Je, Tunao Ufahamu?

Je, Tunao Ufahamu?

hisown

Member
Joined
Jul 30, 2017
Posts
20
Reaction score
33
Wanabodi, nawasalimu; moja kwa moja niende kwenye mada.

Bila shaka ni ni suala pana ambalo ndani yake kuna taaluma mbalimbali. Kwa jinsi yake na namna yake ni mwelekeo unaolenga ustawi wa mtu kiroho na kimwili ukizungukwa na taaluma mbalimbali.
Namna mambo yanavyofanyika na kuonekana katika macho na uzoefu wa watu yanaacha ufahamu wetu binadamu ukistaajabu!
Jinsi yake na namna yanavyotokea katika maisha yetu ya kila siku tangu kale, mambo haya yameathiri na yanaathili ustawi wa mtu kiroho na kimwili.
Jambo la kusikitisha, jamii kwa sababu ya mwelekeo wake iliyochukuwa haioni ni tatizo! Visa vingi ambavyo vinatokea katika familia na jamii vimeondoa ufahamu wa asili wa binadamu na kujenga ufahamu mpya.
Katika kujifunza na kufuatilia taratibu na maisha yenyewe ya mwanadamu nimegundua kwamba, kwa kiasi kikubwa binadamu amepoteza ufahamu wake.
Maisha kama uzoefu msingi wake upo katika roho na mwili. Roho na mwili vyote hujikamilisha. Ukamilifu wa kila kimoja (Roho na mwili) huitaji kingine.
Kwahiyo, ufahamu wa mtu licha ya kuwa upo katika taaluma mbalimbali, lakini lengo kuu na la jumla lipo katika ustawi wa roho na mwili, huo ndiyo msingi na mwelekeo wake mkuu. Inapokuwa kinyume chake hapo ufahamu wa mtu unakuwa na madhara.
Tangu kale mpaka leo, kwa sababu familia na jamii haina tena ufahamu, tumekuwa watu wa matatizo makubwa na yanayoacha madhara makubwa sana kwetu sisi na hadi vizazi.
Kwenye familia, koo au jamii zetu kuna matatizo makubwa ya magonjwa ya ajabu, vifo vya ajabu, mateso na uchungu katika ndoa, mafarakano katika familia, kudhoofika kiuchumi, kutoa mimba, madawa ya kulevya, ndoa za jinsia moja, ushoga, usaganaji na kujichua kwa wanaume, ufisadi na wizi, mauaji, kuhisi mgandamizo, woga, uliopita kiasi, n.k.
Nimezungumza ufahamu kwa sababu matatizo yote haya tulionayo leo ni kwasababu ya kutokuwa na ufahamu. Kwasababu familia/ukoo au jamii iliyokosa ufahamu haiwezi kujua matatizo yake yanatokana na nini na hivyo hudhani kuwa hayo yanayoikumba ni ya kawaida kwa sababu imefumbwa.
Kama ilivyo sayansi (Bailojia) kwamba mtu hurithi chembechembe za mwili (DNA) zinazofanana kutoka kwa baba na mama. Hivyo, mtu pia hurithi tabia mbaya au nzuri kutoka kwa mojawapo ya babu au bibi katika ukoo. Katika maneno mengine ni kusema kuwa kuwa matatizo mengi tunayoyaona leo katika familia/koo au jamii zetu chanzo chake ni babu na bibi zetu.
Ndiyo maana mwanzani nikasema kuwa, pamoja na ufahamu wetu katika taaluma mbalimbali kwa kiwango cha juu, lakini ikiwa ufahamu huo hauwezi kufahamu matatizo yanayotutesa katika familia/koo au familia bado shida kubwa. Kwa sababu; sisi wenye ufahamu huu mkubwa wa taaluma hata kama tutakuwa na kiwango kikubwa cha uchumi pasipo kufahamu chanzo cha matatizo haya yalio katika familia/koo zetu ni kazi bure, kwani baada ya muda fulani watoto wetu, vizazi vyetu au hata sisi wenyewe tutajikuta kwenye umasikini na matatizo yaleyele.
Kwa hiyo, ufahamu wetu katika mambo ya taaluma mbalimbali ni chachu muhimu sana kuelekea ufahamu huu mkuu wa matatizo tuliyonayo katika familia/koo.
Kwa msingi huo ni muhimu wanafamilia kujua mambo mbalimbli yafanyikayo katika ibada za matambiko katika familia/koo zetu. Hapa ni lazima kujua historia ya ibada za matambiko, malengo na madhumuni yake, sadaka zake ni za aina gani na kwa nini hizo na sio nyingine, sifa za mtu anaehusika kufanya ibada ya matambiko hayo ni zipi, eneo la kufanyia ibada za matambiko.
Mkazo mwingine katika kuelewa ibada hizi za matambiko unapaswa uwe katika matokeo yake; je athari zake zinaleta madhara gani kwa washiriki katika familia/koo. Uelewa huu ni hatua muhimu kujua matatizo yaliyopo katika familia/koo wako na ni hatua ya kufanya maamuzi na chaguo sahihi katika kuokoa familia/koo wako.
Ufahamu huu unaweza usieleke kwa watu kwasababu madhara ya dhambi ambayo kimsingi ndiyo matatizo tunayoyaona katika familia, koo na jamii zetu hufamba wahusika. Bahati mbaya kwamba, jinsi madhara yake yanavyotupa katika familia/koo ni ya kushangaza sana-sio rahisi kutambua kuwa tatizo hili ni kwasababu ya jambo hili, inasikitisha sana!
Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa, familia/koo nyingi hufanya ibada za matambiko na sisi kama wana familia/koo hushiriki. Lakini jambo ambalo lisilo wazi kwa wanafamilia/koo wengi huwa hatujui malengo na madhumuni ya matambiko haya. Na hapa ndiyo dhana ya TUNAO UFAHAMU inajitokeza. Niseme kuwa ibada hizi za matambiko ni za siri kwa baadhi yetu wanafamilia/ukoo kutafuta mafanikio ya uchumi. Inaweza isieleweke rahisi kwa wengi wetu katika familia/koo, lakini ukitaka kujua ukweli wa jambo hili jisumbue kudadisi juu ya taratibu za ibada za matambiko za kale zilivyokuwa zinafanywa ulinganishe na za hivi leo kwa kuangalia vipengele hivi: Historia ya Ibada za Matambiko, Sifa za Watu waliohusika Kufanya Ibada za Matambiko walikuwa wa aina gani, Sadaka zilizotolewa zilikuwa za aina gani na kwanini hizo tu, Mazingira ambapo Matambiko yalifanyika na Vitu au Vifaaa vilivyotumika. Unaweza kuelewa siri iliyojificha katika matambiko haya tunayoyashiki na kuyafanya katika familia/koo zetu.
Inaweza isieleweke haraka kwako kwamba HATUNA UFAHAMU ingawa hapa sio wote kutegemea na mwelekeo wako uliouchukuwa katika maisha. Pia ifahamike kuwa kwa sababu ya kutokuwa na ufahamu wengi wetu tumekuwa tukishiriki katika ibada za siri na mambo ya siri ambayo ni ausi na chukizo kwa Mungu na kwa sababu hiyo leo hii tuna matatizo makubwa kwenye familia/koo na jamii zetu ambayo yamefifisha au kuondoa kabisa ustawi wetu kiroho na kimwili hadi vizazi.
Tunao uwezo wa kuyashinda haya matatizo kama tukiamua kuujua huo ufahamu kwa kukataa, kuvunja na kufuta mielekeo yetu inayotupofusha.
 
