Je, tetesi kwamba matokeo ya uchaguzi uliomalizika Simba Sc yanachangia kuathiri uwezo wa timu uwanjani, zina uzito kiasi gani?

Uchawi una nafasi katika mpira duniani. Sio Tz au Africa pekee.

Porto wameajiri mganga huko na yuko kwenye payroll ya timu.
Ni baada ya Benfica misimu iliyopita kuajiri mganga halafu wakachukua ubingwa.

Porto wakasema usitutanie. Ulaya hiyo.
Hii siamini hata kidogo. Hao waganga watia hamasa tu kuwaaminisha wachezaji kutia bidii.

Ingekuwa hivyo vitu vinafanya kazi basi Katavi Rangers ya Sumbawanga (wakati ule) au Reli Kigoma wasingeshuka daraja. Nawngekuwa wanabeba ubingwa hadi leo.
 
Hapa tuko pamoja, uchawi ni kucheza tu na akili ya mpinzani wako, hakuna zaidi ya hapo.
 
Hii siamini hata kidogo. Hao waganga watia hamasa tu kuwaaminisha wachezaji kutia bidii.

Ingekuwa hivyo vitu vinafanya kazi basi Katavi Rangers ya Sumbawanga (wakati ule) au Reli Kigoma wasingeshuka daraja. Nawngekuwa wanabeba ubingwa hadi leo.
Sasa kwani factor ni moja?

1)Uchawi una asilimia zake
2)ubora wa kikosi
3) bahati
4)rushwa(refer Juventus 2007)
nk
 
Chealse hii ni tofauti na Chaelse ya Ibrahimovich wakati akaimwaga pesa za kusajali,hata Mazembe,Enyimba baada ya kupunguza kupump pesa kwenye usajili sasa hivi izo timu zimekua sio tishio tena kama zamani.

tukirudi kwenye mada jibu ni hapana makundi ayahusiki na perfomance ya timu uwanjani.mchezaji anapata nafasi nne afungi hata moja tena ingekua mechi moja tungesema leo hakuwa na bahati lakini jambo hilo la kukosa magoli linatokea zaidi ya mechi nne mpaka tano,tena kabla hata makundi ya uchaguzi hayajaibuka,sasa hapo makundi yanahusikaje na mchezaji kukosa magoli nafasi mpaka nne?
 
Kosa limeanzia kuleta kocha mpya wakati usio sahihi. Simba hakukuwa na tatizo la kocha, walihitajika wachezaji wazuri kuongeza uwezo wa kufumania nyavu.
Hiyo pesa waliyomsajilia kocha ni bora wangenunua wachezaji wazuri.

Yaani ukitaka kujua kuwa viongozi wamekosa vision, Ni pale walimleta Manzoki kwenye uchaguzi, mtu ambaye kuja kwake hakuna impact yoyote kwa mafanikio ya timu. Hajasajiliwa wala hagombei uongozi, sijui alikuwa wa nini!!
 
viongozi wajinga,walikataa kuwapa Vipers kumsajili Manzoki pesa ambazo wameenda kumpa Oatara na Akpan ambao mpaka sasa ni useless kwa timu.
pesa za kumleta mbrasil wangemuongeza Mgunda kuongeza chachu kwa Mgunda ambae kaifikisha timu group stage huku akipambana kupata kikosi cha kwanza.
 
Nakuunga mkono 100%
 
Uchawi una nafasi katika mpira duniani. Sio Tz au Africa pekee.

Porto wameajiri mganga huko na yuko kwenye payroll ya timu.
Ni baada ya Benfica misimu iliyopita kuajiri mganga halafu wakachukua ubingwa.

Porto wakasema usitutanie. Ulaya hiyo.
Kwahiyo Msimbazi Wameiga ULAYA??
 
Sio inawezekana huko kukosa nafasi nyingi za wazi kwa mchezaji ndio nguvu ya ushawishi toka nje inakuwa imefanya kazi yake?
 
