Unajua mitandao mikubwa ya kijamii imekuja duniani kama miaka 15 iliyopita. Bahati nzuri au mbaya tukaichukulia kama vyombo vingine vya habari mfano magazeti, televisheni na redio. Tukatunga sheria za kudhibiti maudhui (Contents) yake huku tukisahau jambo la msingi sana kuliko yote: Mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Instagram, Tik-Tok, Snap-Chat na Telegram haiko kama vyombo vingine vya habari ambavyo huendeshwa na wahariri.
Mitandao ya kijamii hutofautiana kabisa na vyombo katika yafuatayo:
-Mitandao ya kijamii iko kwenye mikono ya ummah (They Belong to public domain),
-Mitandao ya kijamii huwezesha mawasaliano ya papo kwa papo (Enables Prompt and Instantaneous communication),
-Mitandao ya kijamii ni bahari ya mawazo na maudhui isiyo na mwisho (It's an infinite sea of ideas and contents)
-Mitandao ya kijamii kwasababu ya TEHAMA haina mipaka ya kijiografia (ICT enables the Social Media to have no geographical boundaries)
-Mitandao ya kijamii huwakikishia watumiaji kutofahamika kirahisi (Users Privacy is dully guaranteed)
Hivyo mitandao ya kijamii ikiendeshwa na TEHAMA, mbali kabisa na kuwasiliana imetengeneza ulimwengu mpya kabisa ambao sehemu kubwa ya maisha ya wanadamu hufanyika. Naweza kusema kwenye ulimwengu huu mpya (Cyberspace) asilimia 70% ya maisha ya vijana wa leo (millenials) huendeshwa huko: Iwe ni elimu, burudani, biashara, kazi za kiofisi au maisha ya nyumbani. Hivyo katika hii mitandao hutakuta mawasiliano tu, bali ramani nzima ya maisha ya watumiaji(An Entire life Puzzle of Users), mitandao kama Twitter, Instagram, Facebook, nk ni vyombo muhimu sana ambavyo vina nguvu iliyomithirika (They posses an Unprecedented Power).
Sasa palipo na watu wengi hapakosi kuwa na matukio mengi: Hivi vyombo vinaweza kutumika vibaya hata kuhatarisha amani na usalama wa dunia nzima. Wataalamu wa Propaganda wa karne zilizopita kama Sir Alfred Tennyson, George Orwell, Joseph Goebbels na Mao Zedong wangepata vyombo muhimu kaa mitandao ya kijamii basi nadhani wangefanya mambo ya ajabu kuliko hata yale ambayo tunayasoma kwenye vitabu. Mashirika ya kijasusi kama The Gestapo, The K.G.B, The Stasi na The S.S, yangekuwepo kipindi hiki basi nadhani maisha ya mamilioni ya watu wengi yangekuwa rehani.
Kusema kwamba vyombo kama Twitter, Facebook, Instagram, Telegram nk havihusiki sana na maisha ya wanadamu kwasababu vyenyewe hutoa tu Platform lakini maudhui ni ya watumiaji, nadhani tutakuwa tunajidanganya sana na kuna siku tutakuja kuangalia nyuma na kusema laiti tungejua. Hili suala linaathiri maisha ya dunia nzima, hivyo ni lazima dunia nzima ijipange kulikabiri: Tutengeneze sheria za kudhibiti matumizi ya hivi vyombo, tusiwaachie wamiliki kujifanya wanachokitaka (They are in a position of power), tusiziachie serikali zikaamua kujifanyia zinavyotaka na pia tusiwaachie raia watumie wanavyotaka. Mpaka leo hakuna mkataba wowote mkubwa wa kimataifa au kikanda ambao unazungumzia matumizi salama ya TEHAMA na Mitandao ya kijamii. Hili ni ombwe kubwa ambalo inabidi lijazwe na wataalamu hasahasa kutokea Afrika kwasababu sisi ndiyo wahanga wakubwa.
Twitter, Facebook na WhatsApp zinageuzwa kuwa silaha kama ambavyo vyombo vikubwa kama The Washington Post, The New-York Times, The Economist, The Pravda, Radio Free Europe nk vilitumika kuwa silaha za kufanyia uhandisi wa jamii (Weapons of Social Engineering) kipindi cha vita baridi. Nadhani ifike mahali viangaliwe kwa undani na vidhibitiwe, bila hivyo kuna kilio kikubwa sana huko mbeleni.
The Harvard Business Review mwaka jana waliandika Article nzuri sana na kusema kwamba kila mtumiaji wa mitandao ya kijamii anayetumia TEHAMA ni lazima amiliki kifaa maalum ambacho kitakuwa kimesajiliwa na kinafahamika kwamba ni chake kwasababu kitakuwa na saini yake mtu huyu ambayo iko kielekronikali (Virtual Signature). Hivyo hata umiliki akaunti mia ukiandika kitu fulani lazima tutajua wewe ni nani. Lakini wameandika jinsi ya kuzuia uhalifu wa mtandaoni, hawakuandika jinsi ya kudhibiti hawa wamiliki wanaouuza taarifa za watumiaji kwa serikali na makampuni ya kibiashara. Wamiliki wanawajibika kwenye suala za maudhui tu, kitu ambacho mimi nadhani siyo sawa kabisa.