Kuna tatizo hapa kwamba wengi wanaochangia mada hii sio waelewa wa masuala haya na bahati mbaya hawajawahi hata kuishi nchi jirani kujaribu kuona maisha na vitu kule vinaendaje kulinganisha na vyetu hata kidogo hili ni tatizo kubwa sio kweny nyie wachangiaji tu bali ni janga la kitaifa kuwa na wananchi mambumbumbu kazi kungoja propaganda na ngojera zingine zisizokuwa na msingi zinazofanya wananchi wanazidi kuwa waoga na kutotaka hata kujiendeleza zaidi hili ni tatiso sugu ndugu zangu .
Tukiacha hayo hapo juu naamini serikali yetu haina watu wasiofikiria kwenye idara mbalimbali za utendaji hata inapoamua kuingia kwenye mashirikisho kama haya inakuwa imeshaona faida Fulani hata kama sio sasa hivi hata huko mbeleni sio lazima iwe miaka 2 au 4 ijayo hata 50 ijayo angalia nchi kama marekani zimejengwa kwa miaka mingapi mpaka sasa hivi tena kwa ushirikiano kati ya nchi zaidi ya 20 sasa kwanini hilo lishindikane hapa kwetu tena tunauelewano mkubwa kuliko walivyo wao siku zilizopita
Jamani sasa hivi dunia inazidi kuwa kikiji kimoja kila nchi na jamii duniani inataka kujikomboa na kujenga ushirika na majirani zake ili kuleta maendeleo kwa watu wa maeneo hayo kwahiyo hata sisi ni sehemu za jamii hizo tunataka maendeleo lazima tuungane tumalize tofauti zetu tujenge nchi zetu kama ilivyo umoja wa ulaya , USA na muungano wa nchi sehemu mbalimbali duniani .