Je, tungefanya quarantine kwenye UKIMWI ungetoweka?

Je, tungefanya quarantine kwenye UKIMWI ungetoweka?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Nimewaza hapa na hizi quarantine. Corona inaweza kuwa imekuja kutufungua macho. Nchi kama Tanzania asilikia kama 5 ya watu wote wan UKIMWI. Mkoa kama Njombe 14% ya watu wan UKIMWI. Ukiona watu mia moja Njombe jua kuwa 14 wana upungufu wa Kinga Mwilini. Hii ni ishu kubwa sana ukizingatia kuwa mortality rate ya HIV/AIDS ni 100% wakati ile ya Corona ni kama 3%.

Wakati UKIMWI unaingia kulikuwa na kampeni kubwa sana dhidi ya unyanyapaa. Naanza kuhisi kampeni ile ilikuwa kutuzuia tusiwaze kuwekana karantini. Ingeonekana tunafanya unyanyapaa mkubwa sana. Lakini hapo hapo mtu wa Kipindupindu, TB, ukoma, na Corona akitengwa ni sahihi tu.

Hivi tungefanya quarantine dhidi ya UKIMWI tungeweza kuudhibiti? Tukifanya sasa quarantine ya wagonjwa wa UKIMWI tunaweza kuudhibiti?
 
Quarantine kwa huu ugonjwa kwa hasa walio na HIV naona kama nikumtoa mtu kwenye majivu nakumuweka kwenye moto
 
Labda useme hawekwe kwenye mji mmoja wao wenyewe waishi huko, wasiruhusiwe kutoka nje ya mji na wengine wasio wagonjwa wasiruhusiwe kuingia.
Yaani waendeshe mji wao wenyewe na hata viongozi wa huo mji wawe ni waathirika.
 
Inategemea na jinsi ugonjwa unavyoambukiza, sasa HIV quarantine ya kazi gani wakati kitendo chenyewe kinafanyika ndani kisiri
Kufanyika sirini kunazuiaje quarantine isifanye kazi?
 
Labda useme hawekwe kwenye mji mmoja wao wenyewe waishi huko, wasiruhusiwe kutoka nje ya mji na wengine wasio wagonjwa wasiruhusiwe kuingia.
Yaani waendeshe mji wao wenyewe na hata viongozi wa huo mji wawe ni waathirika.
Yap kitu kama hicho. Kila mkoa au wilaya unatenga eneo la kuwaweka waathirika. Ingefanyika zamani zile naona kama ingekuwa rahisi na UKIMWI ungetokomea. Lakini hata sasa inaweza kufanyika. Na uzuri huu ugonjwa upo kwa binadamu tu. Ni rahisi kuutokomeza wote.
 
Labda useme hawekwe kwenye mji mmoja wao wenyewe waishi huko, wasiruhusiwe kutoka nje ya mji na wengine wasio wagonjwa wasiruhusiwe kuingia.
Yaani waendeshe mji wao wenyewe na hata viongozi wa huo mji wawe ni waathirika.
Tungewezaji kuwatambua wote ukiwa kitendo chenyewe Cha kupima Ni cha hiari
 
Tungewezaji kuwatambua wote ukiwa kitendo chenyewe Cha kupima Ni cha hiari
Yes kupima ni hiyari lkn wale ambao watagundulika hospitali wapelekwe huko. Halafu kupima sio hiyari Kama unavyodhani, hospitali wanakupima tu wakiona ugonjwa wako haueleweki
 
Back
Top Bottom