Je tiba hii ni kweli?

kayanda01

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
1,216
Reaction score
1,062
Habari wanajamii. Wapendwa, naombeni kwa yeyote yule mwenye ufahamu na uhakika juu ya tiba zifuatazo atujuze na kutupa ukweli wa mambo, ni kuhusu kutibu/kuponya kabisa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume:

A) Unga wa mizizi ya bamia ilokomaa. Niliwahi kusikia kuwa unga wa mizizi ya bamia ukitumiwa kwenye chai/uji, huwa unatibu au kuponya kabisa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Je hii ni kweli na hakika? Please kama kuna yeyote ana uelewa au amewahi kutumia tiba hii, atujuze kwa faida ya wengi.

B) Dawa ya kiasili iitwayo PUTULU. Nilisikia kuna hii dawa ya kiasili inaitwa PUTULU (ya unga), ambayo ni dawa ya kisunni na hupatikana/huuzwa kwa wingi Zanzibar au misikitini. Nilisikia kuwa dawa hii inatibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Je ni kweli na hakika? kwa yeyote aliewahi kuitumia, please atujuze.

Nawasilisha, pia natanguliza shukrani za dhati kwa niaba ya wahanga wote wa tatizo hili (me inclusive).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…