Je, Tumejiandaa na 'Uvamizi wa WaChina?'

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,246
Ndugu zangu,

Jeshi la Wachina linakuja, wako wengi. Kwenye moja ya picha za magazetini hii leo, inamwonyesha Rais wetu akiwa amezungukwa na Wachina.

Rais amevalia ' Kijamaa', lakini Wachina wamevalia ' Kibepari'.

Naam, China ni taifa kubwa kiuchumi. Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa, ni uchumi wa Kibepari.

Na idadi ya Wachina nayo ni kubwa.
Ili kuweza kushindana kibiashara, China kwa sasa inahitaji mali ghafi nyingi kwa viwanda vyake. China inahitaji nishati pia; mafuta na gesi.

Wachina wameigeukia Afrika. Wachina leo, kwa kutumia mahusiano mazuri na ya kirafiki ya kihistoria, ya tangu ya enzi za Vita Baridi vya Dunia, wanajipenyeza kila kwenye uwezekano wa kuvuna mali ghafi ikiwamo mafuta na gesi.

Nao wanakuja na ahadi za misaada ikiwamo kutujengea WaAfrika barabara, viwanja vya michezo vya kisasa na hata kumbi za Kimataifa za mikutano.

Duniani hakuna cha bure. WaChina wanavuna zaidi ya wanachotupa.

Tujiulize; tunataka nini? Tuangalie pia, masharti ya misaada ya Wachina. Tuangalie vile vile mazingira ya ajira wanazokuja nazo Wachina katika kuwekeza kwao hapa kwetu.

Ilivyo sasa, inatokea wawekezaji wa Kichina wanakuja nchini wakiwa na wafanyakazi wao, na wakati mwingine, hata vibarua wa kubeba zege wanatoka UChina. Hali hii haisaidii kutatua tatizo la ajira kwa vijana wetu.

Na hata inapotokea Wachina wakatoa ajira, basi, mazingira ya ajira huwa magumu kwa vijana wetu. Ujira ni mdogo na masharti ya kazi kwa vijana wetu huwa magumu sana.

Tujiulize pia, uwekezaji wa Wachina unatoa fursa kwa Watanzania kupata maarifa ya kiufundi na kiutawala kwenye sekta ambazo Wachina hao wanawekeza hapa nchini?

Hofu yetu, kama nchi, ni kuendelea kuwa tegemezi, hivyo masikini, huku nchi yetu ikiwa na rasilimali nyingi.

Na tujiahadhari, na ‘Uvamizi wa Wachina.' Yumkinini umetukuta tukiwa hatujajiandaa, kama taifa.
 
Hiyo inaitwa 'Ukoloni mamboleo" na usomi wa maarifa wa wachina wakati sisi tunaendelea na usomi wa vyeti na idadi ya vidato
 
ndio utekelezaji wa makubaliano yake na wachina kuhusu yale madawa ya kulevya aliyokamatwa nayo rizwani au???
 
tunazo rasilimali na zimeshindwa kutuletea maendeleo. Wasipokuja wachina, MTAWEZA KUFANYA CHOCHOTE WENYEWE chini ya hii serikali iliyojaa wezi?????

ADUI NI MAFISADI WA CCM SI WACHINA
 
excellent writing maggid. mamajack umeona hao wachina na vtu vyao baada ya ile habar ya riz na unga kwenye mitandao? tumekuwa tukishambuliwa na wachina kabla ya ile habari. kutatua tatizo la wachina tunahitaji uongoz makini na unaojali.
 
Mkuu Maggid,
kwa maoni yangu, Wachina ni moja ya mataifa wanaaongoza kwa wema duniani, wao ni kazi tuu, hawataki longolongo wala usumbufu wowote usio wa lazima!. Nakumbuka Tianaman Squire, wanafunzi waliambiwa msiandamane, wao wakaandamana!. Kule hakuna kubembelezana!, serikali ikapiga level uwanja huo regardless wangapi waliperish!.

Hata ukikutwa na mzigo au rushwa!, wao hawataki kukusumbua na makesi makesi marefu, ni kumaliza tuu kazi na kuendelea!.

Kati ya wakopeshaji wote duniani, hakuna generous kama China, hebu fikiria anakukopesha dola bilioni 1.2 kwa interest ya 01% tuu kwa mwaka!. Tena anakupatia grace period ya 20 years na kulipa deni ndani ya mika 80!. Nani atakupa mkipo wa miaka 100?!.

Kitu kizuri kuhusu Wachina, hawataki tuteseke, hivyo wanaleta mafundi wao wa kufanya kila kitu mpaka kuziba kubeba zege, na haina haja ya kuwafundisha Watanxzania kwa sababu wataendelea kutuleta mafundi wao kwa miaka yote 100 ya mkopo!. Tena mafundi wao hawalali hotelini kama wazungu, wao wanalala site kwenye yale makontena na hata zile huduma za "kijamii" hawaendi kununua Jolly, wao wanaomba kusaidiwa na waliozunguka jirani na mradi!.

