Ugomvi sio wakutoa matumizi tu ndugu yangu kuna mambo mengi mnaweza kutofautiana kimsimamo na kila mtu akawa anataka msimamo wake ndiyo ukubalike hakuna anayekubali kushindwa hapo tayari ni ugomvi, lakini hauna uhusiano na kununua chakula nyumbani. Kutokuihudumia familia, huwo sio ugomvi ni ushetani unakuwa umeingia kwa kutupiwa pepo au kulogwa na malimbwata ya nyumba ndogo au mpenzi wa nje. Ndugu zangu uchawi upo hata vitabu vyote vya dini vimeandika na kuthibitisha, mtu analishwa dawa anaisahau familia yake hata ndugu zake wa kuzaliwa anawaona kama panya. Familia zinahitaji kumshirikisha Mungu katika kila jambo ili ndoa zidumu bila kuwa na migogoro.