Je, Transhumanism na post humanism itawahi kutia mguu Tanzania?

Okoth p'Bitek

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2019
Posts
1,124
Reaction score
1,384
Kwanza kabisa nianze kwa salamu
Ndugu watanzania mpaka hapa tulipofikia, tayari tunaishi na makundi matatu ndani ya nchi moja licha ya kudai kuwa sisi ni wamoja

Kundi la kwanza ni hawa jamaa wanaotumia lugha ya kiasili katika kuhifadhi silka za kupambania uhai, hapa mila na desturi za makabila ndio zinadumishwa

Kundi la pili ni hawa jamaa wanaotumia lugha ya imani na matumaini katika kuhifadhi silka za kupambania uhai, hapa tutakutana na wakristo na waislamu

Kundi la tatu ni hawa jamaa wanaotumia lugha ya kisasa katika kuhifadhi hizi silka, hili kundi bado halijapewa nafasi kwa kiwango kikubwa kwasababu, ya changamoto wanayokuja nayo ya kuua maadili yaliyowekwa na wafu waliopita,

Kundi la nne ambalo bado halijatia mguu ni hawa jamaa wasiotaka kufa, lengo lao kuu ni kuishi milele, kupata mwili ambao hautakuwa na limit ya kuutalii huu ulimwengu, hili kundi halihitaji chochote kuhusu mwili wa mnyama kwasababu wanadai kuwa huu mwili unazeeka na kuchoka lakini pia una vikwazo vingi,
Hili kundi lengo kuu na dhumuni ni kuhakikisha mwanadamu na teknolojia wanakuwa mwili mmoja, hili kundi pia halijali chochote kuhusu utambulisho, pia linachuki kubwa na uhalisia usiokuwa objective,

kidunia hili kundi tayari lina wafuasi wengi pia na makanisa yanayodai kuwa zawadi ya mungu kwa mwanadamu ni kuishi milele pia tayari wameshanunua eneo.

Swali langu ni je, kwa wale diaspora mlioleta maisha ya kisasa tanzania, mtakuwa tayari kuibeba hii falsafa huko ilipo na kuileta kwenye hii nchi yetu iliyojaa maziwa na asali, na nnawaomba kabla ya kuileta hakikisheni ya kuwa zile papara mlizokuwa nazo za kuleta maisha ya kisasa kabla ya kumuuwa mungu msirudie tena kwa maana majanga mliyoyaacha humu kwa wale walioyapokea maisha ya kisasa yanasikitisha
Leo hii wale waliochagua kuishi maisha ya kisasa ndani ya hii nchi ndio wanaongoza kwa kukashifiwa na hawa wajinga waliochagua kubaki nyuma, wengi wanaitwa mashoga, wapinga kristo, watoto wao mitaani wanaitwa broiler, au watoto mayai, wanawake wakidai haki zao wanaitwa feminist.
 
Kikubwa tuumalize mwendo salama.
Hayo ya kuishi bila kufa ni ndoto
 
hakuna ninacho kiamini kwenye hii dunia hatamimi sijiamini Kama nimimi kweli.!
 
Chai
 
Back
Top Bottom