Siku hizi kumekuwa na teuzi nyingi ambazo hazionyeshi, kuwa zimetokana na uwezo au weledi wa aliyeteuliwa. Chanzo kikuu kikiwa ni katiba inamruhusu mteuzi kufanya huo uteuzi, na matokeo yake tunaona kwamba mifumo ya utendaji na kauli za baadhi au wengi ya viongozi hao kuwa ni za magomvi na vitisho, badala ya kuwekeza katika mifumo ambayo itaendeleza.