Sisi hatuhitaji maandalizi yoyote ya kuwapokea, kwa sasa ndio the best and cheapest contactors wa ujenzi, ndio best na cheapest panel beating garages, kule Kariakoo ndio wanaongoza kwa maduka na wanaishi hadi Mbagala, wanauza hadi karanga na ashkrimu!. Wachina ndio wanao ingoza kwa kufanya "massage" na wanazifanyia hoteli kubwa kubwa, na ukihitaji zile huduma za ziada, unaongeza hela kidogo tuu kuliko hata zile ambazo ungelipia kama ungeenda kununua pale Jolly Club!.

Tanzania tusiwe na wasiwasi kabisa, with Chinese hands, we are very safe!.

P.
 
Good Morning Kaka Pasco,

Najua umechochea mjadala, maana, Pasco nimjuaye anafahamu uhalisia wa tishio la ' Uvamizi wa Wachina'.
 
Last edited by a moderator:
tunazo rasilimali na zimeshindwa kutuletea maendeleo. Wasipokuja wachina, MTAWEZA KUFANYA CHOCHOTE WENYEWE chini ya hii serikali iliyojaa wezi?????

ADUI NI MAFISADI WA CCM SI WACHINA

Mkuu watu wanao walahumu Wachina sijuhi wana agenda gani ya siri, kwani nchi za magharibi tangu tupate uhuru wametuendeleza kivipi? Hivi kweli tuna kitu chochote cha maendeleo cha kujivunia kutokana na ushirikiano wetu na nchi za magharibu miaka nenda rudi - hatuna.

Watu wanacho sahau ni kwamba ma CEO wa kichina wanao simamia makampuni ya Serikali ya Kichina wanalipwa mshahara mdogo sana, yaani ukilinganisha mshahara wa mkurugenzi wa Shirika la umma Tanzania na Uchina utashangaa, Watanzania wanalipwa zaidi ya mara kumi kuliko Wachina! Ndio maana Wachina wakija hapa alafu wafanyakazi wakawadai mishahara minono hilo Wachina huwa linawashangaza sana.

Kwa nini tuanze kuwazulia watu wenye ujuzi wa kutukwamua kwenye mambo mengi tu, mifano tunaiona nchini mwao cha mahimu ni Serikali yetu kijipanga kwa kushirikiana nao kweye nyanja nyeti za kutuletea maendeleo ya haraka haraka kama walivyo fanya kwao - wenzetu Kenya hili wameliweza sana na wako beneti na Wachina - wanawajengea mabarabara ya kisasa, viwanda vya kuhunda magari, CCTV Nairobi, Viwanda vya kuhunda TV na simu, Ujenzi wa kijiji cha kisasa cha Sayansi na tekinolojia kitahusu zaidi mambo ya ICT wezetu Wa Kenya wanapaa sisi tunabaki kuwabeza beza Wachina, kwa bahati mbaya na wao wamekwisha tujulia ndio mana mambo ya maana wanapeleka Kenya, ukiongezea vurugu za GESI ya Mtwara sijuhi watakuwa wanatufikilia nini, Serikali itapaswa kufanya kibarua cha ziada kurudisha imani nao!!

Tusipo acha hizi kampeini za chini chini za kuwaona Wachina ni WEZI, basi sisi kama Taifa tutakosa mengi - Je hilo ndilo tunalotaka. Kwa nini tunaingia katika mtego wa propaganda za nchi za magharibi zenye mlengo wa kuwapiga vita vya kiuchumi Wachina barani Africa, Chunga sana Halliburton wapo nchini ingawa uwaoni au hawavumi lakini kumbuka wana mbinu nyingi.
 
Niliona magazetini wachina wanasomesha watanzania wengi fanimbalimbali kila mwaka bure.is it bad?
Nimeshuhudia wachina wakiwawezesha watanzania kuvaa kwa gharama nafuu.walaumiwe?
Makandarasi wa kichina wanafanya ujenzi wa barabara na majengo kwa gharama nafuu sana. nidhambi?
Nimeona karne hii wachina wakiwakomboa zaidi waafrika kimiundo mbinu(infrustructure) kuliko hao wamarekani ambao hutuletea tuu net za mbuu wakijua kwamba kuna mmarekani anahisa pale AR.
Wachina hawajawahi kupora rasilimali za Africa kama wazungu (its mutual benefit btw countries)
Wachina wametuwezesha kupata bidhaa nyingi mno kulingana na uwezo wa wananchi.niubaya huo?
wachina walitujengea TAZARA tukaiua wenyewe, leo hii wamerudi tena kuikarabati.bado ni ubaya huo?
Serikali ya china ni nchi pekee inayoongoza kuimwagia tanzaia mabilioni ya hela (grants) kuliko hiyo US.
TZ imekalia madini,gesi,makaya mawe,mafuta for 50years baada ya uhuru bila kujipatia maendeleo yenyewe, Je ni mchina alitukwaza au mzungu?
 
