Je, Tumeikosa Huruma Yetu ya Kibinadamu?

Tuone huruma jamani πŸ˜ƒ πŸ˜€ πŸ˜„ 😁

Your browser is not able to display this video.
 
Tunafikia huku kwa mengi kama jamii, inatupasa tukumbuke pia kuwa jamii ni sawa na kioo mbele ya kiongozi yoyote duniani.

Hebrews 13:17

Pole Mjomba
 
Nimepata mtihani mkubwa katika suala hili.

Kwa sababu kanuni zangu mbili zinazoniongoza zimegongana.

Kanuni hizi ni upande mmoja, kuwa na empathy kwa watu walio na matatizo. Kwa kanuni hii, napenda kumpa pole nyingi Mrisho Mpoto. Kwa ubinadamu tu, bila kujali siasa.

Lakini, kanuni yangu nyingine ni kuacha watu wafanye mambo kwa uhuru na kujieleza watakavyo. Kwa kanuni hii siwezi kuwasema wanaombeza Mrisho Mpoto katika wakati huu, kwa kusema "Kifo ni Kifo tu", wakitumia kauli ya rais Samia na kumnasibisha Mrisho na Samia.

Kwa ukweli, ningependa sana kuona Tanzania tunafanya siasa za kukosoana kisera, kifalsafa, kisiasa, na huko kwenye mambo social kama misiba na harusi tunaungana vizuri tu.

Lakini pia, nafahamu kwamba ni vigumu kuwaambia watu waliokandamizwa sana, waliotekwa sana, walioumizwa sana, wafanye civilized politics.

Hitimisho langu nimeona haya ni matokeo ya watawala kushindwa kufanya kazi ya kuwaunganisha wananchi. This is a case of the chickens coming home to roost. What goes around, comes around, what is good for the goose, is good for the gander.

Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Ila pia, kuna haja ya watu wanaotaka mabadiliko kuji organize kama wanataka kususia mambo, wasusie mambo ya kiuchumi kwa wote wanaowaona hawasimami kwenye haki.

Wafanye boycott kwenye mambo ya uchumi, wasusie kununua bidhaa za wafanyabiashara walio enablers wa wanasiasa wasiosimamia haki.

Hiyo boycott ikiwezekana inaweza kuwa na maana zaidi ya hii ya kuchambana mitandaoni na Mrisho Mpoto ambaye ni mtu mdogo sana na hana impact hivyo katika nchi ya Tanzania.
 
Tunafikia huku kwa mengi kama jamii, inatupasa tukumbuke pia kuwa jamii ni sawa na kioo mbele ya kiongozi yoyote duniani.

Hebrews 13:17

Pole Mjomba
Watanzania wanatumia fursa hii kumpika vilivyo mjomba! Kwa hizi comment kama una pressure lazma udondoke
 
Mkuu kwamba tuanzishe Sensa ya kujua vitega uchumi vya machawa wote nchi mzima?🀣🀣🀣🀣(Nisameheme kwa kicheko,kimekuja tu wala sijakiita)
 
Watanzania wanatumia fursa hii kumpika vilivyo mjomba! Kwa hizi comment kama una pressure lazma udondoke
Naamini wakati anachukua "bahasha" alijiapia moyoni "liwalo na liwe",hapo pressure inatoka wapi wakati alikuwa ameshajiandaa kisaikolojia?
 
Sijasoma bandiko lote, ila tujiulize aliyetufikisha hapa ni nani?
 
Mkuu kwamba tuanzishe Sensa ya kujua vitega uchumi vya machawa wote nchi mzima?🀣🀣🀣🀣(Nisameheme kwa kicheko,kimekuja tu wala sijakiita)
Mnaanza na Big Papas wanaomiliki uchumi na kufadhili mfumo kandamizi, hawa machawa wengine ni "kujichumia dhambi" tu.

Watanzania ukiwaambia kumtukana Mrisho Mpoto watajaa.

Lakini ukiwaambia kususia biashara za Mo Dewji, Rostam Aziz, Bakhressa na Abood, huwaoni.

Vipaumbele.
 
Msiba una maana ukiwa kwako kwa wenzio Hauna maana?
 
shida alikuwa hayupo na wananchi ndio faida yake hii.Sasa ajifunze kurudi na wimbo wa shangazi maana wa mjomba tulimuona wa maana sana.
Hiki kitu nasema kila siku. Kuna wasanii walifika walipo kutokana na uhuru wa habari na uhuru wa siasa. Mpoto alikuwa mkosoaji "kiaina" wa mkwere. Masanja alikuwa anamwigiza Pinda, Kuna Lowassa na komba Hawa walikuwa wakiigizwq na mpoki na wakuvwanga.

Leo hii ukikosoa Serikali wanakushambulia eti huna adabu...wanasahau wao pia kama mazingira yangekuwa haya ya Leo basi wasingetoka.

Unafiki
 
Kwa nini aliposti amefiwa??
 
Shikamoo Watanzania πŸ˜ƒ kwenye kupika mnaongoza Afrika
 
Usianzishe ugomvi wa mawe ungali unaishi nyumba ya vioo....
 
Wenye macho ya mwili huona mwisho.
wenye macho ya ndani huona mabadiliko.
Kifo si kilio ni mlango wa tafakari.
Si mwisho ni hatua ya mzunguko.
- Mrisho Mpoto.

Nampa pole bila kuwalaumu wanaoliona tukio hili kwa jicho la tofauti wala kuwaletea jazba za kimazoea.

Hasha, hazifiki!!
Ibn Unuq
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…