Je, tutarajie Canal+ Kuanza Kuonesha Ligi Kuu ya Uingereza hivi karibuni?

Je, tutarajie Canal+ Kuanza Kuonesha Ligi Kuu ya Uingereza hivi karibuni?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Je, wataanza kuonesha Ligi Kuu ya Uingereza na au Ulaya hata kwenye nchi za Commonwealth?

Kwa mujibu wa Mtandao wa Mtandao wa SP ni kwamba Mmiliki wa SuperSport, Multichoice, amekubali ombi la ununuzi la Canal+ ununuzi wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 2.9. na kwamba Kampuni hiyo kubwa ya runinga ya kulipia ya Ufaransa sasa itatafuta idhini ya kisheria kwa ajili ya kukamilisha muamala na hatimae kuitwaa mazima multichoice.

Kufahamu zaidi soma: SuperSport owner Multichoice gives green light to Canal+’s US$2.9bn takeover bid

Baadhi ya Mambo muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu hawa wadau wawili wa burudani ya runinga:-
Canal+ na MultiChoice ni watoa huduma wakubwa katika soko la televisheni ya za kulipia za setelaiti kwa bara la Afrika....kila mmoja anawapa watazamaji kitu tofauti kwa suala la ubora wa video na maudhui kama ifuatavyo:-

1. Canal+ :
  • Ubora wa Video: Canal+ kwa kawaida hutoa ubora mzuri wa video, huku vituo vingi vikiwa katika HD (Ubora wa Juu). Wana mkazo mkubwa katika kutoa picha na sauti zenye ubora wa juu, hasa kwa chaneli zao za "premium".

  • Maudhui anayotoa: Canal+ ina nguvu zaidi katika nchi zinazozungumza Kifaransa barani Afrika. Wanatoa aina mbalimbali za maudhui ikiwa ni pamoja na filamu, michezo (hususan soka) na series za TV za kipekee kabisa. Mara nyingi hawa jamaa wao hutoa maudhui ya Kifaransa na filamu za kimataifa zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kifaransa.

2. MultiChoice :
  • Ubora wa Video : MultiChoice, kupitia chaneli zake za DStv, anajulikana kwa ubora wake mkubwa wa video, ikiwa na chaneli nyingi za HD na hata baadhi chaneli za Ultra HD (4K). Uwekezaji wao katika teknolojia unahakikisha kiwango cha juu cha ubora wa matangazo.

  • Maudhui anayotoa: MultiChoice hutoa aina mbalimbali ya maudhui yanayolenga makundi mbalimbali ya lugha na tamaduni katika bara la Afrika. Hawa jamaa wana umaarufu hasa katika urushaji wao mpana wa michezo kupitia SuperSport, chaneli pendwa za habari na chaneli za burudani za ndani ya nchi husika na kimataifa.

Ulinganifu wa hawa jamaa wawili:
  • Watoa huduma wote wawili wanatoa ubora wa video unaoshindana na MultiChoice labda akiwa na faida kidogo zaidi kumzidi mwenzie kutokana chaneli zake za vituo vya HD na 4K nilizoeleza pale juu.

  • Canal+ ni maarufu katika maeneo yanayozungumza Kifaransa, wakati MultiChoice inawavutia watazamaji tofauti zaidi na matoleo yake mengi ya lugha mbalimbali barani Afrika.

MY TAKE:
Take over kama ina ukweli wowote bila shaka utaongeza nguvu ya ukuaji wa burudani Afrika. Ni wakati pia wawekezaji wetu wazawa kv Azam akaingia kwenye huu mtanange ili tuwe na operator wa kiafrika hasa kwenye haki za kuonesha mpira wa bara la Afrika.
 
Mbona huwa wanaonyesha EPL
Wanaonyesha lakini kwa njia za panya, canal Haina usajili huku na Wala hawalipi Kodi, siku ukidakwa na hiko kisimbuzi utanielewa zaidi, kuna kipindi walikua wanavisaka
 
Back
Top Bottom