Je TCRA au Mamlaka ya Tanzania wanaweza kusoma meseji za Whatsapp? Au zile za kawaida kwenye iPhone?

Je TCRA au Mamlaka ya Tanzania wanaweza kusoma meseji za Whatsapp? Au zile za kawaida kwenye iPhone?

Whatsapp hawawezi soma msg wala kusikiliza calls yoyote!

Kwenye msg na calls za kawaida wanaweza soma na kusikiliza kwa sababu zinapitia kwa mtoa huduma (tigo,voda, airtel nk)
Asante sana. Nilikuwa na hizo hisia. Nadhani issue za privacy kwa bongo huko mna tabu sana
 
za whatsapp, wataweza ziona ila hawataweza zielewa, maana zinakua ni makorokocho(encrypted)
 
Hata mke wako anaweza kusoma msg zako zote au akajua namba zote unazowasiliana nazo and vice versa.
Wewe tu hujaamua.
 
Kuna program iliyoundwa Israel inaitwa Pegasus inadukuu kila kitu
Wakumbuka mawasiliano ya Kinana, Makamba snr na Nape yalivyodukuliwa?
Ukianza kuandika au kuongea chochote inadukuu mpaka taswira yako.
Watawaka wa nchi zote za kiimla wanatumia.
 
Great Thinkers,

Naomba kufahamu, je mamlaka yetu nchini inaweza kusoma jumbe za whatsapp? Na je zinaweza pia soma texts za sms za kawaida kwenye simu za iPhone?

Asanteni.
Yes, wanaweza. Hiyo ni kazi rahisi kabisa hata wewe mtu binafsi unaweza kuifanya. Siku hizi teknolojia imekua Sana, Spyware za kufanyia kazi hiyo zipo nyingi Sana, na zinapatikana kwa urahisi kwa gharama nafuu Sana.

Siku hizi kuna Spyware nyingi Sana za kudukua mawasiliano ya simu, 'mawakala wa wale jamaa' wamepewa au kuwekewa program za aina hiyo kwenye simu zao. Aidha, hata hardware za kudukua mawasiliano ya simu za watu pia zimesambazwa nyingi Sana huko mitaani, a lot of the Spyphones have been distributed to the agents who available within the streets. Endapo kama vifaa vya kung'amua hivyo vifaa vya kudukulia mawasiliano ya simu (Spy Catchers) vingeruhusiwa kutumika kwa raia wa kawaida, Basi nafikiri Wala usingeweza kuuliza swali Kama hilo.
 
Back
Top Bottom