Je tutaweza kufungua nyumba kwa kutumia ufunguo wa gari?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mkoloni alipofika tu kwetu alikimbilia kuzinyonga mila na tamaduni zetu maana alifahamu mila, desturi na utamaduni ndizo nguvu na nguzo za kila mtu, kila familia, kila ukoo na kila taifa. Hizo ndizo anuani za mawasiliano kati yako, familia, ukoo, kabila, taifa na Mungu wao, ndio ufunguo wa kufungulia na kuingia nyumba ya Baba.

Walihakikisha wanafuta anuani zetu za mawaziliano na Mungu wetu sisi na wakatubadilishia vitasa vya nyumba vya milango ya nyumba ya Mungu wakatupatia fungua za vitasa vyao feki. Ona, sisi walituambia ufunguo ni Yesu lakini wao ufunguo wao ni beberu mkubwa mweupe na mwenye pembe ndefu sana (tambiko).

wakati sisi tuliyafuta matambiko yetu (funguo halisi) wakatupa funguo bandia (Yesu na Mohamed SWA), ambazo ni za watu na mataifa ya mashariki ya kati ya Uyahudi na Uarabuni. ambayo funguo hizi zinafanyakazi vizuri tu ya kufungua mlango wa nyumba ya Baba yao.

Sisi kwetu zinagoma kabisa kufungua vitasa vyao feki. Mataifa yaliyogoma kuzipokea hizi fuguo za vitasa feki yanapiga hatua kama vile India na Hindu yao, China na nyoka wao, Nigeria na kwingine ambako mila zao zina nguvu sana.

Mataifa ambayo hata vazi la taifa hawana wanavaa suliali na shati na kuchomekea na kufunga tai hata kama kuna joto kali, ni wababaishaji tu wanaoibia wanawanchi mali zao na kwenda kuzificha kwa mabeberu tena.

871922cf91e3ecfdb7034f9edb3ad02c.png

Uzi huu umeandikwa na kavulata
 
View attachment 2366132

Uzi huu umeandikwa na kavulata

Mbona ujatupa ufafanuzi kuhusu huyo beberu aliyeonekana kwenye mazishi ya queen
 
Back
Top Bottom