Hili suala la urithishaji limekuwa likijitokeza siku hadi siku na sie wenyewe kwa njia moja au nyingine tume/tuna likubali.
Je unataka kujua ni kwa vipi?
1. Hawa watoto wa viongozi walio madarakani au wastaafu nani huwapeleka kugombea?
2. Hata kama ni kwa nguvu ya Baba zao je hugombea wapi? Na tunao/wanao wapigia kura za ndio/hapana ni sie au kina nani?
3. Je ni kweli hawa watoto wa vibopa hawaziwezi/mamluki katika nafasi hizo, wanabebwa au tunawabeba sie?
4. Tufanyeje sie tuso na nafasi hizo, kwani si watoto wa vigogo au wenye pesa, je tuzidi kuangalia na kuvumilia hali hii?
5. Iwapo hatuna uwezo wa mmoja mmoja, Je? Tuunganishe nguvu ili tumchangie mali, pesa na sera ili aweze kuwashinda tusowapenda?
6. Ipi hatima ya Wagombea wetu masikini baada ya kuchaguliwa, je watabaki kuwa wenzetu na tukajumuika pamoja kama zamani? Au watajitenga na kujificha katika majumba yao?
7. Tukiwa makini hayo yatawezekana lakini je? We uko tayari kugombea/ kuchagua au kuchaguliwa na baadaye kutetea jamii yako ilokuchangia?