Je , tutegemee Yanga kupata mapokezi makubwa ugenini kutokana na ukarimu wao wa kuzipokea timu pinzani za Simba katika mashindano ya CAF?

Je , tutegemee Yanga kupata mapokezi makubwa ugenini kutokana na ukarimu wao wa kuzipokea timu pinzani za Simba katika mashindano ya CAF?

mpiga vichwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
2,376
Reaction score
3,811
Naaaam! ni ukweli usiopingika kwamba , timu kutoka nje zinapokuja kucheza na simba katika mashindano ya CAF CL au CAF CC zimekuwa zikinufaika na mapokezi makubwa kutoka kwa Mashabiki wa Yanga wakati mwingine hata viongozi wao.

Aidha, timu hizo zimekuwa zikipewa mbinu mbalimbali na Mashabiki hao ili kuhakikisha zinapata ushindi mbele ya simba katika uwanja wa Mkapa.

Je, kutokana na ukarimu huo , tutegemee Yanga kupata mapokezi makubwa na mazuri ugenini watakapokwenda kucheza mechi zao huko ugenini kutokana na ukarimu ambao huwa wanazifanyia timu hizo?

Ikumbukwe , Yanga wako kwenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa NBC PL hivyo wanayo nafasi kubwa ya kushiriki mashindano hayo musimu wa 2022/2023.
 
Hahaha wacha tuwashukuru watani kwa kuonesha ukarimu wa watanzania kwa wageni hata majumbani "Karibu mgeni, jisikie upo nyumbani"
Ila wana moyo sana maana kila wanayempokea anapigwa na mnyama Simba haha
 
Je kutokana na ukarimu huo , tutegemee Yanga kupata mapokezi makubwa na mazuri ugenini watakapokwenda kucheza mechi zao huko ugenini kutokana na ukarimu ambao huwa wanazifanyia timu hizo?
...Labda watalipwa huu ukarimu, tusubiri muda ukifika tutaona.
 
Timu ndogo kama utopolo huwa zinapokelewa vizuri sababu wenyeji wana uhakika wa kujipigia.
 
Sasa hata wewe mtoa mada unataka wafanyeje...kama mpira hawauwez hata kupokea wageni washindwe?
 
Back
Top Bottom