Je tiba ya ugonjwa wa akili ina upungufu wa nguvu za kiume?

Je tiba ya ugonjwa wa akili ina upungufu wa nguvu za kiume?

omereyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2012
Posts
308
Reaction score
91
Nimekua natumia tiba kwa miaka sita, naendelea vizuri, naogopa kuacha lakini kadiri mda unavyopita nguvu za kiume zinaisha.

Nifanyeje jamani? Msaada tafadhali, nipo mkoani.
 
Wasiliana na waliokupa dawa ujue kama zina madhara au hilo ni tatizo linalojitegemea.
 
Kwa uelewa wangu mimi nguvu za kiume na maswala ya akili yanaendana sana, mfano vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa namna moja au nyingine zinaongeza akili, mfano samaki, karanga, ndizi, parachichi nk
 
Nimekua natumia tiba kwa miaka sita, naendelea vizuri, naogopa kuacha lakini kadiri mda unavyopita nguvu za kiume zinaisha.

Nifanyeje jamani? Msaada tafadhali, nipo mkoani.
Vyawezaendana. Manake kuna madawa yanasaidia watu ambao wapo hyperactive. Kama unayotumia ni ya jamii hiyo lazima nguvu zipunguwe!
 
Dawa za hospital ndo zilivyo,hyo ni side effect,kuna jamaa yangu alitumiaga quinine,masikio yakaziba na kitu hakikwenda mnara wiki nzima,kuanzia siku hyo alikataa kutumia dawa za hospital
 
Nimekua natumia tiba kwa miaka sita, naendelea vizuri, naogopa kuacha lakini kadiri mda unavyopita nguvu za kiume zinaisha.

Nifanyeje jamani? Msaada tafadhali, nipo mkoani.
Mkuu ni kweli kabisa hizo dawa hupunguza nguvu za kiume na hamu ya kufanya mapenzi kama ukizitumia mda mrefu!, hasahasa kama unatumia haloperidol , modicate... hizi kwa kitaalamu tunaziita (the conventional antpsychotics)

Kwa ushauri wangu;

kama hua unahudhuria clinic, ni vizuri ukamueleza daktari wako hili tatizo, kwasababu hii ni sababu nzuri ya wewe kubadilishiwa dawa na kupiwe dawa zingine ambazo ni nzuri zaidi na hazina hilo tatizo mfano olenzapine ambazo kwa kitaalamu hizi tunaita (the newer antpsychotics)

Hizi dawa mpya ni expensive kidogo ila naamini hutashindwa!...nikutakie kila la kheri na tafadhali usiache kunywa dawa!
 
Asante sana,Fidelis.kwa kuwa ninajali siwezi acha
 
Back
Top Bottom