SoC02 Je, tasnia pekee ya uchoraji tamaduni wa Tingatinga upo mikono salama katika karne hii?

SoC02 Je, tasnia pekee ya uchoraji tamaduni wa Tingatinga upo mikono salama katika karne hii?

Stories of Change - 2022 Competition

Young A-chancellor

New Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
4
Reaction score
0
Screenshot_20220808-134811_YouTube.jpg


Tuanze na mwanzilishi na mgunduzi wa tamaduni hii ya sanaa tingatinga. Edward Said Tinga Tinga mwenyewe, bila shaka unamfahamu! Kama la basi muulize babu yako vizuri maana huyu jamaa ndio habari ya mjini enzi za sabini ivi


Alipokuja zake dar 1968 na kuchukua mafuta ya baiskeli na kipande cha ubao wa kuzibia paa za nyumba za kisasa na kutunga michoro yake ang'avu iliyo wakilisha jamii ya watu na mazingira walioishi. Na watu walivutiwa na mchoro wake wa kwanza tu! wa jamaa
Screenshot_20220808-134650_YouTube.jpg

Na akaipa jina Lake la ukoo wa kimakonde.. Tinga-Tinga.

Bwana Edward yeye alikuwa na lengo tu la kuweka msosi mezani na ndo maana hata michoro yake hii haipo maala tadhnifu ambapo tunaweza tukasema tunamuenzi vyema eti!!. Eti kuna za chinichini kwamba kabla hajabuni mchoro wake huo wa kwanza aliwahi fanya kazi katika nyumba ya mkongo mmoja kanda ya kaskazini magharibi na ndipo alipopata wazo hilo...

Akati kisanaa hiyo tunaita hamasa,mhemmko! Ambao unaleta mawazo mapya ya kisanii
Bwana Edward Said alijozolea umaarufu mwisho wa miaka ya sitini mwanzo wa miaka ya sabini. Kabla ya umauti kumkuta mapema kabla hata hajafaid matunda yake jamaa huyu pale
Screenshot_20220808-134259_YouTube.jpg

Samora avenue mwaka 1972 ikiwa ni miaka minne tangu aanze kazi yake hiyo ya kutukuka katika tasnia ya uchoraji lo!

Oh! Utakuwa unajiuliza ilikuaje mpaka mtu anafia katikati ya mji namna iyo? Basi kibaya ni kwamba aliuwawa na polisi wenye gadhabu kwani jamaa alitoka kulewa msasani na mshikaji wake wakapanda gari na kuendesha uku wakiwa chakari. polisi waliwapungia mkono bila ufaulu na ikabidi wajichukulie sheria mkononi kuwatia adabu vikali. risasi zilishambuliwa katika gari Lao na saba zikampata hayati bwana Edward Said Tingatinga.

Screenshot_20220808-134356_YouTube.jpg

Duh! Jamani!! Sio poa.
Sasa ilikuwaje sanaa ikaendelea hataivyo? Nani aliendeleza Ubunifu huu? Alitumia umahiri ule ule jamaa aliyefuata au la!?au alijiongeza?

Bwana Simon George Mpata ndiye alirithi mikoba. ndugu huyu wa hayati TingaTinga alikuwa mwaminifu kulienzi jina la sanaa na hata kuitafutia soko huko nchini Kenya Nairobi ambapo alikutana na bwana Kazumi Oguro mtayarishaji wa magazeti nchini japan
Screenshot_20220808-162112_Google.jpg

Ebwana! apigiwe makofi mengi sana bwana Simon George Mpata katika kutanua njia Pana iliwoje katika tasnia sanifu ya tingatinga kwa sababu gani nakwambia ivyo! Ukienda Google sa hii na ukabofya jina la huyu mjapani hapo kitu cha kwanza kitakachotokeza si kingine bali sanaa ya mkongwe wetu Bwana Simon George Mpata
Screenshot_20220808-162028_Chrome.jpg

Tena kazi yake hii sanifu ndo itajitokeza huu ndo ushindi tunaotaka bana eh!! Kwamba huyo mjapan anatumika kama kitenzi kiunganishi tu! Japokuwa ana mchango

Simon George Mpata alizaliwa mwaka 1942 aliaaga dunia mwaka 1984 mdogo mtu kaka wa kambo kwa mgunduzi Said Tingatinga

Ambaye mchango wake mkubwa ulikuwa ni kuipa umaarufu mkubwa sanaa ya tingatinga nchini japan mpaka Leo hii. Amini eti kunawachoraj wa tingatinga wanapata shavu ya kwenda japan kuchora kuta na mageti makubwa mpaka sasa. na kama hujui.. mahusiano makubwa ya bara la asia na Tanzania yaliunganishwa na sanaa tamaduni kama unabisha! google.

Asa, Simon Mpata bwana!! Hadithi yake sio ndefu sana!! Maana inagongana na ya yule mkongwe mfuata nyayo mtaalam! George Lilanga yaani huyu ndo kiboko balaa!! Baadhi ya magazeti nchini ulaya yalidhubutu hata kumwita Picasso wa Afrika maana!aliitumia nafasi vilivyo!michezo weka kando.Aliwahi tengeneza kazi miamoja za sanaa katika kazi miambili na themanini zilizo kusanywa kutoka kwa wasanii wa kiafrika kwenda jijini Washington marekani mwaka 1978 yani da! we acha tu

Screenshot_20220808-132631_Chrome.jpg

Ninachojaribu kukuonesha hapa ni jinsi tasnia hii ilivyopanda na kushuka ķatika karne mbili zilizo pita ghafla mbele ya macho yetu bila hata sisi kutambua. Leo hii ukiangalia orodha ya sanaa ya uchoraji kumi bora zinazovuma hapa afrika hakuna hata moja itokayo Tanzania hata katika magazeti tofauti tofauti kama @artnet @artspar ambayo haya ni magazeti makubwa ya takwimu za kisanaa sababu pia hata ivyo sanaa ya tingatinga ipo katika majumba makubwa ya maonesho ya sanaa uko ufaransa, italia,ujerumani,japan na nchi nyingine kibao aina ile ya michoro mingine kabisa ya bwana George Lilanga ambayo ntapata kukuonesha kesho

Bwana Said Tingatinga alikuwa mgunduzi na mzalishaji, bwana Simon Mpata alieneza na kusambaza Mchele huo wa sanaa na mwishowe bwana George Lilanga alibeba tasnia iyo ulimwenguni hawa napenda waita utatu mtakatifu.

Nikutakie siku njema mpenzi msomaji tukutane kesho mida kama hii nipate kukujuza zaid nina mengi ya kukujuza
 
Upvote 0
Back
Top Bottom