Je, tunahitaji divine intervention and miracles kusuluhisha matatizo ya kibinadamu?

Je, tunahitaji divine intervention and miracles kusuluhisha matatizo ya kibinadamu?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Amani iwe nanyi wana JF

Tukiwa katika kipindi cha kwaresma kwa sisi wakristo na ramadhani kwa wenzentu waislamu. Ni vyema kukita tafakari zetu kwenye mambo yenye upako.

Hakika mwenye-enzi Mngu ni mwema siku zote, yeye ndiye autujaliae uhai na afya njema kwa wale awapendao na pia anayejua hatma zetu. Aidha, yeye ndiye mwenye kugawa riziki kubwa na ndogo kwa wale awapendao.

Kimsingi, Mungu anajua yale tunayostahili na kila mtu amepewa kile anachostahili. Sisi wakristu tunasema kazi ya Mungu haina makosa. Na hata tukipoteza wapendwa wetu tunasema, bwana ametoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.

Lakini maisha yetu wanadamu yamejaa changamoto nyingi, nyingine za kujitakia na nyingine za kiasili. Utatuzi wa changamoto hizi, wakati mwingine, huwa ni mgumu au beyond ordinary human capacity (earthquakes, pandemics kama Covid 19, cancer, etc )

Je katika kutatua matatizo yetu wanadamu tunahitaji divine intervention and miracles au we need to stretch our brains a little bit more than before?

Tangu kuanza kwa ulimwengu, wanadamu wametumia akili kusuluhisha matatizo yao japo vitabu vya dini vina visa ambavyo Mungu aliingilia, ila sehemu kubwa imefanywa na wanadamu wenyewe

Sasa ni ipi nafasi ya wachungaji, maaskofu, mitume na manabii ambao wanatuambia wana weza kusuluhisha matatizo yetu kwa kutumia maji, mafuta, vitambaa, kufokafoka na pengine sala na dua.?

Je divine intervention and miracles are reliable methods of solving human problems? Tuendelee kumuomba Mungu atujlie hekima na busara ya kutafuta namna bora ya kusuluhisha matatizo yetu.
 
Mchungaji anamuombea mwenye malaria katika kanisa linalopakana na duka la madawa, halafu baada ya maombezi, muumini anatoa sadaka ya elfu 10,000, fedha nyingi kuliko gharama za dawa ya malaria.

Kuombea mvua katika eneo ambalo liko kilometa moja kutoka ziwani au mtoni, au maji yako ardhini, mita zisizozidi 50
 
Mwisho kabisa, je Mungu anahitaji tip, sadaka au any consideration ili atusaidie?
 
Mchungaji anamuombea mwenye malaria katika kanisa linalopakana na duka la madawa, halafu baada ya maombezi, muumini anatoa sadaka ya elfu 10,000, fedha nyingi kuliko gharama za dawa ya malaria.

Kuombea mvua katika eneo ambalo liko kilometa moja kutoka ziwani au mtoni, au maji yako ardhini, mita zisizozidi 50
mtu anatuambia tufunge kwaresma kitu ambacho hakiwi supported na msahafu wetu wakristo, ni utapeli pia
tena kufunga kwenyewe unaajiamulia tu ufunge vipi.
mambo ni mengi unafiki ni mwingi
watu wana malengo yao, sisi tunawafuata tu
 
Hakuna "mtu" aliyekuambia au kukulazimisha kufunga.Ni maamuzi/agizo la kijumuiya (mapokeo)inayohusu hilo.Upotoshaji mwingine muwe mnabaki nao mioyoni tu.
 
Hili la kufunga lina maelekezo maalumu , ni repentance

Yoel 2:12-17
Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.

Swala ni utatuzi wa matatizo yetu
 
Kwa kweli tunahitaji Mungu aingilie kati ili kutatua matatizo yetu na yuko karibu kuingilia kati.