Unataka kutuaminisha kuwa tukiwa na ufahamu wa kiroho tutaepeka matatizo tuliyonayo..? au mimi kichwa maji sijakuelewa.?
 
Miaka ya 60,uchumi,hali yetu turikuwa sawa na Singapore,Korea,China,Leo hii karne ya 21,wenzetu wamepiga hatua kubwa,sana,sisi bado tuko vilevile,
Na hii,sio kwasababu,wao wameacha imani za matambiko,na sisi bado tumezikumbatia,au wao "wamemrudia" Mungu ndio maaana wameendelea,hii sio kweli,huko China,Korea,Singapore,hakuna huu upentecoste unaouhubiri,waliwekeza kwenye sayansi,na tekinolojia,wwliwekeza kwa watu wao,hawa kukaa kanisani kuhubiri injiri,walifanya kazi,
Hizi story kwamba,babu alikuwa mchawi,basi na Mimi nitakuwa mchawi,ni majibu mepesi sana,
Watu wa ulaya,wameitesa,dunia,biashara ya utumwa,mauaji ya wayahudi,lakini ni katika jamii hiyo hiyo watu kama,bill gate,wametokea,hata sisi yupo dangote,
We should not spiritualize our economic problem,tunaitaji sayansi na tekinolojia kufika huko,sio kukesha tukiomba,au kwenda kwa wachungaji feki kuvunja laana,we need to work,
 
Back
Top Bottom