Je, tishio la El-nino ni mbinu kututoa DP World!

Wabonho tujenge utamaduni wa kusoma au kutafuta habari, tunatia aibu sana, Swala la hizi mvua ziko hadi kwenye Website za FAO na walisha tahadharisha na sio Tanzania tu bali ni East Africa yote.

Tutafute habari
 


Who cares?
 
Kuwaamini hao TMA hakuna tofauti na kuamini waganga wa kienyeji.
 
MAONO NILIYOYAONA WAKATI NIKISIKIZA VIDEO U-TUBE UNYAKUO TV KUHUSU MAFURIKO YAJAYO MAY.

Nikiwa naendelea kusikiza video, uliopita kama USINGIZI hivi, ghafula nikaona,

Nilikuwa nyumbani, ndani ya nyumba, Hali ya hewa ikiwa tulivu kabisa jua likiwaka.

Cha kushangaza katika maono hayo, nilikuwa ndani ya nyumba, lakini nilikuwa na uwezo wa kuona Kila kitu kilichoendelea nje.

Niliona na kusikia upepo mkalia ukivuma Kwa Kasi Kutokea mashariki, nilidhani ni dalili ya mvua ya kawaida,

Kufumba na kufumbua, nami nikaona mbinguni juu ,duara jeusi lenye kuzunguka mithili ya sahani flat, palikuwa na maji yakizunguka Kwa Kasi katika duara Hilo, maji hayo hayakudondoka hata tone chini ardhini,

Wakati nikiendelea kutizama duara lile likizunguka, ndipo nikaona umetokea mfuniko uliokuwa umeziba maji Yale ,RANGI ya mfuniko ilikuwa bilauli ukifunguka na kumimina maji Yale ardhini tulipokuwepo na Kisha kujifunga.

Baada ya kuona tukio lile, nilihisi hatari inakuja, sasa kitendo Cha Mimi kutaka kuwambia wenzangu ndani ya nyumba kwamba tutoke na kuchukua zana za kutuepusha na hatari, ghafula nilijiona nikielea juu ya maji sikuona mtu mwingine yeyote, hapakuwa na nyumba Wala mti, au mlima ulioonekana. Vyote vilikuwa ndani ya maji.

Mwisho wa maono!!

Cc: 7seven

Tresor Mandala
 
Mtoa mada umewaonea sana TMA. Mimi ni mdau wa Climate Change. Taarifa hii TMA walianza kuliongelea mwezi wa Tano. Na kuongelea tena tarehe 4June wakisema wanaendelea kufuatilia Hali hiyo kufuatia mgandamizo wa hali ya upepo bahatini na wakaahidi kuelezea kwa kina Mwezi August. Tuwaache wafanye kazi yao kwa Sasa wana mitambo ya kisasa sana Jiwe aliwanunulia.
 
Mkuu

Hii itakua KWA Tanzania nzima au KWA dar tu!!?
 
Mkuu

Hii itakua KWA Tanzania nzima au KWA dar tu!!?
Bandari salama ndo inasoma hatari kubwa, ingawa matatizo hayo yatakuwa Mahali Mahali.

Mungu kutuonyesha haya, anataka tuombe, wote Kwa pamoja tukusanyike na kulia kuomba TOBA Ili atuepushe.

Watu na viongozi wanauona ujumbe lakini wanapuuza, wanausubiri yakitokea ndo wastuke,

Hapo bandari salama kama ikitokea inavyoonekana ktk Roho, mji hautakuwepo tena!!!
 
Wabonho tujenge utamaduni wa kusoma au kutafuta habari, tunatia aibu sana, Swala la hizi mvua ziko hadi kwenye Website za FAO na walisha tahadharisha na sio Tanzania tu bali ni East Africa yote.

Tutafute habari
Matapeli mlianza siku nyingi, na sasa ni muda wa kuumbuka tu.
Tlaatlaah
 
kwamba mafuriko yakuumbue kwa kiburi chako cha kutochukua tahadhari, right?
Matapeli mmeumbuka na mautabiri yenu ya kubumba. Huu uzi ni wa 2023 nao ulikuwa ni utabiri wa kitapeli kama huu. Mnatunga uongo wenyewe, na kuuamini wenyewe🤣
 
😂😂😂😂 nacheka kama mazuri!
 
Matapeli mmeumbuka na mautabiri yenu ya kubumba. Huu uzi ni wa 2023 nao ulikuwa ni utabiri wa kitapeli kama huu. Mnatunga uongo wenyewe, na kuuamini wenyewe🤣
kipindi cha Nuhu walikuwepo wenye kiburi zaidi yako gentleman,
so,
just relax tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…