Je,Tusherehekee sikukuu?

Kigoma Independent

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
3,519
Reaction score
2,055
Ndugu wapendwa Sikukuu za kidini na Sikukuu nyingine zinazopendwa na watu wengi ambazo husheherekeawa sehemu nyingi za walimwengu Leo,hazikutokana na Biblia.Basi, Sikukuu hizo zilianzia wapi?Fikiria mifano michache:
✓Ista;"katika agano jipya hakuna lolote linaloonyesha kwamba ista ilisherekewa",yasema The Encyclopedia Britannica.Ista ilianzaje?ilitokana na ibada ya kipagani .Ingawa inasemekana kwamba Sikukuu hiyo ni ukumbusho wa kufufuka kwa Yesu,desturi zinazohusiana na Sikukuu ya Ista si za kikirsto.Kwa mfano The Catholic Encyclopedia inasema hivi kuhusu Yule "sungura wa Ista" :Sungura huyo ni mfano wa kipagani na sikuzote huwakilisha nguvu za uzazi.
✓Sherehe za mwaka mpya;Tarehe na desturi zinazohusiana na sherehe za mwaka mpya hutofautiana katika nchi mbalimbali.Kuhusu chanzo cha SIKUKUU hiyo,The world book Encyclopedia inasema:"Mtawala mroma Kaisari Yulio aliteua januari 1kuwa Sikukuu ya mwaka mpya katika mwaka wa 46 k.w.k.Waroma walitenga siku hiyo kwa ajiri ya Yanu, mungu wa malango,milango na mianzo.Mwezi Januari ulipata jina lake kutoka kwa Yanu ,aliyekuwa na nyuso mbili -------------kama ukiangaria mbele na mwingine ukiangaria nyuma ".kwa hiyo sherehe za mwaka mpya zinatokana na mapokeo ya kipagani.
✓Mkesha wa Sikukuu za watakatifu wote("Halloween").The Encyclopedia Americana inasema:"Desturi fulani---fulani zinazohusiana na mkesha wa siku ya watakatifu wote zilizotokana na sherehe za kidini za kiselti za kabla ya enzi za ukristo.Waselti walikuwa na Sikukuu kwa ajiri ya miungu wawili wakuu----mungu just na mungu wa watu .......,ambaye Sikukuu yake ilikuwa Novemba 1,mwanzo mwa mwaka mpya wa kiselti.Pole kwa pole , Sikukuu hiyo ya wafu ikaingizwa katika desturi za kikristo.
✓Sikukuu nyingine; Sikukuu zinazohusiana na kuwatukuza wanadamu na mashirika ya kibinadamu hayampendezi Mungu.
 
Ni Lazima Kila Tulifanyalo Limpendeze Mungu?

Si Udikteta Huo?
 
Si kila kifanyikacho duniani basi kiwe kwenye Bible vingine ni utaratibu tu wa binadamu kitu cha muhimu kisiwe kiovu mbele za Mungu na hapo mi sioni uovu wowote watu wakiadhimisha hizo siku
 
Si kila kifanyikacho duniani basi kiwe kwenye Bible vingine ni utaratibu tu wa binadamu kitu cha muhimu kisiwe kiovu mbele za Mungu na hapo mi sioni uovu wowote watu wakiadhimisha hizo siku
Kama Ni hivyo,unazani Kuna Jambo ambalo binadamu anaweza kulifanya ambalo biblia ailizungumzii na kumpendeza mungu kweli?
 
Kama Ni hivyo,unazani Kuna Jambo ambalo binadamu anaweza kulifanya ambalo biblia ailizungumzii na kumpendeza mungu kweli?
Yapo mengi tu mbona,mfano wewe kuchati unafikiri Mungu kalizungumzia kwenye kitabu chochote cha dini au watu kutumia maroboti kufanya kazi utaanza kuwaza labda wanamkosea Mungu lakini sio kweli kuna mambo mengine tunapaswa kutumia akili tulizonazo za kutambua mema na mabaya
 
Kutengeneza maroboti ni kosa,tena kubwa sana na wanaotengeneza watapata tabuna Sana, kwasababu wanaiga na kukosoa uumbaji wa Mungu,Kwa mfano ilifikia hadi wakati wakataka kutengeneza roboti na kutaka kuliwekea hadi mifumo yafahamu but wakakosa pumzi,je unazani hiyo ni sahihi?,na Kama ni sahihi,je wangeweza wangesemaje kuhusu uumbaji wa Mungu?,je wangeamini Kama Mungu alimuumba binadamu?nijibu.
 
