Jacob Mulikuza
Member
- Jul 15, 2021
- 16
- 61
Mwaka 2014, Benki ya Maendeleo ya Afrika iliandaa kongamano lililofanyika nchini Rwanda ambalo nilipata abra ya kusikiliza. Kongamano hilo, lilikuwa linafanya kumbukizi ya kila mwaka ya Benki ya Maendeleo ya Afrika iliyoanzishwa Julai Mosi, 1966; liliongozwa na tafakuri isemayo ‘Uongozi na Afrika tuitakayo’.
Kongamano hilo, lilialika wageni mbalimbali mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali Afrika na duniani kote. Jambo lililonivutia zaidi, ni viongozi wakubwa wa nchi kuwa sehemu ya mjadala hususan, marais waliokuwepo na waliopo madarakani na wale waliopita wakijadili namna ambayo uongozi sahihi na madhubuti utawezesha kupata Afrika mpya.
Marais walioshiriki kwenye majadiliano walikuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais Kenya William Ruto wakati huo alikuwa makamu wa Rais, Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, Rais mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na Rais mstaafu wa Tanzania hayati Benjamin Mkapa.
Nilifarijika sana kusikiliza kongamano hili, kwani lilinipa fikra mkururo baada ya kusikiliza matamanio ya viongozi wetu wa sasa na waliopita juu ya Afrika wanayoitamani. Fikra hizi, zinaenda sawia na mjadala chokozi ulianzishwa na JamiiForum ambazo zimenifanya kuandika makala hii nikijiuliza, je, tunajua Tanzania tuitakayo kama taifa?
Kwenye karne hii ya ishirini na moja, ni vyema tukaanza kufikiri kama Afrika kwa pamoja na kuacha kujigawa kwenye mipaka tuliyochorewa tangu enzi za ukoloni. Kuendelea kufikiri ndani ya mipaka yetu, kunatuvunja nguvu kama bara na kuendeleza matatizo dungudungu yaliyopo kwenye kila nchi husika. Aidha, huwezi kutamani Afrika bora bila kuanza na nchi bora kwanza. Hivyo, tafakuri yangu itajikita kuangazia Tanzania tuitakayo kwa sasa na mustakabali wake.
Ni dhahiri shahiri kuwa, kwa miaka 63 ya Uhuru na miaka 60 ya Muungano; taifa letu limepiga hatua lukuki kwenye kila nyanja ya maendeleo. Hii sio kusema hapakosi changamoto, la hasha! Kumekuwa na maeneo mbalimbali ambapo kama taifa tumekwenda shelabela na tungehitaji kuboresha ili kuwa na taifa bora litakalovutia nchi zingine barani Afrika na mwishowe kuwa na Afrika bora kwa ujumla.
Tuanze kutafakari mfumo unaotumika Tanzania leo hii kuongoza taifa letu. Kwenye katiba yetu ya mwaka 1977 mfumo rasmi tunaoutambua ni Ujamaa na Kujitegemea, ambao sina hakika sana kama bado Imani yetu iko huko ama tumeshatoka. Hoja ya msingi hapa, tunapaswa kama taifa kuwa na mfumo bora utakaoongoza taifa letu kufika maendeleo tunayoyahitaji. Mfumo huu, utatufanya sote kwa pamoja tuamini na kutenda vile ambavyo mfumo utatuongoza. Tunahitaji mfumo imara na shirikishi utakaotokana na watanzania wenyewe ambao pamoja na viongozi tunaowapa dhamana watauamini na kuuishi na kila mara kuupambanua.
Kwa kukosa mfumo thabiti na sahihi, historia inatuonyesha kila zama hubadilika kutokana na hulka ya kiongozi. Pindi, tunapobadili uongozi na mfumo ama aina ya uongozi hubadilika na kuongoza kwa kadiri ya maono ya kiongozi husika na sio kutokana na mfumo wa nchi. Tunahitaji mjadala wa kitaifa kupata mstakabali wa mfumo sahihi wa kuiongoza nchi yetu, yamkini maandalizi ya katiba mpya yanayoendela yataweza kujibu hoja hii na kutufikisha pale tunapostahili.
Mataifa mengine kama Marekani, mfumo wao rasmi ni Ubebari na wanautukuza na unawanufaisha, China wao wanamfumo jumuishi wa Kisoshalisti na Kibepari ili hali Uingereza wao ni mfumo wa Soko Huria. Hivyo, kuwa na mfumo thabiti kama taifa utatuwezesha kujitambulisha kama taifa na kuacha kuwa wafuasi wa nchi za Magharibi. Taifa letu bado ni tegemezi kwa mikopo na misaada kutoka kwa wahisani ambao huja na masharti kemkemu nasi kwa hofu ya kukosa fedha hizo tunapiga goti na kusema hewala. Hivyo, endapo tutakuwa na mfumo thabiti itatuwezesha kuwa na taratibu sahihi za uzalishaji mali zitakapunguza ama kuondoa mikopo kandamizi.
Kwa miaka ya hivi karibuni, msisitizo umewekwa kwenye Tanzania ya viwanda. Ni jambo jema na linavutia kusikia, ila mikakati ya kupata nchi ya viwanda bado haiko wazi. Swali llinalonijia mara nyingi, je, tunataka nchi ya viwanda vya wawekezaji wa nje ama watanzania wenyewe (hivi sasa wanaitwa wawekazi wa ndani)? Je, tunajua ni viwanda aina gani tunahitaji ama tunahitaji viwanda mseto?
