1. Kwa ujumla tumeridhika kuwa utekelezaji umekuwa mzuri kwa upande wa mamlaka zinazohusika na usafirishaji majini yaani SUMATRA, Zanzibar Maritime Authority na mamlaka za Bandari za nchi zetu mbili.

2. Baraza limeagiza vyombo hivyo viwe na hadidu za rejea zinazofanana kwa vigezo vya ubora ili nchi yetu iwe na viwango vinavyofanana vya ubora wa meli na huduma za usafirishaji baharini kwa pande zetu mbili za Muungano.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…