Je, tutegemee Mh Benard Membe kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi kama wengine?

Je, tutegemee Mh Benard Membe kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi kama wengine?

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
4,509
Reaction score
23,653
Habari wanabodi,

Kwa hili vuguvugu na joto la kisiasa linavyoendelea nchini tanzania hivi sasa (Kufukuzwa uwanachama Mh Membe n.k) na sintofahamu za wapinzani kusulubiwa pasipokua na huruma.

Na kwa jinsi tulivyojengewa "MAZOEA" na watawala wetu ya kila ambae haungi "JUHUDI" ataishi kama shetani kwa "KUFUNGWA MDOMO - Kesi za uhujumu uchumi, kupotezwa, kuuliwa, kutekwa, kufungwa, kuhojiwa, kutukanwa, kudhalilishwa, kupimwa mkojo, kufilisiwa, kusulubiwa n.k).

Licha ya mataifa yenye nguvu duniani (Marekani, UK, Canada n.k - Mabeberu) kukemea, kusikitishwa, kupunguza misaada, kuwekewa vikwazo baridi na moto juu yetu tanzania na baadhi ya viongozi vipenzi kwa mkuu.

Je, tuegemee Mh Benard Membe (Jasusi Mbobezi) kufungwa mdomo kwa kufunguliwa kesi zisizo na dhamana au kupotezwa au kutekwa (Kama kina Azory Gwanda, Kabendera, Ben Saanane, Tito Magoti, Mo Dewj, Yusuf Manji, viongozi wa upinzani na wengine wengi)???

Je, tutaendelea na ujeuri wetu wa kutowasikiliza wanaokemea na kuonya???

Mtazamo;

* Tuweke akili zetu sawa kwa huko tunapoelekea, mabeberu kama wataamua kutusukumia janga moja ameizing (Kama vile CORONA VIRUS) nchini kwa makusudi, halafu wakagoma kutupa msaada, basi tutaangamia taifa zima.

* Tuweke "UCHAMA" pembeni kwenye ishu za kitaifa.
 
Hilo neno "kama wengine" nimelipenda sana mkuu wangu!
Hatari, hio "KAMA WENGINE" ni kama hawa hapa viongozi wa Chadema waliochinjwa (Walionyamazishwa) Wilaya ya manyoni.

Ukweli nchi yetu imefika pabaya sana, uchaguzi ukifika inaweza ikawa hatari juu ya hatari.

Halafu utawala upo kimya juu ya haya mauwaji.
tapatalk_1582995525976.jpeg
 
Back
Top Bottom