Je, tunajifunza historia ya nchi kwa manufaa?

Je, tunajifunza historia ya nchi kwa manufaa?

Librarian 105

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
356
Habari zenu wanajamii?!

Wataalamu na walimu wa historia duniani kote wanaeleza fani ya historia inamsaidia binadamu kujua alipotoka, alipo na anapoelekea. Nikitafakari hili, nawaza historia ya nchi yetu tumeitumia vipi kutuletea manufaa? Tangu babu zetu kina Mkwawa na bibi zetu wapambane na kukataa utumwa na ukoloni kulinda himaya yetu ya Tanganyika.

Kisha baba wa taifa na kina bibi Titi na mapambano ya kudai uhuru..., kote huko tunasoma mashuleni hadi vyuoni lakini sijapata kuona tija ya manufaa katika kuboresha hali za maisha yetu au mapambano ya kupiga vita unyonyaji utokanao na mifumo yote ya ukoloni.

Nafikiri tatizo lipo katika mitaala ya elimu, huenda inatujenga Watanzania kuwa elimu ni kwa ajili ya kujibia mitihani. Wakati umefika sasa wa kudai mitaala ya elimu kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya vyuo kumwandaa Mtanzania kuijua historia yake (mazingira ya mapitio ya nchi yake) na njia mujarabu za kukabiliana nayo ili kuboresha njia za maisha yake na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Shukrani wanajamii.
 
Kuitekeleza Io elimu ni ngumu maana mfumo wa uendeshaji elimu unategemea ufadhili na wafadhili Hawataki elimu ya kumkomboa mwenyeji Bali kumuandaa kuwa tegemezi na kibaraka
 
Kuitekeleza Io elimu ni ngumu maana mfumo wa uendeshaji elimu unategemea ufadhili na wafadhili Hawataki elimu ya kumkomboa mwenyeji Bali kumuandaa kuwa tegemezi na kibaraka
ndio inatakiwa tuanze kujikomboa apo kwenye kutafuta maarifa
 
Back
Top Bottom