Je, ufugaji wa ng'ombe wa kienyeji unalipa?

Kigorohe

Senior Member
Joined
May 21, 2019
Posts
160
Reaction score
255
Habari zenu wana JF,

Nimerudi tena kuomba ushauri wenu kwa sababu palipo na wengi hapaharibiki jambo.

Leo naomba waliowataalam wa ufugaji hasa ng'ombe wa kienyeji waniambi je, unalipa. Mimi kama kijana napenda sana kupambana huku na kule kuhakikisha maisha yanasonga. Nipo Arusha naomba msaada wenu
 
Fuga wa maziwa mkuu na Arusha maziwa hayawezi kosa mteja.
 
Kama unataka ya kunywa nyumbani na salio uuze sawa, ila kama biashara bora hata ufuge machotara, Maana unakuta local anakupa 5ltrs per day while chakula na gharama za muhudumu(cowboy) ni constant na kama ungefuga chotara.
 
Nunua ndama kama 200k wafuge kienyeji kama ulivosema around mwaka unawauza by around 600k.

Mifugo ni utajiri. Nina mpango wa kununua ndama wa 150k each nawaacha kwa bi mkubwa kijjn wawe wanamsaidia kulima na maziwa pia, muda wwte nkihitaji pesa nauza.
 
Mkuu wanalipa sana kwasababu kwa hapo arusha ni rahisu kupata ng'ombe kutoka kwa Wamasai bei rahisi kidogo,

NB. Ng'ombe wa kienyeji ni kwa ajili ya nyama maziwa ni kuwalazimisha, ukifuga kwa wingi ndio matunda utayaona si chini ya miaka 5+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…