Je, Tuchel ataendeleza ubabe Darajani?

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105


Chelsea itakuwa mwenyeji wa Newcastle katika moja ya mechi mbili zilizopangwa kuchezwa leo Jumatatu usiku.

Itakuwa mechi ya sita ya Thomas Tuchel.

Tangu kuchukua nafasi ya Frank Lampard kama kocha mkuu wa Chelsea mwezi uliopita, Mjerumani huyo, ambaye anaweza kuona timu yake ikipanda katika nne bora ikiwa wataifunga Newcastle United huko Stamford Bridge leo usiku, ameinoa Chelsea kwenye michezo mitano katika mashindano yote, akishinda nne na sare moja .

Baada y sare ya bila bao na Wolverhampton Wanderers huko Stamford Bridge katika mchezo wake wa kwanza, Tuchel ameiongoza Blues kwa ushindi mara nne mfululizo, kuwashinda Burnley (2-0), Tottenham Hotspur (1-0), Sheffield United (2-1) na hivi karibuni Barnsley (1-0).

Mchezo mwingine utakao pigwa hii leo ni kati ya West Ham ambaye atakuwa nyumbani kumkaribisha Sheffield United.
 
Newcastle huwa ni ving’ang’anizi na wanastick kwa game plan yao mwanzo mwisho.

Ila kwa kuwaTuchel ni tactician mzuri na mzee wa kusoma mchezo na kubadili gear angani (tofauti na Lampard ambae alikuwa clueless bila plans B, C, D), hii game Chelsea wanashinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…