Mmmhhh hapo umeangalia maroboti yanayofanana na binadamu tu lakini kuna maroboti mengine hayapo kimfumo wa binadamu hii ni kutokana na kazi ambayo yametengenezwa kuifanya
Pamoja na hayo ila mi sioni kama kutengeneza roboti ni vibaya kwani yule ni roboti na atabaki kuwa roboti hawezi kuwa binadamu af ukisema kuwa ni kosa kwa sababu wanaiga uumbaji wa Mungu sijui wanamkosoa kwaiyo tuseme na kutengeneza ndege ni dhambi kwa maana binadamu hakuumbwa awe anasafiri angani aliyekuwa wa angani ni ndege(mnyama) ndo maana akapewa mabawa we mkuu huoni kama kuhukumu Hilo kosa kwa upande huo inakuwa sio Sawa maana hii ni teknolojia hayo maroboti yanasaidia kurahisisha kazi haijalishi yana fananaje
 
Umendaika vema

Ila tambua kuwa kila jambo lifanywalo mfanyaji ndio anajua maana yake,
Mfano,

Kuna watu wanasema eti ukiandika Mungu ya herufi ndogo yaani "m" ndogo eti humaanishi mungu huyu tunae mwamudu,
Ila mm nasema nikiandinga mungu au Mungu maana yangu ni ile ile kama wewe unaona tofauti shauri yako

Kuna neno X-mass ambayo watu wengi wanamaanisha christmass,kuna mtu nakwambia eti X-Mass ni ya kipepo,mm nasema shauri yako maana yangu ni Christmass

Narudi kwenye maada

Kama Inst kwa mawazo yako na imani yako ni upagani basi kwa imani yangu akili zangu ni ukristu
Tarehe moja ya Jan kila mwaka mimi kwa akili zangu na imani nasherekea mwaka mpya,kama ww unasherekea miungu wawilili haina shida,

Tatizo ni imani,

Kama unaamini unakula wali samaki wakati unakula wali na picha ya samaki brother,

Kama unaamini new yr ni ya kipagani endelea usiache
 
daaaaahhh" watu wenye imani ya dini mnamatatizo Sana" kama kutengenezwa" maroboti ni kosa" je wazungumzia vipi utengenezwaji" WA magari" .. ndege".meli" treni" etc maana hivyo vyote" vimegunduliwa" baada ya binaadamu kufanya tafiti mbali mbali za wanyama" ... hata maghorofa nayo" ni mfanano WA Miti Mirefu""....
 
Kwa ujumla ndugu yangu alphaking2023,Nadhalia ya teknolojia kwa ujumla aimpendezi Mungu,na ukifuatilia Sana wanasayansi wengi huwa Wana amini kwamba akuna Mungu,na hata ukiangalia moral's decay ambazo zinatokea sasa hivi kwa ujumla utokana na hizohizo teknolojia na ndio huo uwezo wa kufanya hivyo unawapa viburi hasa wazungu kuwa they can do anything like Mungu,kumbe ki nothing tu ko utengenwzaji wa maroboti,magari,ndege na e.t.c kwa ujumla upoteza mantiki ya kwamba Mungu ni muweza wa yote ok.
 
Kwanza kabisa pole ndugu yangu kwa kuandila kwa hasira Sana,
Pili hakuna jina ambalo huandikwa kwa herufi ndogo hasa majina ya pekee Kama Mungu,na ikitokea ukaandika kwa herufi ndogo Hilo jina ujuw kwamba umekosea na ndo mana autakuta Biblia imeliandika kwa herufi ndogo kwa sababu ni lile jina lililo kuu zaidi ya yote,ko takuwa umefanya makosa Kama utaliandika kwa herufi ndogo na Ni kosa kisheria.
Tatu,Kama ukisema Ista au krismas unasheherekea,je kweli vyanzo vyake vinatokana na Kumpendeza Mungu?na je,Biblia inaonyeaha ni halali kuzisheherekea?kwa sababu hakuna msitari wowote ambao unaonyesha hivyo vitu.
Nne, kimantinki sherehe mbalimbali kama,nanenane,sabasaba,muungano, boxing day,mapinduzi,mashujaa na nyinginezo nyingi azipatani na mafundisho ya kweli.
 
Vyote ni batili machoni pa Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…