Yesu alitupa ishara
Luka 21:10,11:" Taifa litapigana na taifa na ufalme kupigana na ufalme. Kutakuwa na MATETEMEKO MAKUBWA YA ARDHI, NA MAGONJWA NA UPUNGUFU WA CHAKULA KATIKA SEHEMU MBALIMBALI, pia kutakuwa na mambo yenye kuogopesha na ishara kubwa kutoka mbinguni".

Mstari wa 31 sura hyohyo akamalizia kwa kusema:"Vivyo hvyo, ninyi pia mtakapoona mambo hayo yakitukia, jueni kwamba UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA".

Suluhisho pekee kwa matatizo yetu wanadamu ni UFALME WA MUNGU.

Ufalme huo utatufanyia nini wanadamu?

1. KIFO kitaondolewa(isaya 25:8)
2.NJAA itakomeshwa(zaburi 72:6)
3.MAGONJWA yatakomeshwa.(isaya 33:24)
4.TUTAPATA KAZI zenye kuridhisha(ABSORBING WORK)(Isaya 65:23)
5.Wapendwa wetu waliokufa watafufuliwa.(yohana 5:28,29)

Na ahadi nyngne nyingi..

Ili tunufaike tunahitaji kupata ujuzi wa kweli kumuhusu Mungu.(Yohana 17:23.)
 
Mataifa masikini yameamua "kufungulia" makanisa, hasa ya kikristo, yanayojiita ya uponyaji, ili ku "coverup" mapungufu ya huduma za kijamii, kiafya na kiuchumi.

Mtu anaombewa ili apone magonjwa, tatizo hili lingetatuliwa kwa kuwa na huduma bora za afya, wa maleria, moyo,Figo, na Kila aina ya ugonjwa utibiwe kitaalamu.

Matatizo ya kiuchumi, Sasa wachungaji wamekuwa wanahubiri utajiri, maana yake mifumo yetu ya kiuchumi Ina matatizo, kwa nini mtu aamini utajiri wa miujiza ya kanisani?
Hapa ndipo wasomi wangeingia kati, na Serikali, kusaidia jamii.

Mifumo ya kisiasa isiyokidhi, inafanya watu waone kwamba hawana pa kukimbilia
 
Hakuna "mtu" aliyekuambia au kukulazimisha kufunga.Ni maamuzi/agizo la kijumuiya (mapokeo)inayohusu hilo.Upotoshaji mwingine muwe mnabaki nao mioyoni tu.
Acha hasira mkuu
Unafuata mapokeo yaliyokemewa, AU HAYO YENU NI TOFAUTI

Wakolosai 2:8​

8 Angalieni mtu ye yote asiwateke kwa falsafa duni na potofu ambazo hutegemea mapokeo ya kibinadamu na mafundisho ya kidunia, na wala si Kristo mwenyewe.
 
Mataifa masikini yameamua "kufungulia" makanisa, hasa ya kikristo, yanayojiita ya uponyaji, ili ku "coverup" mapungufu ya huduma za kijamii, kiafya na kiuchumi.

Mtu anaombewa ili apone magonjwa, tatizo hili lingetatuliwa kwa kuwa na huduma bora za afya, wa maleria, moyo,Figo, na Kila aina ya ugonjwa utibiwe kitaalamu.

Matatizo ya kiuchumi, Sasa wachungaji wamekuwa wanahubiri utajiri, maana yake mifumo yetu ya kiuchumi Ina matatizo, kwa nini mtu aamini utajiri wa miujiza ya kanisani?
Hapa ndipo wasomi wangeingia kati, na Serikali, kusaidia jamii.

Mifumo ya kisiasa isiyokidhi, inafanya watu waone kwamba hawana pa kukimbilia
Hakika,

Udhaifu katika uongozi, maendeleo kidogo kwenye uchumi na sayansi na teknolojia, umasikini, uvivu, roho mbaya na chuki vyote hivi vinamtinga mtu mweusi, mtanazania wa kawaida.

Je kukesha kwa gwajima, kakobe au yule mwamposa kuna weza kutatua haya?
 
Back
Top Bottom