Je, Ugonjwa wa Virusi vya Korona vimelea vyake vilitengenezwa au vilitokea tu?

Je, Ugonjwa wa Virusi vya Korona vimelea vyake vilitengenezwa au vilitokea tu?

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
3,443
Reaction score
4,006
Wakuu wenye bongo bobevu,

Hili bandiko limekusudiwa kuuliza wataalamu wabobezi kwamba, mosi,

1. Je, vimelea vya virusi vya Korona vilitokea tu kutokana na nguvu ya asili na mabadiliko ya hali hewa ikiwa na chanzo cha viumbe hai ama mimea au vimetengenezwa na binadamu kupitia utafiti wa utukutu kwenye maabara wenye lengo lolote hasi au chanya?
2. Kwa nini ugonjwa wa virusi vya Korona vilianzia nchini China ambayo kwa sasa kwa kiasi fulani wamefanikiwa kupunguza maambukizi yake?

3. Je, magonjwa yote yatokanayo na virusi huwa yanatokea yenyewe au mpaka utukutu wa binadamu uanzishe?

4.Ni ugonjwa upi utokanao na virusi tiba na kinga ilishapatikana?

5. Kwa nini chanjo ya kupambana na virusi vya aina fulani ni sharti itokane na virusi vinavyobabihiana na hivyo vinavyosababisha binadamu afya yake ikatetereka?

6.Ni kwa kiwango gani tabaka la juu ya anga ya nchi kama Tanzania bado lina utando wa hewa ya oksijeni aina ya 'O3' (Ozone layer) ili kuzuia uchafuzi wa hewa tunayovuta?

7, Kwanini watu wanatoa kampeni ya uvaaji wa barakoa (Face Protective Mask) ambayo kimsingi inafunika mdomo na pua pekee ikiacha wazi macho ambayo ninaambiwa virusi vina nafasi kubwa kumwingilia mtu endapo atakutana na mtu aliyeambukizwa kisha akapiga chafya mbele yake au wakati umebebwa kwenye pikipiki macho yanakuwa hayajafukiwa?

8. Kwanini ugonjwa uliojitokeza mahali pengine na kusafirishwa kwanjia mbalimbali ikiwemo mwingiliano wa binadamu hapa duniani unasababisha mifarakano yakijamii hasa ikichochewa na wanasiasa weney mitazamo tofauti ya kiitikadi badala ya kuwaunganisha ili kupambana nao kwa njia sahihi, wakati sahihi, mahali sahihi na malengo sahihi?

9.Kama wanasiasa na wanasayansi wanaleta misuguano kwenye jamii na tawala za nchi kuhusu namna boar ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO kwanini wapendekeza kila nchi na mtu kutumia njia zilizoainishwa na shirika la afya duniani kama ugonjwa haujatengenezwa Maabara wakati magonjwa mengine wanaridhia kutumia njia mbadala kama njia za kitabibu zinashindikana?

10. Kwanini baadhi ya wanasiasa wanapinga kumshirikisha Mungu kutoa ufunuo wa namna bora ya kupambana na huu wa mlipiko ambao wanautumia kushambulia tawala za nchi zilizoko madarakani kama hawakuutengeza kwa minajili ya kufarakanisha watu na serikali zao?

11. Je, kweli shirika la afya duniani linatumika kutaka kufanikisha kupunguza idadi ya watu walioko duniani kwa sasa kutoka bilioni saba nukta saba (7.7 Bln) na kushuka hadi bilioni nne (4Bln) kwasababu eti ongezeko hilo haliendani na rasilimali zilizopo kwa matumizi yao vinginevyo yanaweza kutokea mauji ya raia kwa kukosa chakula na huduma nyingine za kutosha?

12. Je, mpaka sasa shirika la afya duniani limefanikiwa kupata dawa za kuponya UVIKO na kwanini wanazidharau njia za asili zitokanazo na mimea asili ambayo hata mababu zetu walizitumia hata sasa hospitali hupendekeza wagonjwa kutumia kwa kuwa zinavirutubisho ambavyo havijaathiriwa na kemikali?

WATAALAMU WA TANZANIA na AFIKA MKO WAPI? HIVI NI KWELI NGOZI NYEUSI IMELAANIWA KIASI HAWAWEZI KUFANYA UGUNDUZI?

JITOKEZENI HARAKA MCHUKUE NAFASI YENU

VIONGOZI WA KIROHO HIMIZENI UJASIRI WA KIROHO kwa kuwa kupitia ninyi Mungu aliye hai ndiyo hutoa uponyaji kupitia waganga, matabibu, manesi na wanasaikolojia wanaohimiza kuacha kukata tamaa. Tukabiliane adui asiyeonekana kwa macho ya nyama ila matokeo yake ni sawa na uaharibifu wa nguvu za GIZA.

Karibuni
 
Back
Top Bottom