Juzi lara alipost thread hapa ya wachina kunyang'anywa mamilioni pale mwenge. huenda ndo kampeni zimeanza nini za kuwafukuza.
ila tatizo la hawa jamaa wao wanafanya kila kitu kwa kutumia watu wao hata tukiwapa barabara kujenga kila kitu mpaka sementi, mainginia ma tekinishia nk wanatoa kutoka kwao. they are dangerous too.
 
Wachina hawadhibitiki duniani,wana jeuri na kiburi na wala hizo mnazoita haki za binadamu kwao si kitu muhimu iwapo hazina maslahi kwao.Jambo la kushukuru Mungu ni kuwa,bado wanaongozwa na misingi ya maadili ya uadilifu.Ole wetu siku watakapoanza kuwa na roho kama za viongozi wetu!Mtajuta!maana hawasikiagi cha UN wala wala watetezi wa haki za binadam!Mtanyongwa hapahapa na hakuna atakayekoroma na mali zenu zitakwenda tuu!Kwani mtawafanya nini?mna ubavu?
 
kweli kabisa ase mi nawaona hawa jamaa ndo msaada mkubwa sana kwetu despite mambo madogo madogo yanorekebishika, hizi zitakuwa western propaganda wabongo tusizitilie maanani sana.

SUPPORT CHINESE, WITH CAUTION OFCOz.
 
Ndugu zangu,

Jeshi la Wachina linakuja, wako wengi. Kwenye moja ya picha za magazetini hii leo, inamwonyesha Rais wetu akiwa amezungukwa na Wachina.

Rais amevalia ' Kijamaa', lakini Wachina wamevalia ' Kibepari'.

Naam, China ni taifa kubwa kiuchumi. Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa, ni uchumi wa Kibepari.

Na idadi ya Wachina nayo ni kubwa.
Ili kuweza kushindana kibiashara, China kwa sasa inahitaji mali ghafi nyingi kwa viwanda vyake. China inahitaji nishati pia; mafuta na gesi.

Wachina wameigeukia Afrika. Wachina leo, kwa kutumia mahusiano mazuri na ya kirafiki ya kihistoria, ya tangu ya enzi za Vita Baridi vya Dunia, wanajipenyeza kila kwenye uwezekano wa kuvuna mali ghafi ikiwamo mafuta na gesi.

Nao wanakuja na ahadi za misaada ikiwamo kutujengea WaAfrika barabara, viwanja vya michezo vya kisasa na hata kumbi za Kimataifa za mikutano.

Duniani hakuna cha bure. WaChina wanavuna zaidi ya wanachotupa.

Tujiulize; tunataka nini? Tuangalie pia, masharti ya misaada ya Wachina. Tuangalie vile vile mazingira ya ajira wanazokuja nazo Wachina katika kuwekeza kwao hapa kwetu.

Ilivyo sasa, inatokea wawekezaji wa Kichina wanakuja nchini wakiwa na wafanyakazi wao, na wakati mwingine, hata vibarua wa kubeba zege wanatoka UChina. Hali hii haisaidii kutatua tatizo la ajira kwa vijana wetu.

Na hata inapotokea Wachina wakatoa ajira, basi, mazingira ya ajira huwa magumu kwa vijana wetu. Ujira ni mdogo na masharti ya kazi kwa vijana wetu huwa magumu sana.

Tujiulize pia, uwekezaji wa Wachina unatoa fursa kwa Watanzania kupata maarifa ya kiufundi na kiutawala kwenye sekta ambazo Wachina hao wanawekeza hapa nchini?

Hofu yetu, kama nchi, ni kuendelea kuwa tegemezi, hivyo masikini, huku nchi yetu ikiwa na rasilimali nyingi.

Na tujiahadhari, na ‘Uvamizi wa Wachina.' Yumkinini umetukuta tukiwa hatujajiandaa, kama taifa.
wanakaribishwa kwa mikono miwili ITS OVA NOW
 
Aisee hivi ni kweli Watz tumelogwa?kuna comment nikisoma hapo juu i feel dizzy?kweli?!yawezekana kweli moyo wa nchi upo Bagamoyo.
 
kweli kabisa ase mi nawaona hawa jamaa ndo msaada mkubwa sana kwetu despite mambo madogo madogo yanorekebishika, hizi zitakuwa western propaganda wabongo tusizitilie maanani sana.

SUPPORT CHINESE, WITH CAUTION OFCOz.

Naam kiongozi wangu. NI heri mchina anachukua tanzanite ya $10 mil. alafu anakujengea barabara na shule ya $5 mil. Kuliko USA au Uk wanaochukua $10 mil and then wanawapa Serikali $5 mil.kuondoa umasikini. Kie kie kie

Sent via EyePhone
 
sisi wenyewe ndo wezi tusiwasingizie wachina..kwani wanatulazimisha?
 
Back
Top Bottom