Hili la kumleta Manzoki kwenye uchaguzi kweli lilikuwa tusi kwetu.

Lakini naona kama tabia ya viongozi kubadilisha makocha haraka tofauti na kuongeza wachezaji wazuri inachangiwa na upatikanaji kirahisi wa makocha husika, kuwapata huwa hakuna ushindani kama kugombania wachezaji wazuri na wapinzani wetu.
 
Wale mabosi wa Vipers nao kuna wakati niliwaona kama walitufanyia figisu makusudi kwasababu Manzoki alionesha kuitaka sana Simba Sc.
 
Mpira ni pesa sawa, lakini kuna mambo mengine licha ya uwekezaji yanahitaji bahati pia, kama kuchukua vikombe.
Bahati ni jambo linalotokea mara chache sana tuseme kwenye mara 100 linaweza kutokea mara 1.
Sasa sielewi unavyosema vikombe vinachukuliwa kwa bahati
 
Wale mabosi wa Vipers nao kuna wakati niliwaona kama walitufanyia figisu makusudi kwasababu Manzoki alionesha kuitaka sana Simba Sc.
Figusu kiaje? Yaani mshindwe wenyewe kufika price tag ya mchezaji halafu lawama muwape viongozi wa vipers? Yaani nyie washabiki wa Simba huwa mnachekesha sana, kwenye failure zenu lazima tu mutafute mtu wa kumlaumu [emoji119][emoji119]
 
wakati tunachangia humu tulisema sema haiko salama ,kuna makundi hayaridhiki ndio maana yakaja na ajenda ya kubadili katiba....sasa wala usiumize kichwa...kundi lile ambalo linalitaka kubadili katiba ,na yule jamaa kushindwa ,hao ndio mdili nao...ukitaka majina na vikao vinakofanyika ,tutawasaidia
 
Simba ni mbovu watu wasijifiche kwenye uchaguzi uliyokwisha pita, Kama Simba ingekuwa na quality players na wanapata matokeo huu upuuzi eti makundi ya uchaguzi ndio chanzo Wala usingekuwepo. Hawa waliochaguliwq na walioshindwa uchaguzi wapo hapo kama wanachama but hawana authority power yoyote yakuamua Mambo ndani ya Simba.
Anayepaswa kulaumiwa ni Mo Kama mwekezaji Kwanini hatoi pesa yakutosha kwaajili ya usajiri?, Inawezekanaje akatoq pesa ya kuweka kambi Dubai zaidi ya 500m+ alafu ashindwe kutoa 400m za usajili wa mchezajj mzuri?. Matokeo haya uhusiano na matokeo bali viwango duni vya wachezaji ndio kikwazo Cha matokeo.
 
Bahati ni jambo linalotokea mara chache sana tuseme kwenye mara 100 linaweza kutokea mara 1.
Sasa sielewi unavyosema vikombe vinachukuliwa kwa bahati
Mbona Guardiola hashindi vikombe kila anakopita licha ya ubora wa vikosi vyake? kama bahti ni kukosa mara moja kama ulivyoandika, basi angetakiwa awe anashinda kila wakati.
 
Figusu kiaje? Yaani mshindwe wenyewe kufika price tag ya mchezaji halafu lawama muwape viongozi wa vipers? Yaani nyie washabiki wa Simba huwa mnachekesha sana, kwenye failure zenu lazima tu mutafute mtu wa kumlaumu [emoji119][emoji119]
Lile suala la Manzoki lilikuwa na kona nyingi sana, mara mchezaji aseme mkataba wake umeisha, mara nyingine unakwisha December, huku viongozi wake wakidai bado unaendelea..

Hapo kuwalaumu viongozi wa Simba Sc pekee ni kuwaonea, Manzoki mwenyewe alionekana hajitambui, wala hajui nini kilikuwa kwenye mkataba wake, huku anadai mkataba wake ulipotea ukiwa saved kwenye simu!, ina maana hakuwa na hard copy?

Manzoki alikuwa mzinguaji tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…