Kuna mambo najaribu kujiuliza, kwa mwenyeji wa ndanda anaweza kunisaidia, kuna misikiti karibu na shule hiyo labda? wanafunzi (wanaopenda) wanaruhusiwa kwenda kuswali? Na wanaruhusiwa mda gani? kwa sababu tunajua muda wa vipindi mashuleni. na lini?
Ni kweli iko haja ya kuwa na msikiti hapo shuleni? au labda pana kanisa? je kuweka msikiti kwa sababu pana kanisa ndio njia pekee ya kutatengeneza usawa?
Hii ndiyo bottom line kwangu.
Bahati mabaya tabia za binadamu ni ngumu kuzitabiri, unaweza kukuta kwamba kuna katika hao waliogoma kuna ambao hata pangekuwa na msikiti huwa hawaendi na wala wasingekwenda kuswali.
Ukiniuliza mimi shuleni ni mahali mtu amekwenda kusoma, naelewa kila mtu ana dini yake ambayo inapaswa kuheshimiwa na ndiyo maana tukapewa siku ya ijumaa kuwa nusu siku kwa ajili ya hilo, na pia jumapili!
Huwa nakereka sana pale watu wanapoamua kufanya suala la dini kama ni la vikundi! Mmoja mmoja tunafanya mambo ya aibu halafu katika vikundi tunajifanya wamoja na kudai haki bila kujua kuwa hakuna haki iliyo bila wajibu!
Imani yangu ni kwamba, moja, hakuna dini nzuri au mbaya, kwa sababu wengi wa waumini (ukiacha wale ambao labda kwa sababu moja ama nyingine waliamua kubadili) walijikuta kwenye dini kutokana na malezi waliozaliwa wakayakuta. Mbili, dini inapaswa kutufanya tuwe wema zaidi, tupendane zaidi, kwa ujumla tutende matendo mema coz Mungu ni mmoja.