Kama tunataka Tanzania ya viwanda vitokanavyo na watanzania wenyewe ni vyema tukaanza kuboresha na ama kubadili mfumo wetu wa elimu kwa ujumla. Hivi karibuni, natambua wizara ya elimu imeeleza mabadiliko itakayoyafanya kwenye seka ya elimu kuanzia mwaka 2027 na kwa kuwa bado mabadiliko hayo hayajafanyika ni vyema tukajiuliza, je, elimu tunayotoa kwa vijana wetu leo inakidhi mahitaji? Je, viwanda vitapatikana kwa aina hii ya elimu? Je, msisitizo wa elimu utabadilika kutoka kwenye kuajiriwa kuwa kujiajiri?
Alhasili, kama elimu yetu kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu haitobadilika, kamwe, hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda vya watanzania wenyewe ila tutakuwa na Tanzania ya viwanda vya wawekezaji kutoka nje ya nchi huku watanzania wakibaki kuwa wafanyakazi katika viwanda hivyo wakilipwa mishahara kidogo na kuleta migomo kila kukicha.
Namna bora ya kufikia Tanzania ya viwanda itakayotufikisha kwenye uchumi wa kati, ni kufanya mbadiliko sahihi na kwa dhamira ya dhati kwenye mfumo wetu wa elimu utakaosaidia vijana wetu kuwa wabunifu, wenye kutumia teknolojia hususan akili mnemba (Artificial Intelligence). Mabadiliko ya elimu yetu yanapaswa kuzingatia vitendo zaidi badala ya nadharia kwani viwanda vingi vinahitaji watu wenye ujuzi zaidi wa kutenda.
Tukiangazia swala la kilimo, Tanzania bora tunayoitaka ni ile yenye kilimo chenye tija kwa watu wake, kwani kilimo ni uti wa mgongo kama alivyotuasa Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Nyerere. Takwimu za NBS za mwaka 2019/20 zinaonyesha 65.3% ya watanzania ni wakulima walio vijijini ambao huzalisha mazao ya Biashara na chakula kulisha taifa letu na mataifa mengine ya Ulaya na Marakeni. Kilimo cha taifa letu kinaongozwa na propaganda nyingi na kauli mbiu mpya kila kukicha zinazoasisiwa na viongozi wapya madarakani kila uchao, hivyo, ni muda sasa kilimo chenye tija kikarudi mikononi mwa wakulima wenyewe. Kwenye vikao vya hivyi karibuni bungeni, tumeshughudia taarifa zikitolewa wanufaika wakubwa wa fedha za kilimo ni wajanja wachache wanaopora kutoka kwa wakulima wetu kwa njia za udalali ama zabuni.
Natambua kuwa nchi yetu ina wataalamu wengi sana wa kilimo na wamefanya tafiti nyingi na mbalimbali juu ya kilimo chetu. Je, tafiti zinazofanywa na wataalamu wa kilimo zinafanya nini kusaidia kuboresha kilimo cha taifa letu na wakulima wa chini kabisa? Ni vyema sasa tukafanya tafiti za kilimo zenye tija badala ya zile za kuongeza shahada na kuishia kukaa kwenye makabrasha na kula vumbi ofisini tu. Tafiti hizi zitusaidie tuondokane na kilimo cha jembe la mkono, kutegemea mvua, tuondokane na wadudu waharibifu na mengine mengi. Hapa nataka kusema, tafiti zilizopo na zilizofanywa ziwe hai kwa kutumiwa badala ya kufaidisha wahisani walizoziomba.
Kwa upande mwingine, Tanzania tuitakayo ni ile yenye uongozi bora na imara. Uongozi sio tu changamoto kwa Tanzania bali Afrika kwa ujumla. Je, tuna viongozi wa namna gani? Je, viongozi hawa wanaamini nini? Je, viongozi hawa wanamienendo gani? Je, viongozi wetu wako kwa maslahi ya nani? Ni maswali ya muhimu yatakayoweza kutusaidia kutofautisha kati ya kiongozi na mwanasiasa. Kwani mtu anapaswa kuwa kiongozi kwanza kabla ya kuwa mwanasiasa, lakini uhalisia sivyo ulivyo.
Taifa letu bado linachangamoto ya uongozi, japo leo hii kila mtu anamini anaweza kuwa kiongozi. Viongozi wengi tulionao leo hii hawako kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wa chini bali wengi huangali maslahi yao zaidi. Taifa hili linahitaji viongozi wenye nia ya kulisogeza taifa hili mbele kwa kushirikana na watu wanaowaongoa badala ya wao kuwa viongozi wajuzi. Tunahitaji viongozi wabunifu na wenye kufanya mambo kwa weledi na sio wale wakuamriwa na kutenda bila kufikiri. Tunahitaji viongozi majasiri wanaoweza kusema ukweli wakati wote bila kujali watu watasemaje. Na pia tunahitaji viongozi ambao watajua ya kuwa maamuzi ya kisomi yanayozingatia utafiti ni bora kuliko maamuzi ya kisiasa ambayo yatawafurahisha wanasiasa kwa kuwa wanawapa ugali wa kila siku. Ni muda sasa tuweze kama taifa kutofautisha siasa na uongozi ili kuifikia Tanzania tunayoitaka.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika sote ni ndugu tutende kama taifa

Upvote
62