Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 557
- 858
Tunajenga nyumba nzuri na za viwango vya juu lakini zinaungua moto, zinabomolewa na kuharibiwa vibaya sana ila hatuachi kujenga.
Magari yanapata ajali na kuteketea kwa moto ila hatuachi kununua, kuyapanda na kusafiri nayo.
Watu wanafiwa na watoto wao, wanazaa wengine wanakuwa walevi, majambazi, makahaba ila hatuachi kuzaa.
Watu wanaanzisha biashara kubwa na kufanikiwa sana ila baadaye zinafilisika kabisa, ila hatuachi kuanzisha biashara.
Watu wanasomesha watoto wao hadi wanafika ngazi za juu sana, anamaliza chuo na kuanza kazi, hana hata mwaka mmoja anafariki Dunia, na mwingine ana miaka 5 hana kazi ila hatuachi kusomesha na kusoma.
Watumishi wanabomolewa makanisa waliyojenga kwa gharama kubwa na kwa mateso mengi, ila hatuachi kujenga kwa kisingizio cha wengine walipatwa na majanga.
Watu wanaoa na kuolewa, wanapatwa na shida mbaya kwenye maisha yao ya ndoa, mke au mume anamuua mwenzi wake, mke au mume anamwacha mwenzi wake, mke au mume anakosa uaminifu wa ndoa yake. Pamoja na hayo Dunia haijawahi kusimama kuacha kutokea ndoa nzuri, bado ndoa zinaendelea kufungwa kila siku.
Tusijaze fikra hasi kwa mtu mmoja kutokewa na jambo tunalotaka kuliendea katika maisha yetu, tuwe na ufahamu mzuri katika hilo.
Mabaya yapo mengi sana ila tusitumie mabaya kuwa na mtazamo mbaya kwa watu au makundi fulani au mambo fulani.
Acha kusema sitasoma kwa sababu hakuna ajira, acha kusema sitajenga kwa sababu fulani nyumba yake iliungua moto.
Acha kusema sitapenda au sitaoa/kuolewa kwa sababu ndugu yako alipatwa na shida kwenye ndoa yake.
Bila kujalisha kilimtokea nini mwingine bado dunia inao uzuri wake wa kufanya jambo hilo hilo likawa halina ubaya wowote na likawa juu na Bora sana.
Muhimu kukua na kuacha kusambaza upotofu, acha kutoa maarifa mabaya kuhusu jambo fulani, bali tuwaelimishe watu kwa misingi ya neno la Mungu.
Soma neno ukue kiroho
Iwe jua iwe mvua soma biblia
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081