Je, Tanzania ni taifa la kidini?

ASIWAJU

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
1,938
Reaction score
1,632
Habari za saa wanachama wa hii platform pendwa, nilikuwa na swali muhimu kwenu wanachama lenye kuhitaji majawabu kutoka kwenu.

Swali lenyewe muhimu ni hili:-
Je Taifa letu la Tanzania ni la kidini au sio la kidini ?

Tafsiri nyepesi zaidi ya swali langu ni hii: Je taifa letu Tanzania ni la wale tu wenye dini za kikristo na kiislamu[ ndizo dini za serikali ya Tanzania] au ni taifa lisilo egemea katika dini yoyote ile ?

Karibuni wajuvi wa mambo mpate kunijuza kwa faida yangu na ya wanachama wengine.
 
"Nchi yetu haina dini ila watu wake wana dini-" Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.🙏🙏🙏
 
Dini ni Imani !! Kila mtu hapa Nchini ana imani yake na ndio dini yake !!
 
Rais anapoandaa mambo ya Hijja na serikali kutoa pesa kwa suala hilo, jibu liko wazi.
 
Serilali na Ccm kwa sasa ni kama kamati ya hijja au baraza la maulid
Kwa hiyo taifa letu la Tanzania ni la kidini si ndivyo unavyo maanisha ndugu ?
 
"Nchi yetu haina dini ila watu wake wana dini-" Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.🙏🙏🙏
Ila ina jishikiza kwa dini kuu mbili [ uislamu na ukristo ] je nipo sahihi juu ya kauli yangu ?
 
Dini ni Imani !! Kila mtu hapa Nchini ana imani yake na ndio dini yake !!
Serikali ya taifa letu imejishikiza katika dini kuu mbili uislam na ukristo je nipo sahihi na kauli yangu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…