NIMEULIZA HIVYO KWANI WATANZANIA WENYEWE TUKIENDA KUNUNUA VITU VYA KUTUMIA NYUMBANI TUNAULIZA VITU VYA KENYA.MFANO WA VITU HIVYO NI SABUNI PANADOL,SUFURIA YAANI VILE VITU VINAVYO TUMIKA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU.NA ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA WAMEKUWA NA WASIWASI HATA WALE WENYEVIWANDA AMBAO SISI AKINA KAJAMBA NANI TULIFIKIRI WATACHEKELEA.jE NINI KIFANYIKE WAKUBWA?
Ndugu yangu uko eneo gani la nchi hii ? Mimi niko moshi sasa hivi na kila ninachotumia kila siku nanunua toka viwanda vya Tanzania idadi hiyo imekuwa inaongezeka kila siku hata nilipokuwa Nairobi siku 3 zilizopita niliweza kupata mahitaji haya haya ninayoyataka kwa kununua bidhaa za Tanzania nikiwa kwenye nchi ile , kwasasa viwanda vyetu vinajitahidi sana na uchumi wetu unakuwa kwa kasi ya ajabu labda miaka 10 inayo Tanzania inaweza kuwa kinara kwenye soko la pamoja na afrika mashariki kama hali ikiendelea kuwa kama ilivyosasa hivi .
Na kwa msisitizo unachoweza kufanywa kwa urahisi zaidi kwenye shuguli za soko hili ni mfano
Wewe uko njombe unashona vikapo vile vikapo sasa vitaweza kuuzwa Kenya au Rwanda bila masharti na sheria zingine ambazo zilikuwa zinazuia bidhaa kama hizo toka nchi moja au nyingine kama huwezi kuuza wewe basi kuna vyama vya wafanya biashara vinavyonunua vikapo hivyo na kuvipeleka kwenye masoko mengine ya nchi jirani kama kungekuwa na tatizo kwenye jumuia kitu kama hicho ni ngumu kufanya hilo ni moja
Lingine ni kwamba kuna baadhi ya vitu vitafanyika kutokana na sheria za nchi husika kama masuala ya ardhi na zingine zingine
This is our challenge. there is no more a room for blur blur.
We need to be serious on our makings, offerings and mindset.
Kuna tatizo hapa kwamba wengi wanaochangia mada hii sio waelewa wa masuala haya na bahati mbaya hawajawahi hata kuishi nchi jirani kujaribu kuona maisha na vitu kule vinaendaje kulinganisha na vyetu hata kidogo hili ni tatizo kubwa sio kweny nyie wachangiaji tu bali ni janga la kitaifa kuwa na wananchi mambumbumbu kazi kungoja propaganda na ngojera zingine zisizokuwa na msingi zinazofanya wananchi wanazidi kuwa waoga na kutotaka hata kujiendeleza zaidi hili ni tatiso sugu ndugu zangu .
Tukiacha hayo hapo juu naamini serikali yetu haina watu wasiofikiria kwenye idara mbalimbali za utendaji hata inapoamua kuingia kwenye mashirikisho kama haya inakuwa imeshaona faida Fulani hata kama sio sasa hivi hata huko mbeleni sio lazima iwe miaka 2 au 4 ijayo hata 50 ijayo angalia nchi kama marekani zimejengwa kwa miaka mingapi mpaka sasa hivi tena kwa ushirikiano kati ya nchi zaidi ya 20 sasa kwanini hilo lishindikane hapa kwetu tena tunauelewano mkubwa kuliko walivyo wao siku zilizopita
Jamani sasa hivi dunia inazidi kuwa kikiji kimoja kila nchi na jamii duniani inataka kujikomboa na kujenga ushirika na majirani zake ili kuleta maendeleo kwa watu wa maeneo hayo kwahiyo hata sisi ni sehemu za jamii hizo tunataka maendeleo lazima tuungane tumalize tofauti zetu tujenge nchi zetu kama ilivyo umoja wa ulaya , USA na muungano wa nchi sehemu mbalimbali duniani .